Vita dhidi ya Ufisadi: Tujiadhari na kina Marando!

Nilimsikia siku moja akisema siasa imemfilisi. Nadhani karudi kwenye uwakili wake wa kujitegemea ambao kwa hapa Tz unalipa kwelikweli na kwa muda mfupi tu. Jamaa hawa(Advocates) mimi huwa nawafananisha na waganga wa kienyeji akina Chief Matunge, Prof. Maji Marefu, Sheikh Yahya,...
 

Heshima mbele mkuu Masaki...Kwa masahihisho kidogo ni kwamba Mabere Nyaucho Marando kwa sasa anafanya kazi za uwakili tu...Muda wake wa kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki ulimalizika so si Mbunge kwa sasa...Kimsingi NCCR-Mageuzi ni kama ilikufa baada ya Mrema kuhamia TLP...Na hata huyo Benedict Mutungirehi katika uchaguzi wa mwaka 2000 alishinda ubunge wa Kyerwa kwa tiketi ya TLP(alihamia TLP pamoja na Mrema)..
 
Huyu Mabere Marando alikuwa mwanasiasa machachari sana nchi ya Tanzania ilipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Hivi yuko wapi siku hizi?
Ni nini kimemaliza umaarufu wake katika uwanja wa siasa hapa TZ?

Huyo jamaa ni system tena kamili, machachari yote ya zamani yalikuwa ni mchezo wa kuigiza tu. Yupo kwenye system, sema hana part ya kuigiza kwa sasa.

Ni sawa na wengine wengi.
 
Huyu jamaa amezimwa na siasa za fitina amefichwa kabisa na wanasiasa wa fitina kali ndani ya CCM anatafuta mahala pakutokea.Ila walimmaliza sana enzi zile itabidi asubili sana.
 
cha muhimu ni maneno anayoyasema leo kama ya kweli au si ya kweli. na kama anatoa ushauri tuuangalie huo ushauri kama unaweza kutusaidia au la. ni ushauri wa maana au wa ovyo.
vipi kama kulikuwa na mwizi mtaani kwenu aliyekuwa anakuibia halafu baadae akasema ebanaee, ukitaka usiibiwe basi fanya hiki na kile na wewe ukapima ukaona ni kweli hiyo ni njia nzuri kuzuia wizi baadae. utaukataa ushauri huo? utaukataa kwa sababu umetolewa na aliyekuwa adui yako zamani? ni makosa kukataa ushaur.

well, zamani au sasa marando anaweza kuwa alikuwa au ni mtu wa ccm, ambayo inatuhumiwa kukumbatia ufisad mbalimbali. lakin leo hii marando akisimama na kusema ufisadi wa ccm ulikuwa unaendeshwa na unaendeshwa hivi na vile na ikiwezekana akatoa ushauri jinsi ya kuumaliza, je, tumpuuze hata kama kwa akili ya kawaida ikaonekana ndo njia nzuri?

tusimpuuze. tumsikilize. tupime ushauri huo. kama unafaa utumiwe. kama haufai, upuuzwe.

mwizi akija na kukuambia anakuibia kwa njia hii na ile, hatuoni kuwa hiyo itasaidia kujihami dhidi ya wiz kesho?

mramba, yona, amatus, kweka etc (ni mfano tu, maana mahakama 'haijawatia hatiani'). wakija na kutuhubiria jins rushwa inavyopokelewa, kuombwa na kutolewa, tusiwasikilize? wakitupa somo jinsi ya kudhibiti rushwa tusiwasikilize? tusipowasikiliza tutakuwa tunafanya kosa kubwa.
ni muhimu kuwasikiliza wote na halaf tutafakar. ni vigumu kutafuta suluhisho la tatizo ambalo hulijui vizur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…