Tanzania sio wageni kwa FDI tumekuwa nazo na hazijawahi kuwa na manufaa yoyote.
Kodi ndogo na ajira za kubangaiza hazina maana yoyote.
Tuna hitajika kuwa sehemu ya uwekezaji wowote na sio kuokoteza makombo ya kodi na ajira za kuonewa huruma.
Nchi kama Botswana na nyinginezo zina mifumo mizuri ya uwekezaji ambayo inawanufaisha wananchi na approach ya awamu ya tano ilikua ni kutupeleka huko.
Ila sasa kinachofanyika ni kurudi kule kule Misri ambapo watanzania wanageuka watumwa kwenye nchi yao wenyewe.
Sawa mkuu. Lakini hebu tuwatizame hawa watz kwa undani..
Watz ni liability katika uwekezaji katika nchi yao.. kwa sababu
1. Walio wengi hawana upeo wa kiuwekezaji, wanafikiria tu ajira.. ajira..
2. Watz hawana mitaji na vyombo vya kifedha vya ndani haviko tayari kuwakopesha. Na kutokana na la kwanza hapo juu, mabenki yanaweka riba kubwa kwa sababu risk ni kubwa ukimkopesha mtanzania ambaye hana experience/connections/attitude sahihi katika uwekezaji
3. Ujuzi hafifu.. watz wengi hawana ujuzi (technical skills) karibu katika kila uwanja wa maendeleo, kuanzia kilimo hadi kuchakata chuma.. hii inatokana na sababu za kihistoria.. kwamba mfumo wa elimu uliopo sasa na uliokuwapo toka kale hauna mashiko wala misingi stahiki.. upo kama boshen, ili tu ijulikane watoto wanaenda shule wakati hakuna lolote. Siasa za elimu ya Tz hazieleweki kabisa, ni vigumu kufahamu kama nchi ni kitu gani tunakitaka.
4. Wivu wa viongozi wazawa dhidi ya wazawa.. viongozi wa Tz hawana akili kabisa kwani wao huamini locals wakiwa na pesa basi ni vigumu kuwacontrol. Jambo hili ni kweli kabisa. Sasa kwa vile uongozi wa nchi hii upatikanaji wake ni wa kimichongo na kikashfa hivi, watu wenye pesa na wanaojitambua wasingekubali kirahisi kufanyiwa mambo ya kikhanithi. Kwa hiyo ni sala za viongozi na hila za wazi kuhakikisha watz wanaendelea kuwa mafukara na waendelee kuwa yes men ili viongozi wale kiulaini
5. Watz wengi bado ni mbumbu mbumbu, tena wenye ile mentality ya "hainihusu". Hata katika hali ambayo watz wanakandamizwa, basi wao kila mmoja kwa wakati wake husema hainihusu.. kwa ujumula hii ni akili ya kizembe sana, na kwa sababu imejengeka kwa muda mrefu, basi watz wataendela kuumia kwa miaka mingi ijayo. Sikuamini wakazi wa Kimara walivunjowa nyumba zao tena mchana kweupe na bila fidia na hakuna kilichotokea.. niliumia sana rohoni. Hata kuitisha maandamano, kufunga barabara.. watu waliona powa tu kwa vile hiyo kadhia haikuwahusu.. watz ndo tulivyo.. tunaona powa..
Nikirudi kwenye mada, Mtakatifu Jiwe alitumia udhaifu walio nao watz kufanya alivyofanya. Si kwamba huo ni mwisho, unaona pia aliyemrithi amefanya hivyo.. kuamua kwamba mfanyakazi aongezewe buku 10, hata kama sheria ya Establishment inataka kila mfanyakazi kuongezewa mshahara kila mwaka kuendana na hali ya mfumuko wa bei.
Mwisho, kina Jiwe wataendelea kuwepo, na pengine kuharibu zaidi, kwa sababu tuna style mbovu ya maisha kama watz.
Asantee