Vita kati ya maji ya Kilimanjaro na Maji ya kampuni zingine

Vita kati ya maji ya Kilimanjaro na Maji ya kampuni zingine

Nikipiga Kili zangu hafu ukaniletea maji Uhai, lazima nitapike.

marufuku uhai kuuzwa Bar.

ukiona bar wanauza maji ua Uhai, ukienda jikoni haukosi kukuta mende.

hahahaaa ya kweli hayo prophet!!!??
 
Nimewahi kununua maji ya uhai na nilikuwa na kiu kwelikweli, ile kufungua chupa, harufu niliyokumbana nayo ni balaa!!! Toka siku hiyo mimi na hayo maji uhai hatuivi japo yanauzwa bei poa...
 
hhahaha nimekumbuka kitu
maji ya uhai watu wengi wa Dar wanatumia kwa kuogea wakati ule wa matatizo ya maji
sijawahi kuona mtu anaogea kilimanjaro.
uhai viwango duni.simpo
 
Kusema ukweli mimi nikiyanywa (Uhai) tumbo huwa linaniuma. Nimeazimia kuachana nayo kabisa vinginevyo niwe sina jinsi ya kupata maji mengine na ninywe kidogo tu kutuliza kiu. Angalau CoolBlue na Maji Afrika yana ubora, Uhai ni mabaya sana na yanachakachuliwa mno na kwa ujumla TBS yake ni karibu na sifuli.

Tena nakumbuka kuna wakati kulikuwa na yale ya 50ya kwenye nailoni ,yalishapigwa marufuku kwa ajili ya uchafuzi wa mazingira.Yale maji ilikuwa ukimaliza kunywa na ukaingiza mkono ndani unakuta mtelezo wa ajabu kama mlenda.sijui kama ni kitu cha kawaida lakn mie ilikuwa inanitia kichefu
 
Malalamiko ya huyo jamaa hayana msingi kwa sababu kama ulivyosema kila mtu ana uhuru wa kuchagua product za kuuza sehemu yake ya biashara na inashangaza mtu kubebelea mimaji hadi sehemu hiyo huku akijua kwamba hapo kuna kinywaji kinauzwa. Kwa hili hata angeenda na gold label angefurushwa nayo kama ambavyo mtu angeenda na chakula chake cha kutoka kwa mama ntilia na kuingia nacho hotelini. Mbona hajiulizi kwa nini maji ya Kilimnjaro yalikuwa yanauzwa kwenye world cup Afrika ya Kusini na hakukuwa na hayo maji yake ya Uhai?

Mbona mnamlaumu mleta mada pasipo sababu? Kwenye free market economy ni kosa kubagua bidhaa kwakutoziweka kwenye shelf kama ni uchaguzi basi customers watachagua based on labels. Kama kuna something to do with quality siyo kazi ya suppliers ku control quality na kuweka standards bali ni kazi ya sijui ni kamisheni ama ni nini hapa nyumbani I think foods and drugs ama tbs lakini si kazi ya retailers ama whole sellers. Wao kufanya hizo segregetion ni against the rules na standards za WTO ambapo Tanzania ni signatory. Ni kazi ya fair competition kuregulate hizo behaviours kama kweli kuna hiyo hali lakini kama kawaida governance ni issue hapa nyumbani; utakuta wenye hisa ndiyo hao hao vibosile huko fair competition maana conflict of interests na ethics ni vocubulary zisizokuwepo kwenye dictionary yetu ya governance.
 
Umenena. Baadhi ya sehemu hizo wafanyakazi wameonywa kuwa wakithubutu kuuza maji mengine WATAFUKUZWA KAZI. Ndiyo ukweli huo.
 
Pia tusisahau kuwa Maji kama UHAI nayo yamethibitishwa na TBS.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Labda fair competition washushe quality za product zingine ili zishindane kwa usawa!!!, vinginevyo ndugu yangu biashara ni ubora
 
Kwenye marketing wanasema price inatumika kuonyesha ubora wa bidhaa. Kwahiyo wafanyabiashara huongeza bei ili wateja waamini kuwa bidhaa ile ina ubora. Ninakumbuka bwana mmoja alikuwa ananisimulia kuwa mchele anaouza umetoka katika gunia moja. Yeye kaamua kutenganisha. Mwingine anauza kilo sh 700 na mwingine shs 1000. Lakini cha ajabu ni kwamba ule uliowekea bei ya shs 1000 unanunuliwa kwa haraka saana, kwa hiyo na yeye huchota wa shs 700 na kuweka kwenye shs 1000. Kwahiyo huenda UHAI wamekosea kuyauza maji yao bei rahisi, kwahiyo wateja wanaamini ni quality.
 
Pia kama Kilimanjaro wanahusika kuzuia baadhi ya bidhaa zisiuzwe sehem fulani hapo watakuwa wanavunja masharti ya ushindani huru. Itakumbukwa TBL walipigwa fine kwa hili. Ishu hapa ni nani asiyetaka bidhaa ya mwenzake iuzwe. Je, ni Kilimanjaro au mtu mwenye eneo lake la bidhaa!
 
Mbona mnamlaumu mleta mada pasipo sababu? Kwenye free market economy ni kosa kubagua bidhaa kwakutoziweka kwenye shelf kama ni uchaguzi basi customers watachagua based on labels. Kama kuna something to do with quality siyo kazi ya suppliers ku control quality na kuweka standards bali ni kazi ya sijui ni kamisheni ama ni nini hapa nyumbani I think foods and drugs ama tbs lakini si kazi ya retailers ama whole sellers. Wao kufanya hizo segregetion ni against the rules na standards za WTO ambapo Tanzania ni signatory. Ni kazi ya fair competition kuregulate hizo behaviours kama kweli kuna hiyo hali lakini kama kawaida governance ni issue hapa nyumbani; utakuta wenye hisa ndiyo hao hao vibosile huko fair competition maana conflict of interests na ethics ni vocubulary zisizokuwepo kwenye dictionary yetu ya governance.

Sasa ndugu yangu kwenye free market unalazimishwa na sheria kuweka bidhaa ambazo haziuziki wakati wewe unachofanya ni biashara na sio maonyesho ya bidhaa? hebu nijuze hapo inakuwaje
 
siku hizi kuna maji ya Afya jelo tu unapata lita moja safi kabisa,maisha yanasonga
 
Maji ya Kilimanjaro yanakubalika sana , nyanda za juu kusini yapo sana ,ila maji ya nyanda za juu kusini hayafiki moshi

Sijawahi ona maji ya ,dew point ,mkwawa, Mbeya drop ,yale ya sumbawanga Moshi huwa yanaishia Dodoma tu
 
Natumaini wengi wenu mtakuwa mmegundua hali ambayo si nzuri katika biashara ya ushindani kati ya maji yenye chapa ya KILIMANJARO na maji kama UHAI na mengineyo.

Hali iliyopo ni kuwa katika sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam kama vile Baa maarufu mbalimbali, Kumbi za Starehe, Club za Usiku, Mahoteli, Migahawa mbalimbali pamoja na mikutano na semina mbalimbali utakuta sehemu zote hizi maji yanayouzwa ni ya KILIMANJARO. Binafsi nimeishazuiwa kuingia na maji ya UHAI katika baadhi ya sehemu hizi kwa kuambiwa kuwa maji hayo hayaruhisiwi kwa maelezo kuwa maji yanayoruhusiwa ni ya KILIMANJARO tu? Je hii ni haki? na Je FAIR COMPETITION COMMISSION wanalijua hili? na kama wanalijua hili tatizo, je ni hatua gani wamechukua ili kuleta usawa katika ushindani wa biashara hii ya maji ya kunywa?
KWANINI UENDE NA KINYWAJI CHAKO SEHEMU AMBAPO WANAVINYWAJI KAMA HIVYO? LAWAMA ZINGINE HAZINA MASHIKO.

MI KWENYE KAGROSARI KANGU UJE NA BIA MKONONI WAHI HUKALII KITI
 
Mimi ni mnywaji mzuri wa maji, kwa siku lazima ninywe sio chini ya 3 litres kuna vitu nime observe ktk mjadala huu
1.Quality
Maji ya kilimanjaro wakati wanaanza uzalishaji walikuwa wana ya extract kule kule Moshi, lakini demand ilivyokuwa kubwa dsm na mikoa mingine + ushindani wa maji ya dsm ambayo gharama za usambazaji zilikuwa ndogo ikabidi waanze extraction ya maji dsm. Na hapo ndipo walipouwa quality ya maji ya Kilimanjaro. Kwa mtu mzoefu wa maji kwa hivi sasa maji ya kjro na uhai hayana tofauti yoyote ukiacha mazoea ya wateja na branding/packaging ya kjro ilivyo nzuri. Nakumbuka maji ya kjro in quality yalikishindana na Africa na Cool Blue

2.Pricing
Kuna watu huthaminisha vitu kwa kuangalia bei. Kilimanjaro amefanikiwa watumizi wengi wa Kilimanjaro hujisikia wanapo ya tumia maji hayo kwa sababu za hisia zilizojengeka kuwa vitu vya bei chini quality yake iko chini kitu ambacho si kweli KILA MARA
Hapo hapo kwenye Pricing SSB yeye mbinu yake ni ile ile ya Bei chini ili ufanye mauzo makubwa kwa watu wengi. Lakini na yeye kuna maji mengine yamekuja ni mazuri kuliko Uhai, kuliko Kjro kama Masafi na Afya na yanauzwa bei chini sana lakini hajashusha bei ili kulinda jina kama anavyofanya Kilimanjaro

3.Contents
Hizi bidhaa zote zimepitishwa na TBS. Tunaposema haya maji ni mazuri haya ni mabaya tunatumia vigezo gani. Utakuta wengi wetu tunaangalia ladha. Kuna vitu kama PH, Chlorine nk vinamatokeo gani ktk afya zetu ?

4.Kuchakachuliwa
Hamna mtu anaetaka bidhaa yake ichakachuliwe. Bidhaa kama Uhai ni rahisi kuchakachua kwa sababu ya wider distribution Channel yake na aina ya wateja walengwa na maeneo husika. Kwa Cool Blue ni kitu kigumu kwa sababu ina aina ya wateja ambao wako sensitive in quality na hayapatikani Kila sehemu, Lakini hata hayo wajanja wakiyataka wanazalisha

5.Uthubutu wa Kujaribu
Watanzania hatuna tabia ya kujaribu brands nyingine
Watu tushacrem kwamba maji ni Uhai au Kjro baaaasi
kuna brands kama
1.Afya
2.Dasani
3.Cool Blue
4.Masafi
5.Ndanda
6.Lulu
7.Dew nk nk nk
Hii inatunyima fursa ya kuonja vitu vingine vitamu zaidi kwa bei rahisi zaidi

Regards
 
Back
Top Bottom