Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,501
Nimefika Dodoma tangu wiki iliyopita mwanzoni na nimekuwa nafuatilia mwenendo wa bunge la katiba. Watu wamekuwa wakijiuliza ukimya wa chenge kuthibitisha kutaka kugombea uenyekiti wa bunge kama Samwel Sitta alivyoeleza bayana.
Kinachirndelea hapa ni kwamba sasa CCM wamekuja na plan B ya kutokumsimamisha Chenge na badala yake Dr Migiro ndie asimame kutaka uenyekiti kupambana na Sitta.
Sababu kubwa ni kwamba Chenge ndie amehusika kuandika rasimu mbadala ya katiba na hivyo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuielezea maudhui yake na CCM imeona asiwe mwenyekiti ili aweze kuisimamia rasimu mbadala ya CCM. Hapo ndipo wameona wamsimamishe Dr Migiro.
Ninapoandika hapa, CCM wabunge wake wanakutana saa kumi kamili leo jioni hii kupitisha azimio hilo licha ya kwamba kuna kundi kubwa linamtaka Sitta toka ndani ya CCM na wameapa hawatakubali kuburuzwa. Sitta na wenzake wanaendelea na kampeni na kufukia mashimo kuwa kumpa sitta uenyekiti ni ushindi kwa upinzani na wanaopenda haki walio against misimamo ya kichama.
Lakini upinzani nao unataka kusimamisha mgombea wao wa uenyekiti licha ya kumuunga pia mkono Sitta.
Nitaendelea kuwaeleza kitakachojiri katika party caucus ya CCM kama nikipata ukweli wa kilichojadiliwa na hata kinachozunguka duru hizi za uchaguzi wa mwenyekiti wa bunge la katiba. Kwa sasa tambueni kuwa sio Chenge vs Sitta tena bali Dr Migiro vs Sitta