Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Vita Ukraine Haiwezi Kuisha kwa Kuipuuza Urusi, Jumuiya za Kimataifa Zitambue Hilo

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Edorgan akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin jijini Moscow
MSAIDIZI Mkuu wa Rais wa Uturuki amesema kuwa jumuiya ya kimataifa haiwezi kumaliza vita nchini Ukraine kwa kuipuuza Moscow.
Amesema hayo wakati Erdon na Putin wakijiandaa kukutana, katika mkutano wa ngazi ya juu unaokuja baada ya Uturuki kusaidia kupata makubaliano ya kurejesha mauzo ya nafaka ya Bahari nyeusi ya Ukraine ambayo ilikuwa imezuiliwa na uvamizi wa Urusi.
Mkurugenzi Mkuu wa mawasiliano wa Rais wa Uturuki Fahrettin Altun, ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba makubaliano hayo yanathibitisha mafanikio makubwa ya Uturuki katika juhudi za kuirejesha amani kati ya Ukraine na Urusi huku akikosoa nchi nyingine zinazochochea vita kuendelea.


Uturuki imekuwa ikijitahidi kushiriki katikakutatua mgogoro kati ya Urusi na Ukraine
Kiongozi huyo wa Uturuki alinukuliwa akisema:
“Ukweli ni kwamba baadhi ya marafiki wetu hawataki vita iishe wanamwaga machozi ya Mamba, Jumuiya ya kimataifa haiwezi kumaliza vita nchini Ukraine kwa kuipuuza Urusi, Diplomasia na amani lazima vitawale.”


Uturuki imeshauri ili vita kati ya Urusi na Ukraine iweze kutamatika basi kuna kila sababu ya kutoipuuzia Urusi katika majadiliano ya kidiplomasia
Alimaliza kwa kusema kuwa baadhi ya Watu walikuwa wakijaribu kudhoofisha juhudi za Uturuki bila mafanikio, lakini hakutaja watu hao ni akina nani.
Ikumbukwe kuwa katika siku chache zilizopita Uturuki imesaidia katika kusainiwa kwa Mkataba mpya Mjini Istanbul Unaoiruhusu nchi ya Ukraine kuuza nafaka yake nje ambapo Meli ya kwanza kutoka Ukraine ikibeba mahindi imeelekea nchini Lebanon.
Vita Ukraine Haiwezi Kuisha kwa Kuipuuza Urusi, Jumuiya za Kimataifa Zitambue Hilo
MSAIDIZI Mkuu wa Rais wa Uturuki amesema kuwa jumuiya ya kimataifa haiwezi kumaliza vita nchini Ukraine kwa kuipuuza Moscow. Amesema hayo wakati Erdon na Putin wakijiandaa kukutana, katika mkutano wa ngazi ya juu unaokuja baada ya Uturuki kusaid