Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?



Most of this is rubbish; hasa hiyo uliyopigia rangi. Mambo ya kijeshi yanatakiwa yaripotiwe na watu waliokuwamo jeshini siyo waliosikiliza hadithi. Tangu vita ile inaanza hadi inakwisha Nyerere hakuwahi kusafiri nje ya nchi! alitumia muda wote Dar es Salaam wala hakwenda hata Butiama kwenye mapumziko ya yake ya krismas kama ilivyokuwa kawaida yake. Ni kweli kuna ndege zetu zilitunguliwa Musoma kwa kuingia katika anga lile bila taarifa kwa vile zilitakiwa zitue Mwanza lakini kutokana na protocol za airport wakalazimika kwenda Musoma ambako Kikosi cha Kiabakari kilikuwa on the alert muda wote kwa vile Amini aliwahi kuahidi kuwa angekwenda kupiga Butiama. Lakini hayo yalitokea katikati ya vita yenyewe wala siyo mwanzo wa vita kama unavyosoma hapo. Ilitokea wakati wa wa mapambano ya Lukaya wakati jeshi letu lote limeshaingia Uganda. Je hiyo Batallion moja ya Msumbiji ilikuja kuuangana na brigedi gani wakati brigedi zetu za vita zote zilishaingia kwenye theater? halafu watu wanasema batallion wakati jeshi letu lilikuwa linapigana kwa division! Upuuzi kabisa
 

Kaka Jeshi ni taasisi kubwa, yenye watu wengi na mambo mengi huwezi kujua yote.

Mimi nina source za Wanajeshi waliopigana hiyo vita wanasema wazi walipigana bega kwa bega na askari kutoka Msumbiji.

Nimekuwekea na source ya kitabu cha waandishi wa habari waliokuwa msitari wa mbele waliokuwa embedded katika majeshi yetu, tena kitabu kilichochapwa na kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na serikali ya Tanzania Publishing house

Hata hicho kitabu unakataa account yake, wakati kimehaririwa na kupitishwa na serikali ndo maana kikaruhusiwa kuchapwa nchini ktk kampuni hiyo ya serikali.

Tukubaliane tu, si kwa sababu wewe ulikuwa hujui kama hao askari wa msumbiji walishiriki hiyo vita basi imaanishe eti hawakuwepo.

Kiufupi ni kuwa source zangu zinaniambia walikuwepo, na pia accountza wengine mfano huo wa kitabu nilichokwambia pia zinathibitisha uwepo wao.

Kaka usiwe mbishi, ukiwa jeshini haimaanishi unajua yote yanayoendelea katika uwanja wa mapambano!. Endelea kutafuta taarifa zaidi utazipata tu!

Kufanya alliance siyo udhaifu, ni moja ya strategy ya kijeshi, tukisema kuwa tulifanya alliance na Msumbiji kwenye ile vita haimaanishi tunalidunisha jeshi letu, bali tunaeleza ukweli wa hali katika uwanja wa mapambano
 
Mengi uliyoandika ni sawa, lakini conclusion zako siyo kweli. Kitabu unachoquote sidhani kama kimepitia peer review yoyote kama siyo collection ya hearsay tu. Jana hapa nimekosoa kitabu kingine ambacho nacho kimeandika hearsay pia kuhusu jeshi letu huko Seychelles. Kuna vitabu vinavyoandika hisia za mwandishi na kuna vinavyoandika ukweli wa mambo nje ya hisia za mwandishi; cha kwako ni kile chenye hisia za mwandishi. Ukiweza mtefute Brigadier General Ben Msuya umwulize, kwani yeye ndiye aliyeteka jiji la Kampala, mwulize kama hayo ni kweli; bado yuko hai na huwa anaruhusu interviews.

Kinachonishangaza ni pale unapozungumza msaada wa batallion moja kwenye jeshi lililokuwa na divison tatu; kuna vitu vingine huhitaji kuambiwa, viko obvious sana
 

Kaka Jeshi ni taasisi kubwa, yenye watu wengi na mambo mengi huwezi kujua yote.

Mimi nina source za Wanajeshi waliopigana hiyo vita wanasema wazi walipigana bega kwa bega na askari kutoka Msumbiji.

Nimekuwekea nw source ya kitabu cha waandishi wa habari waliokuwa msitari wa mbele waliokuwa embedded katika majeshi yetu, tena kitabu kilichochapwa na kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na serikali ya Tanzania Publishing house

Hata hicho kitabu unakataa account yake, wakati kimehaririwa na kupitishwa na serikali ndo maana kikaruhusiwa kuchapwa nchini ktk kampuni hiyo ya serikali.

Tukubaliane tu, si kwa sababu wewe ulikuwa hujui kama hao askari wa msumbiji walishiriki hiyo vita basi imaanishe eti hawakuwepo.

Kiufupi ni kuwa source zangu zinaniambia walikuwepo, na pia accountza wengine mfano huo wa kitabu nilichokwambia pia zinathibitisha uwepo wao.

Kaka usiwe mbishi, ukiwa jeshini haimaanishi unajua yote yanayoendelea katika uwanja wa mapambano!. Endelea kutafuta taarifa zaidi utazipata tu!
 

expand...
Tunaweza kuwa na Dividision tatu lakini tukapata aina fulani ya askari tunaowahitaji kwa wakati huo. Usidharau hata role ya mtu mmoja katika uwanja wa mapambano, Mtaalamu mmoja wa mitambo kadha wa kadha anaweza kuwa na faida kubwa sana kijeshi.

Wewe unasema niulize askari, lakini nakupa maelezo ya Askari wetu aliyekuwa na hao askari wa msumbiji katika uwanja wa mapambano hutaki kukubali.

HHapa Cha kufanya ni wewe kuendelea kuuliza source tofauti tofauti, ipo siku utafanikiwa kupata wale waliokuwa nao watakueleza!.
 
Sisi tulikuwa tufundisha jeshi la msumbiji; tuwaombe nini wanafunzi wetu? Kuna hii hadithi ya kwamba walikuwa wanazijua BM40 kuliko watanzania jambo ambalo halina ukweli wowote. Kanali Kotta alikuwa ni mtaalamu wa mitambo hiyo ya long range gun artilleries na Howitzers kama ulikuwa hujui.

Siwezi kuuliza watu wengine kwa sababu nilikuwa ndani ya saga lenyewe, hao unaowauliza labda nao ni wa kusimuliwa.
 

Kaka soma New York times ya mwaka 1982 ikielezea Kuhusu Tanzania kuisaidia Msumbiji katika vita vyake vya uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe na pia ikielezea Msumbiji nao kutusaidia kwa askari kwenye vita dhidi ya Amin.

Hiyo habari unaweza kuisoma kwenye archives za Newyork Times hapa:

TANZANIAN MILITARY ADVISERS WILL BE SENT TO MOZAMBIQUE
 
Unarudia yale yale ninayokataa; New York Times hawakuwa kwenye theater ile, tafuta waliokuwa kwenye theater yenyewe wakuambie. Vita ile ilikuwa ni wakati wa vita baridi ambapo Tanzania haikuwa na uhusiano mzuri kabisa na Marekani, kwa hiyo hao New York Times nao ni watu wa kusimuliwa tu kwani hawakuwapo uwanjani.

Sijakataa kupata misaada wa hali na mali, ila ninakataa msaada wa kueletewa wapiganaji. Tanzania ilikuwa na wapiganaji wengi sana tena mahiri sana kuliko unavoaminishwa; katika vita ile tulitumia kama nusu tu ya mabingwa wetu wa vita. Yaani kama hujui kuwa sehemu kubwa ya ufanisi ulioleta uhuru wa msumbiji kupatikana ni kutokana na jeshi letu bali unaamni kuwa wao guerrillas walikuwa bora kuliko sisi; ni vigumu kupokea ukweli ninaokwambia. Nitakuelewa kwa upungufu huo.
 

Hata hao waliokuwepo kwenye vita wamenithibitishia, na hili nimelieleza sana Je nao pia hutaki?
 
Hata hao waliokuwepo kwenye vita wamenithibitishia, na hili nimelieleza sana Je nao pia hutaki?
Mimi nimekuambia nilikuwapo; sikusimuliwa. Je ni nani wa kumauanini, aliyesimuliwa au aliyekuwapo. Halafu vile vile ni wazi hujui ukubwa wa jeshi letu wakati huo; yaani unaongelea batallion moja kutoka Msumbiji wakati sisi tulikuwa na batallion mbili huko huko Msumbiji na batallion nyingine kule Zimbabwe wakati huo. Usikariri mambo, open your mind utafuta habari harafu uunganishe mwenyewe. Jiulize mambo mawili;

(1) ile batallion tuliyoletewa na msumbiji walikuwa na miili ya chuma kuwa hakuna hata mmoja wao aliyejeruhiwa au kuuwawa. Kama baadhi yao walikufa au walijeruhiwa, je kumbukumbu yao iko wapi?

(2) Je ni kweli kuwa Tanzania hatukuwa waungwana kiasi kuwa baada ya vita hatukututoa shukrani yoyote kwa wapiganaji hao waliotusaidia; yaani sisi ni watu wa ajabu namna ile?
 
Yaap!!!.Nimekuelewa mkuu.
 
Hahahaha, Mkuu hii JF ya sasa si ya km kipindi kile
 

(1)Kwenye ishu ya kufa kuna majibu yote matatu, ama kuna waliokufa, au hawakufa yote yanawezekana, Mathalani Tulikuwa na Wanajeshi zaidi ya 40000 kwenye uwanja wa mapambano askari tuliopoteza hawakufika hata 1000, which means survival rate ilikuwa ni kubwa!.

(2) Haukuwa peke yako vitani, tena wewe ulikuwa askari wa akiba kama ulivyosema huko awali, hauna uhakika wa nini haswa kilitokea msitari wabele. Waliokuwa na hao wasumbiji kwenye units zao Wanakiri kushirikana nao, nashangaa ushuhuda huu huutaki!, Kila saa unaukwepa ushuhuda huu

(3) Ishu ya askari wa Msumbiji toka mwanzo ilikuwa clouded na secrecy, hii ni kwa sababu Nyerere hakutaka hii vita ionekane as if ni ya Afrika nzima, hakupenda Afrika idhani Tanzania inatumia position yake ya frontline state kujisaidia kwenye vita zake yenyewe dhidi ya member mwingine wa OAU, Hata hivyo hakuna siri duniani!.
 
Nakukubalia point ya pili, ila ile ya kwanza na ya tatu ni pure speculations; hazina ukweli wowote na haziwezi kuthibitishwa.
 
Afande umeshaambiwa ilikuwa siri kubwa, na wewe ulikuwa afande wa ngazi za chini na vigumu sana kwako kupata siri zote za jeshini na mipango ya vita,kitu kingine ni uzalendo wako na nidhamu propaganda za enzi hizo zikiongozwa na RTD ambacho ni kitu cha kujivunia kwa kazi yako.Kusema Tanzania ilipewa battalion na Msumbiji haina maana kuwa Tanzania na wewe mwenyewe msingeweza kushinda vita.JF ni uraiani siyo kambini na tutakupinga kwa hoja na ushahidi wa source za habari ambazo baada ya miaka wazee wengine wanaamua kuziachia tu kwani hazina madhara yoyote,sina uhakika kama unaficha kwa makusudi au ni kweli una uhakika 100% na kitu unachopinga.Endelea kushusha madini tufahamu wapi tulilishwa matango pori na RTD.
 
Hapana mzee; nilikuwa niko COMMs ya Brigade ya Magharibi , na nilikuwa kati ya vijana tuliokuwa tunakusanya habari za kupeleka ofisi ya Brigade Coommander kila siku kabla hajaandika oda yake ya siku; wenzagu walioendelea na jeshi walifikaia kuwa majenerali na makanali. Nilikuwa napata habari nyingi sana kuliko hata maluteni kanaili wakati huo; sivyo unavyodhani. Nliachana na mambo ya kijeshi takriban miaka 35 iliyopita, na niliondoka Tanzania zaidi ya miaka 25 iliyopita, kwa hiyo sina cha kuficha wala cha propaganda. Ninaandika yale ninayojua kikamilifu, mengine ambayo huenda bado ni classified kuhusu njia tulizopitia kuingia Uganda.
 
Asante sana Mwalimu kwa elimu. Kumbe Urusi huyu tunaejitapa kuwa alikuwa ni mjamaa mwenzetu, kumbe ashawahi kumsaidia adui yetu. Najaribu kuwaza ingekuwaje kama Urusi angeendelea kutoa support kwa Uganda kwa kipindi chote? Pengine historia ingekuwa tofauti sana.
 
Kiuhalisia ile vita haikuwa na Ulazima

Watanzania walikufa wengi sana kuliko Waganda.

Ukikutana na wanaoijua ile vita vizuri watakueleza.
Vita ilikuwa ya ulazima kwani Amin alijua Tanzania awamuwezi kwakuwa alikuwa na vifaa vya kivita kuliko sisi!nakwakuwa alidhamilia kuchukua kagera yote vita ilikuwa aihepukiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…