Mwaka 1978 Msumbiji ilikuwa na miaka minne au mitano tu ya uhuru na ilikuwa bado inaitegemea sana sana Tanzania kiulilinzi katika kupambana na uvamizi kutoka Rhodesia na South Afrika. Kulikuwa na askari wengi wa Tanzania waliokuwa wakiisadia Serikali ya Samora dhidi ya mashambulizi hayo, na vile vile katika kufundisha jeshi lake. Msumbiji hawakuwa na jeshi la kuja kusaidia Tanzania hata la mtu mmoja tu.