Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Two of my uncles participated in that War from day 1 and they share the same stories of what happened during that war. Therefore it is the TRUTH you can take it or leave and formulate your own truth.
Muwe mnatutafsiria kwa Kiswahili!
 
That’s you opinion but you were not there when my Uncles shared their stories about what happened during that war.

I don't buy this pal.
Its all made up
 
Vita ni kitu kibaya sana japo story zake huwa za kusisimua.
Ni kweli vita ni mbaya sana maana inaleta huzuni kwenye familia nyingi inaleta Umaskini kwenye Taifa hata familia watu wanakufa na wengine wanaporudi au wanapokuwa vitani wanapata matatizo ya kisaikolojia na wanakosa msaada huvyo wengi hupoteza maisha na kuacha familia zikiwa kwenye shida lukuki.
 
Vita ni kitu kibaya sana japo story zake huwa za kusisimua.
Vita siyo lelemama, tena afadhali siku hizi kuna GPS. Wakati huo makamanda wetu walikuwa wanaongoza vikosi kwa kutumia ramani, rula na compass tu. Mojawapo ya mafunzo ya makamanda wakati huo ilikuwa ni map reading: kwa hiyo hakuna kamanda wa jeshi ambaye alikuwa hajui kusoma grid reference, magnetic variation, contours na kutumia namba hizo kupanga ruti. Wakati mwingine makamanda walikuwa wanakutana na vikwazo kuwa ramani haikuonyesha chaka zito lisilopitika ambalo sasa wamekutana nalo kwenye ruti zao lakini wanalipangua. Halafu sehemu kubwa ya mapigano yale yalikuwa ni ya kutembea kwa miguu maporini.

Niliandika sehemu nyingine kuwa vita ni mapigano siyo ya kutupiana ngumi bali ni ya kurushiana risasi za moto na mizinga na vile vile kutegana mabomu njiani. Chochote kati ya hivyo kikikukuta hakikuachi kama mwanzo; ama utakufa, au utapoteza viungo kadhaa kwenye mwili wako. Ni bahati nzuri sana sehemu iliyokuwa na resistance kubwa dhidi ya jeshi letu ilikuwa ni huku maeneo ya kusini tu. Baada ya Colonel Msuya kuteka Kampala, kaskazini ya Kampala hakukuwa na resistance kubwa tena kwani askari wengi wa amini walikuwa wakikimbilia ama Sudan au Zaire. Askari wetu wengi waliofariki katika vita ile ilikuwa ni kwenye mapambano ya mwazo pale mto Kagera, na kwenye meneo ya Masaka, Mbarara na kidogo sana (huenda wasisozidi 10) kule maeneo Kasese. Casualty report ya jeshi letu lilipoingia Kampala ilikuwa pia ni ndogo sana.

Jeshi liliporudi, kulikuwa na vilema kadhaa ambao Nyerere aliahidi kuwa watatunzwa na taifa, ila sijui kama hali zao zilendeleaje. Kaka yangu ambaye alikuwa frontline kwenye kikosi cha mizinga sasa hivi yuko hoi bin taaban huko kijijini akisumbuliwa na uzee na ufukara, mimi huwa nampelekea allowance ya kama dola 300 kwa mwezi ili alipe bili zake. Rafiki zangu tuliokuwa nao reserve pale brigade ya faru wakamua kuendelea na jeshi baadhi yao bado wako jeshini. Wawili ni majenerali kwa ngazi tofauti, mmoja alikuwa Luteni kanali JKT ila akapata msukosuko fulani ya ufisadi ambao mahakama iliimkuta hana hatia, ila akaamua kustaafu mapema. Mwingine alikuwa Kanali wa Air Force (huyu nilisoma habari zake kama miaka kumi iliyopita alipomtolea bastola mfanyakazi wa kampuni ya kupaki magari ambaye alikuwa ameweka chain ya kulock gari yake akimtaka alipe ushuru wa parking katikati ya jiji) na mwingine alikuwa Luteni Kanali wa Infantry lakini leo sijui wote hao wawili wako wapi kwani sijapata habari zao kwa muda mrefu sasa, nadhani wameshastaafu. Ninaojua kuwa bado wako active ni wale majenerali wawili ambao habari zao bado zinandikwa magazetini.
 
Jana wakati naangalia TBC Kwenye sherehe za Mashujaa zilizoongozwa na Rais nilipatwa na masikitiko makubwa sana hasa nilipouona ule Mnara wa MASHUJAA wa vita vya Kagera niliwakumbuka sana wapiganaji wenzangu waliopoteza maisha yao wakiwa mstari wa mbele wa mapambano ya kuuondoa Utawala wa Nduli Idd-Amin wa Uganda.

Niliwakumbuka askari 25 waliokufa wakiwa kwenye platoon yangu niliwakumbka mmoja baada ya mwingine na nilisema MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA LENGO NA NIA YETU ILIKUWA NI MOJA TU KUILINDA HADHI YETU YAANI NCHI YETU.

Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa NHN 66482612.

Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea station ya ISAKA-Kahama.

Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978 Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234 Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa Mapambano 03-11-1978 Mchana

Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi niliitwa na Major mmoja kuwa nichukue askari wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.

VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-
1. Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia mpaka na Rwanda na Zaire.
2. Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3. Brigadier Marwa alielekea Masaka
4. Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika na majeshi yetu kujipanga vile.

KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN

Baada ya majeshi ya Amin kuchukua eneo la Mutukula, walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya Magharibi wakati huo alituma Battalion moja kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi wakati wa usiku kusudi wakapambane na wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo, wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa askari. ..bahati mbaya sana tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele kitendo hicho cha kurudishwa nyuma kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel (wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....

Baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid aliondolewa from front line kama ilivyokawaida ya war plans...maana kamanda aliyepigwa hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi wapi alikosea.

Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujeruman na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T 55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana kuliko sisi.Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika 25 tu.

VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE

Baada ya mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale askari wa Amini walikuwa pale Mutukula.

Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion) walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti pale Masaka ambapo Brigadier Marwa alikuwa kajichimbia.

Wakati Amin bado anafikiria afanyeje kuhusu vipigo hivi vya Masaka, Mbarara na Mtukula, akapewa taarifa nyingine kuwa kulikuwa na kipigo kingine kimeanza kutokea Kasese kuelekea Kampala; hiki kilikuwa ni kipigo cha Brigadier Walden. Basi kuanzia hapo ndipo vita ile ilipoanza kupendeza kweli kweli kwa majeshi yetu,. Walianza kuwabomoa majeshi ya Amini yaliyokuwa miji hiyo huku yakiayaacha yale ya Mtukula pale pale na bendera yao ili wajifie wenyewe kwa kukosa supplies kwa vile walikuwa hawapati chakula wala msaada wowote kutoka ndani ya Uganda tena.

Baada ya kugundua kuwa kuwa alikuwa amezungukwa sana kwa vile majeshi yake mazito yalikuwa ndiyo yameshathibitiwa, Amini akaitangazia dunia kuwa amevamiwa na majeshi ya Tanzania (na kweli safari hii alikuwa amevamiwa kikwelikweli). Hata hivyo Nyerere naye akajibu kuwa jamaa huyu alituvamia akachukua sehemu ya Kagera, na kuitangazaia dunia. Ili kuionyesha dunia kuwa anasema kweli, Nyerere na Sokoine walikaribisha ujumbe wa OAU pale Kagera na kuwaomnyesha kuwa lie eneo la Mutukula bado lilikuwa linakaliwa na majeshi ya Amin na bendera yake bado inapepea. Kufanya hivyo kulifanya jumuia ya kimataifa isimwamini Amin katika kipindi ambacho alikuwa akipewa kipigo safi sana.

HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA

Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka wiliwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.

KIPIGO CHA LUKAYA

Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindii ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mshiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani

Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zatu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.

Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.

BRIG GEN MOSES NNAUYE

huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana..akiwa ni vikosi vya bendi na burudani...[ie mwenge jazz,na kwaya ya luteni komba...]hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...

Ma-CDF wetu kwa kadri niwezavyo.

WAKUU WA MAJESHI CDF

1.1964-1974: Sarakikya
2.1974-1980: Twalipo
3.1980-1988: Musuguri
4.1988-1994: Kiaro
5.1994-2001: Mboma
6.2001-2007: Waitara
7.2007-2016 Mwamunyange
8.2016-Venance Mabeyo-

CHANGAMOTO ZA VITANI

Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mble wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya KarumaKwa maajabu, Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe

2. Gen Msuguri alikuwa siyo msomi sana lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha. Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.

3. Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

..kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.

Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.

..Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

..Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.

..baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

..Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

..Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.

Every nation and every country has been blessed by great individuals. They have left footprints. Their lives and actions tells us the purpose of life and living. Maj. Gen Mwita Chacha Marwa a.k.a Kambale was never a scholar neither a good politicians but he is worth a role model to many of us. we can learn from him and make our lives beuatiful and worth living. God has decided to call him at the time when Tanzania may have wanted him more, we are in a critical time of struggle, struggle that can not be compared to theirs at that time. But it a struggle that pose danger to survival of this nation

Ndugu zangu, vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake..., vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha..., "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga........." Think about it..

Mimi Binafsi siwezi kumsahau Baba Nape kweli alikuwa Mwanasiasa safi aliweza kuwahamasisha watu mpaka wengine tulisahau kama kuna kufa vitani alikuwa na uwezo mzuri sana wa kujieleza na kumwelezea Adui alivyo dhaifu mpaka ninyi askari mnamkubali na mnaamini kuwa kweli Adui huyu si chochote tutamfumua tu, vilevile John komba alikuwa ana uwezo wa kutuburudisha kiasi cha kujisikia kuwa tuko nyumbani na aliyekuwa tunamzimia sana ni wale vijana wa Johns corner ile Bendi ya JKT na tuliporudi kweli walituimbia wimbo ambao wengi uliwatoa machozi ambao unasema hivi-MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.Mwenge Jazz nao hawakuwa nyuma kutumbuiza wapiganaji tunawashukuru sana.

Nitaendelea...
Simulizi yako imekosa uhalisia kwa kukosekana mchango wa MTU muhimu sana katka vita vya Kagera ambae hakutajwa na si mwingine ni Brig Kitete ambae alikuwa mkuu wa mbinu za kivita (War Planner) alifariki muda mfupi baada ya vita kwa ajali ya gari jijini dar.
 
Simulizi yako imekosa uhalisia kwa kukosekana mchango wa MTU muhimu sana katka vita vya Kagera ambae hakutajwa na si mwingine ni Brig Kitete ambae alikuwa mkuu wa mbinu za kivita (War Planner) alifariki muda mfupi baada ya vita kwa ajali ya gari jijini dar.
Soma vizuri hiyo ipo na nimeelezea vizuri sana pitia sehemu ya Pili na ya Tatu!!
 
Soma vizuri hiyo ipo na nimeelezea vizuri sana pitia sehemu ya Pili na ya Tatu!!
Nimeona mkuu, hongera sana.
Ni masahibu gani yalimkuta kamanda Dominic Nshimani mpaka kupelekea kunyongwa? A decorated hero, so sad.
 

VITA VYA KAGERA: Nyerere, Samora wakubaliana kumpiga Idi Amin-5​


Muda mfupi baada ya Rais Julius Nyerere kulitangazia Taifa jijini Dar es Salaam kuhusu uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania kumpiga, Alhamisi ya Novemba 2, 1978, alipanda ndege kwenda Beira, Msumbiji kwenye mkutano na mwenyeji wake, Rais Samora Machel.

Ilikuwa aahirishe safari hiyo lakini alilazimika kwenda kwa sababu alikuwa mwenyekiti wa Nchi za Mstari wa Mbele (FLS) katika ukombozi. Nchi nyingine ni Angola, Botswana, Msumbiji, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

Wakati huo pia kulikuwa na mgogoro wa mpaka kati ya Zambia na Zimbabwe (zamani Rhodesia) uliosababishwa na Rais Kenneth Kaunda wa Zambia. Nyerere ndiye aliyekuwa ameitisha mkutano wa kushughulikia mgogoro huo.

Kaunda alikuwa amefungua mpaka wake na Zimbabwe, jambo lililomkera sana Nyerere na Samora.

Nchini Rhodesia, mwanasiasa aliyeitwa Ndabaningi Sithole, ambaye ni mwanzilishi wa chama cha Zimbabwe African National Union (Zanu) kabla ya kuangushwa na Robert Mugabe, alikuwa mshirika wa karibu sana wa Idi Amin.

Kwa hiyo kufunguliwa kwa mpaka huo kulimfadhaisha Mwalimu Nyerere, hasa wakati huo ambao tayari alikuwa na mgogoro na Uganda. Kwa namna fulani Rhodesia ilikuwa na uhusiano wa kijeshi na utawala wa Idi Amin wa Uganda.

Katika ukurasa wa 114 wa kitabu chake cha For the Sake of Argument: Essays and Minority Reports, mwandishi Christopher Hitchens anasema wakati fulani “akiwa ofisini, (Sithole) aliomba msaada wa Idi Amin wa kuunda jeshi lake binafsi”.

Jumatatu ya Julai 17, 1978, ikiwa ni miezi minne kabla ya kuzuka kwa Vita vya Uganda, jarida la Facts and Reports (volume 8), katika habari iliyoandikwa na David Martin iliyokuwa na kichwa kilichosomeka “Sithole Guerrillas Fly to Amin for Training”, kulikuwa na tuhuma za uhusiano huo wa kijeshi.

“Dikteta Idi Amin ameshutumiwa vikali kwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa maelfu ya vijana wa washirika wa Ian Smith (wa Rhodesia) kwa madhumuni ya kuwatumia kuvuruga harakati za ukombozi nchini Zimbabwe,” aliandika mwandishi huyo.

Jarida jingine la International Bulletin (volume 4) la Julai 1978, lilizungumzia suala hilo.

“Mshirika mweusi wa Ian Smith, Mchungaji Ndabaningi Sithole anafundisha jeshi lake binafsi nchini Uganda,” liliandika jarida hilo. Pia, jarida la Africa Research Bulletin’ likaripoti kuwa “Mchungaji Ndabaningi Sithole amepokea idadi kubwa ya wapiganaji kutoka Uganda kwa Idi Amin pamoja na vifaa vya mafunzo”.

Zilikuwapo pia habari kwamba ndege za Rhodesia zilikuwa zikitua katika viwanja vya ndege vya Uganda—Entebbe na Nakosongola.

Habari hizo na nyinginezo za ushirika wa Idi Amin na Sithole, zikijumlishwa na ile ya Zambia kufungua mpaka wake na Rhodesia, zilimfanya Mwalimu Nyerere kwenda Beira, Msumbiji, kujadili jambo hilo haraka kadri ilivyowezekana.

Nyerere na Samora walikutana jioni ya Novemba 2, 1978 kujadili jambo hilo na kuridhika kuwa Idi Amin alitumiwa na mataifa mengine kuivamia Tanzania kwa lengo la kumuondoa Nyerere katika harakati zake za ukombozi wa Zimbabwe dhidi ya akina Ian Smith na mshirika wake, Mchungaji Ndabaningi Sithole, na kwamba huenda Uingereza ilikuwa nyuma ya mpango huo.

Baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa halikuwa jambo la bahati mbaya kwamba vita vya Kagera kuzuka wakati huo muhimu wa mazungumzo kati ya vikosi vya ukombozi na serikali ya wachache ya Ian Smith nchini Zimbabwe.

Walisema wapinzani wa ukombozi walitaka kudhoofisha jitihada za Mwalimu Nyerere “kwa gharama zozote”.

Baada ya kutafakari yote hayo, Nyerere alimhakikishia Samora kwamba Tanzania ingeweza kupambana na Idi Amin bila kupoteza lengo lake la harakati za ukombozi wa Zimbabwe.

Walikubaliana kuwa kikosi cha jeshi la Tanzania kilichokuwa katika mpaka wa Msumbiji na Rhodesia kirejee Tanzania na, zaidi ya hilo, Samora naye akaahidi kutoa kikosi chake kuja kusaidiana na Tanzania.

Ndani ya siku chache, wanajeshi wa Msumbiji wakawa wamewasili Kagera tayari kwa mapigano. Hakuna chombo chochote cha habari cha Tanzania kilichoandika taarifa zozote za wapiganaji wa Msumbiji kuwasili Kagera.

Hata hivyo, kitabu cha War in Uganda cha Tony Avirgan na ?Martha Honey kinasema “ushahidi mdogo sana kwamba wapiganaji wa Msumbiji walikuwa Tanzania ni nakala ya gazeti Noticias iliyoachwa kwenye ukumbi wa mapumziko wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza.”

Waandishi wa kitabu hicho, ambao walikuwa uwanja wa vita, wamesema mbali na wapiganaji hao 800 kutoka Msumbiji, hakukuwa na wapiganaji wengine kutoka taifa jingine lolote duniani waliokuwa wakipigana bega kwa bega na wapiganaji wa Tanzania dhidi ya majeshi ya Idi Amin.

Katika lile juma la pili la Novemba 1978, pamoja na magumu yote waliyokumbana nayo kama mvua, Tanzania iliweza kuwaandaa vyema wapiganaji wake.

Soma Zaidi: Idi Amin avunja daraja la Mto Kagera - 4

Juma hilo ndipo alipowasili Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu kuongoza mapambano. Pamoja na kwamba Tanzania ilisikitishwa sana na kuvunjwa kwa daraja la Mto Kagera, ilipata nafasi ya kufanya maandalizi ya kutosha bila hofu ya kuvamiwa na majeshi ya Idi Amin ambayo yangeweza kulitumia daraja hilo kushambulia upande wa pili.

Cc Nguruvi3 , Kichuguu, Pascal Mayalla , Shwari
 
@Elichoma ulituahidi kitabu mrejesho ukoje kuhusu kitabu mzee wangu.
 
Back
Top Bottom