Vita vya majimaji mpaka jina la Songea

Mack...
Ninao wazee wangu Wangoni.
Hapo Songea uliza habari za marehemu Abdallah Simba.

Huyo ni babu yangu.

Uliza utaelezwa historia yake kwani alikuwa ndiye Liwali wa maeneo hayo.
ielezee hiyo historia ya huyo mtu
 
Mack...
Ninao wazee wangu Wangoni.
Hapo Songea uliza habari za marehemu Abdallah Simba.

Huyo ni babu yangu.

Uliza utaelezwa historia yake kwani alikuwa ndiye Liwali wa maeneo hayo.
Babu yetu umeharibu mada ya watu

Mwenzako kaanzisha mada vizur kabisa wewe umeingiza udini kwenye mada yake

Kama ulikuwa unayajua yote haya kwanini usingefungua topic yako? Dah!

Yaan sisi tunajivunia majina ya kibantu wewe unajivunia majina ya kitumwa
 
Beira...
Huwa nashindwa kufanya mjadala na mtu anaeingia katika mjadala na kejeli na kurusha majina wewe fulani wewe hivi, wewe babu.

Mwisho inaishia matusi nk.

Una hoja unaweza ukasema, ''Mzee Mohamed...'' hapa najua nazungumza na mtu mwenye adabu zake kamili vinginevyo ni kinyume cha hivyo.
 
Kwahiyo unakataa kwamba wewe siyo babu?
 
Kwahiyo unakataa kwamba wewe siyo babu?
Beira...
Hapana mimi ni mtu mzima sana nina wajukuu Alhamdulillah ninachokueleza ni staha.

Umri wangu ni miaka 67 hivyo nikiamini wewe ni kijana mimi ni sawa na baba yako naweza kukuzaa kwa hiyo nastahili heshima ya huu uzee wangu.

Ikiwa nitahisi dalili za utovu wa adabu kutoka kwako kwa jinsi unavyoandika naingiwa na hofu ya kuvunjiwa heshima.

Ndipo nikakuelekeza hata namna ya kuandika ikiwa kumtaja mtu kwa umri wake ni muhimu kwako.

Unaweza kuandika hivi: "Mzee Mohamed..."

Yaweza labda kwenu umefunzwa adabu vingine lakini kwa kawaida ya mtoto aliyelelewa hatafanya hivyo kwani ukimtaja mtu kwa hiyo namna yako ni umemtukana.

Ningeweza kukaa kimya na ukawa mwisho wetu lakini nimekuchukulia kama kijana unaehitaji kuelekezwa na ukajua.
 
Mack...
Ninao wazee wangu Wangoni.
Hapo Songea uliza habari za marehemu Abdallah Simba.

Huyo ni babu yangu.

Uliza utaelezwa historia yake kwani alikuwa ndiye Liwali wa maeneo hayo.
Shikamoo Mzee wangu

Kwanza pole na msiba wa kijana wetu Sheikh Zingizi nasikia Jana ijumaa alilala mauti na kuzikwa Msasani

Pili ahsante kwa historia ,wangoni wakwe zangu ,Mungu akuzidishie
 
Hahahaha, Mzee wangu Mohamed Said wala usitumie nguvu ,hii kitu ungewapa reference wakasome wenyewe
 
Hahahaha, Mzee wangu Mohamed Said wala usitumie nguvu ,hii kitu ungewapa reference wakasome wenyewe
Mtu Chake,
Nimegundua kuwa hii ndiyo njia nyepesi sana ya kuelewana.

Kuna mtu tunafanya mjadala lakini mwenzangu kaghadhibika na lugha ya kejeli imetamalaki sana dhidi yangu anashikilia kuniita ''sheikh,'' kwa kejeli.

Kila ninavyomfahamisha hasikii.
Namwambia kuwa mimi si sheikh unaiweka sifa hiyo sipo.

Nikamwekea hivyo vitu ili turejee nyuma tuelewane.

Hakika alinielewa na lugha ikabadilika akarejea na adabu kamili.
Mimi hainifurahishi sana.
 
Hahahaha, hua natulia sana pindi uwekapo mabandiko yako

Natumai wanaelewa ila kdg kdg
 
Hahahaha, hua natulia sana pindi uwekapo mabandiko yako

Natumai wanaelewa ila kdg kdg
Mtu...
Historia hii huwezi kuisikia ukaipuuza na laiti kama si kuwa nilizaliwa na wazee hawa na katika kipindi kile nisingeyajua haya yote.
 
Huyo mzee ni laghai, muongo na aliejaa hila! Anataka watanzania kila wanachowaza wawaze udini tu!

Binafsi namwona mhalifu tu, anapenda sana watu wabaguane ki dini! Mwl aliwaita watu kama hao wajinga na wapumbavu!
 
Huyo mzee ni laghai, muongo na aliejaa hila! Anataka watanzania kila wanachowaza wawaze udini tu!

Binafsi namwona mhalifu tu, anapenda sana watu wabaguane ki dini! Mwl aliwaita watu kama hao wajinga na wapumbavu!
Mzizi...
Umeghadhibika na ukighadhibika unapoteza umakini na staha inakutoka.

Hapana udini katika kusahihisha historia iliyoandikwa kwa makosa.

Mimi singependa umwingize Mwalimu Nyerere katika mjadala huu ila uwe umeisoma vyema kwanza historia ya Tanganyika na changamoto zilizokuja na uhuru.

Historia hii naamini mimi naijua vyema na nimeandika sana na moja katika tatizo kubwa baada ya uhuru kupatikana ilikuwa nafasi ya Uislam katika Tanganyika huru.

Hili lilizungumzwa katika Muslim Congress mwaka wa 1962.

Hii ni historia labda wewe huijui na inakughadhibisha kusikia kuwa hili ni tatizo tulilonalo katika jamii.

Hapana haja ya kuhamaki isome historia na haya yote yatakuwa wazi kwako.

Unàweza kuanza kwa kumsoma P. Van Bergen (1981), John Sivalon (1992) na Hamza Njozi (2002).

Kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku.
 
Kama una miaka 67 wewe siyo sawa na baba yangu

Wewe ni sawa na babu yangu
 
Kama una miaka 67 wewe siyo sawa na baba yangu

Wewe ni sawa na babu yangu
Beira...
Mjukuu wangu wa kwanza ana miaka minne.

Mwanangu wa kwanza nimempata 1984.
Fanya "interpolation," utapata jibu.

Uandishi unataka sana kufikiri.

Sababu kubwa ni kuwa kuweka kitu katika maandiko ni kuweka "record."

Hiki ndicho kinakuwa kipimo cha uwezo wako.

Anaekusoma atajua kama una kitu au mtupu.

Ikiwa umeonyesha uwezo wa akili nzuri utaheshimika.

La akikuona hamna kitu ikiwa ni muungwana ndiyo mwisho hatokujibu.

Utaona kapotea.
 
Wewe sema ujuavyo lakin lakin wewe ni babu tu
 
Nimejifunza na nimeelewa historia, lakini hao wanaotuletea udini sijaelewa na sidhani kama ina tija sana, zaidi utaanza ugomvi dhidi ya waislamu na wakristo, kwa hali kama hii utagundua kwamba Nyerere angekuwa muislamu basi nchi hii ingekuwa inafuata misingi ya kiislamu lakini Mungu ana makusudi sana.
muanzisha uzi hajataja dini ila kuna watu bado wanavinyongo na nguvu ya dini zao (acheni hizo)
Nyerere alikuwa na akili sana kuweka uhuru wa kidini, japo yeye ni mkristo lakini hakuwahi kujisifia eti ni Nguvu ya ukristo au laah,.....
Mungu wetu ni mmoja sasa hayo matabaka ya kidini yatatuletea faida gani,

Kama hao akina Abdul Sykes walikuwa wanashawisiana kuunda TANU tangu 1950 sasa walikuwa wapi mpaka Nyerere aje aanzishe 1954 na atupe uhuru 1961?
mimi sijui Historia japo inaniuma navyoona kitu cha kawaida mtu anakuja kuingizia mambo ya kidini wakati mada haihusiani na hivyo
Wakristo tumshukuru sana Mungu kwa kutupatia mtu mwenye busara sana aliyetusaidia kuikomboa nchi kutoka kwa wakoloni maana bila hivyo ingekuwa shida sana kutokana na haya yanayoonekana sasa.
 
Windson,
Kila jamii na kila watu wana historia.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imeandikwa lakini cha kustaajabisha historia hii imewafuta wazalendo wengi sana.

Imesadifu kuwa historia hii ni historia ya wazee wangu na ninaijua vyema kwa kuwa achilia mbali kuwa waasisi wa harakati za kudai uhuru ni wazee wangu, mimi nimezaliwa katika kipindi hicho.

Baadhi ya wazalendo hawa nimewajua toka udogoni.

Kwa kuona upungufu huu ndipo niliponyanyua kalamu nikaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU nikitumia Nyaraka za Sykes.

Kitabu kikachapwa London 1998 kwa Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili ikachapwa Nairobi mwaka wa 2002.

Kitabu hiki kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika na nimeeleza mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni.

Wako ambao hawakupendezewa na kitabu hiki lakini pia kuna wengi sana wamekipenda kitabu kiasi sasa tunakwenda toleo la nne.

Hakuna suala la udini labda kama waliowafuta wazee wangu kwenye historia ya chama walichokiasisi walifanya hivyo kwa udini kwa kuhofu kuonyesha mchango wa Waislam katika kudai uhuru wa Tanganyika.

 

Tukiachana na kasumba na ushabiki wa dini, Ki-uhalisia hakuna mtume yeyote aliyekuja na majina kwa ajili ya kuwaita wafuasi wake. Tulio wengi tumeathirika na kasumba kutokana na kutopenda kufanya utafiti hata ule mdogo kuhusu baadhi ya mambo tunayoyaamini.

Ndiyo maana leo hii Waafrika walioupukea uislamu hudhani kuwa yale majina ya kiarabu ndiyo ya KIISLAMU kitu ambacho siyo kweli maana hata Mtume Muhamad (SAW ) aliyakuta. Waafrika waliyopokea UKRISTO nao hudhani ya kuwa yale majina ya kizungu ndiyo ya KIKRISTO kitu ambacho pia si kweli maana majina yalikuwepo kabla mitume hawajafika.

Ki uhalisia majina yametokana na mila za watu mbalimbali ndiyo maana hata watu weupe (Waarabu, Wazungu, waajemi, wachina, wajapani na wakorea) wanatofautiana majina kulingana na lugha na tamaduni zao. huwezi kukuta mchina anaitwa jina la kijapani au ukute muhajemi anaitwa jina la kiarabau. Hata wazungu ni mara chache kukuta Muitaliano anaitwa jina la kirusi.

Sisi wazee wetu hawakuwa wakihoji au kudadisi, wao waliopokea tu mradi wamepewa na weupe (Umasikini mbaya ) ndiyo maana leo hii baadhi yetu tumefikia kuhoji kwa nini fulani ana jina la kiislamu halafu anaenda kanisani (& vice versa). Tujitambue tuanze kutukuza vyetu (japo tumechelewa)
 
Mie siwezi kugadhabiika kwa ajili yako Babu MS...japo hupendi kuitwa babu sijui kwanini!

Nawapa tahadhari tu watu wasioweza kubaini nia yako ovu uliyoificha chini ya kivuli cha "kuijua sana historia"!
Bahati nzuri watu wengi wanaanza kukustukia kuwa unachanganya mambo makusudi kitapeli kulaghai watu!

Mwl ntamtumia tu, hakuna mtu mwenye haki zaidi ya kutumia misemo ya Baba wa taifa! Ni kweli wadini aliwaita wajinga wakati akawaita wapumbavu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…