hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Vita vya muda mfupi baina ya ndugu wawili India na Pakistan
Vilivyomalizwa na Dogfight (vita vya ndege kwa ndege)
Niliandika post hii muda ila sikuwa nimeipost kwasababu kadha wa kadha). Fuatana nami upate maarifa kwa kifupi.
Pakistan na India wote ni Wahindi kwa asili. Waligawanyika kwa mtazamo wa kiimani. Pakistan ni waislamu na India ni Wahindu. Wakati ule wote wakiwa ni nchi moja, walikuwa chini ya ukoloni wa Muingereza toka 1857 hadi 1947. Wakati wa harakati za uhuru waislamu wa kihindi waligoma mbele ya Waingereza walipotaka kutoa uhuru kwa India moja, wakataka mgawanyo. Walidai haiwezekani muislamu na muhindu wakakaa pamoja. Hivyo mnamo 1947 chini ya Muingereza zikazaliwa nchi mbili mahasimu hadi leo hivi. Sina nafasi kwa sasa kuelezea historia yote ilivyokuwa, nataka tu upate kilichojiri katika vita vya muda mfupi vilivyotokea hivi karibuni.
Vita vya muda mfupi (tar 7 hadi 10/ may 2025)
Baada ya tukio la kigaidi lililoua raia 40 wa India katika jimbo lenye mzozo la Kashmir kwa upande wa India. Mnamo tar 7 may India iliishambulia Pakistan kwa ndege vita na kuharibu baadhi ya miundo mbinu kadha kwa kadha. Kesho yake Pakistan nayo ikajibu kwa Drones za kutosha ambazo zililenga shabaha katika sehemu kadha wa kadha ikiwemo bezi ya kijeshi ya India. Katika vita hivi, India ilionesha ufanisi katika drones na air defense system huku Pakistan ikionesha ufanisi katika dogfight na mashambulizi ya ndege kwa ujumla.
Dogfigt mnamo may 7 na kuamkia may 8
Ndege za Pakistan za J10 ambazo ni zao la China zilifanikiwa kuangusha ndege 3 za India aina ya Rafael kutoka Ufaransa na Su 30 kutoka Urusi. Ingawa Pakistan inadai ni zaidi ya hizo. India nayo ilidai kuwa imetungua ndege kadhaa za hasimu wake huyo kwa makombora ya ulinzi. Yalikuwa ni mapigano makubwa ambayo yameshuhudiwa na ulimwengu wa vita. Mapigano haya sio mageni kwa Pakistan na India na duniani kwa ujumla. Ni marudio tu. Pambano la mwisho la dog fight duniani lilifanyika mnamo 2019 kati ya India na Pakistan. Pakistan kupitia F16 ambazo ni zao la US ilizitungua ndege za India za MiG-21 Bison and an Su-30MKI ambazo ni zao la Urusi katika mapigano ya angani. Lilikuwa ni pambano la tatu la dogfight kati ya India na Pakistan. Pambano hili lilizipa soko ndege za F16 duniani. Haya yalikuwa ni mafanikio ya pili kwa ya ndege za F16. Mara ya kwanza ndege hizi zilijibebea ujiko katika vita vya Balkan (kosovo war) mnamo 1999. Pale F15 na F16 Falcon zilipotungua ndege nne za Urusi aina ya Mig29s. F16 ilitengenezwa kuchukua nafasi ya F15 iliyotengenezwa mnamo 1969 ambayo daima imeonesha ubabe wa anga kwa ndege pinzani. Ilipata sana utukufu mkubwa katika vita vya ghuba (1990-1991) baada ya kuzigaragaza ndege za Soviet katika dogfight. Ndege hii imeuzika sana nadhani ndio ndege yenye mauzo mengi kuliko ndege zingine za Marekani. Wakati Trump amefanya ziara hivi majuzi katika nchi za ghuba amepokelewa na ndege F15 angani kwa nchi zote za kiarabu alizoenda. Ifuatayo ni aina za ndege ambazo Pakistan na India wanamiliki.
Ndege vita za Pakistan
Zinatoka China, Marekani, na Ufaransa.
1. J10: ni ndege kutoka China ambayo muundo wake based yake ni F16 ya Marekani. Deng Xioping rais wa China mnamo 1981 alianzisha project ya ndege vita kwa kukusanya wataalamu mbalimbali wa ndani na wa nje wa nchi. 1988 taarifa za kijasusi zilivuja kwamba Israeli imehusika kutoa wataalamu wake ambao walihusika kutoa tekinolojia ya f16. Israeli ilikanusha ila majasusi wa Urusi wakathibitisha. Israeli inakashfa nyingi ya kuuza tekinolojia ya Marekani kwa China ikiwemo mtambo wa kudhibiti mitandao ya kijamii. Mnamo 1994, J10 zikakamilika na kuingia kwenye operation mnamo 2006. Ni ndege za kizazi cha tatu. Hivyo mnamo tarehe 8 may kazi yake imeonekana na kuipa China utukufu.
2. JF-17 Thunder. Ni ndege iliyotengenezwa na Pakistan kwa ushirikiano na China.
3. F-16 Fighting Falcon: Ndege za Marekani ambazo zilianza kutengenezwa toka 1973 hadi 2019, ndio ndege zenye soko kubwa duniani na zipo katika nchi nyingi.
4. Mirage III Dassault na Mirage 5 Dassault. Ndege za Ufaransa.
5. F-7. Ndege za China.
Pakistan hana ndege vita za Urusi zaidi ya ndege kubwa ya mafuta tu.
Ndege vita za India
Zinatokana na mataifa matatu, Ufaransa, Uingereza, na Urusi.
1. SEPECAT Jaguar: ni Ndege vita iliyoundwa kwa ushirikiano wa Uingereza na Ufaransa mnamo 1968-1981
2. Mikoyan MiG-29. Ni Ndege vita iliyoundwa zama za Soviet, iliundwa mnamo 1970 dhidi ya F15 na F16 za Marekani.
3. Dassault Mirage 2000: Ndege ya Mfaransa iliyoundwa mnamo 1970
4. Rafael: Ndege vita za Ufaransa za mwaka 1986 zilizoangushwa na J10 za China.
5. Sukhoi Su-30MKI. Ndege za Urusi
India hana ndege za mapigano za Marekani bali ana Sea Hawk helkopta ya mashambulizi pamoja na C-130J Super Hercules ndege ya usafirishaji wanajeshi na Boing tank kwajili ya mafuta.
Hivyo katika kuvutana kijeshi kati ya India na Pakistan ilibidi Trump aingilie kati na kuwapatanisha maana wote walikuwa wamesogeza majeshi yao mipakani tayari kwa vita. Mnamo jumamosi tar 10 may, wakafikia makubaliano ya kusimamisha vita kwa upatanisho wa Marekani. Nchi hizi mbili wote ni washirika wa Marekani. Zama za kati Pakistan alikuwa ndio mshirika mkubwa wa Marekani na NATO kijeshi ili kuzuia utanukaji wa ushawishi wa USSR kwa Asia kusini pamoja na dhidi ya China. Na India alikuwa upande wa Soviet Union lakini katika mianzo ya India walikuwa na urafiki wa jadi na Marekani toka 1893 kabla ya India haijapata Uhuru. Na US ilichangia msukumo wa uhuru wa India maana wote walikuwa na mkoloni mmoja. Urafiki wao ulikuwa ni wa pekee hata kuisaidia India dhidi ya China wakati wa vita vya mipaka 1962, China ilishinda ingawa pia ilipoteza wanajeshi wengi. Uhusiano wa US na India ulianza kuingia doa baaada ya Kennedy kuuawa mnamo 1963, Marekani wakati wa rais Lyndon Jongnson ikaanza kuwekeza kijeshi kwa Pakistan dhidi ya Sovieti na China. Iliona kuwa Pakistan ina mpaka mkubwa na China ambao unatoa nafasi kuidhibiti China, India haikutaka uhusiano huo. Ingawa Marekani haikuachana na India moja kwa moja. Mnamo 1965 India na Pakistan wakaingia vitani tena juu ya mipaka, wote walidai ushindi ila kwa uhalisi Pakistan ilishinda maana muathiriwa mkubwa alikuwa ni India. Katika vita vya anga, Pakistan ilidai ilitungua ndege 104 za India na kupoteza ndege 19 huku India ikidai kutungua ndege 73 na kupoteza 35. Mnamo 1967 India ikaingia vitani tena na China, India ikafanikiwa kurejesha utukufu wake baada ya kuishinda China na kuifanya ijisalimishe.
Mnamo 1969 kutokana na pressure kubwa kutoka China na Pakistan, India ilipiga magoti kwa Marekani ili ipate msaada ila Richard Nixon rais wa Marekani hakuonesha kujali. Hivyo India chini ya waziri mkuu Indira Gandi kishingo upande hakuwa na jinsi zaidi ya kugeukia upande wa Soviet (USSR) na wakasaini mahusino ya kijeshi mnamo 1971. Marekani ikakasirishwa. Mwaka huo huo 1971 Pakistan na India ziliingia vitani, vita vilikuwa vikali sana. Na mwisho Pakistan ilishindwa na kujisalimisha.
China na US zilikaa upande wa Pakistan, na ulimwengu wote wa Kiarabu ukakaa upande wa Marekani na Pakistan. (Wakati huo China na USSR walikuwa na uhusiano mbaya). Huku Israeli na USSR zikakaa upande wa India. Israeli ikaipa India silaha za kutosha. Soviet nayo ikaipa India zana za kutosha ikiwemo nyambizi na carrier za ndege. Hadi leo hivi India ni marafiki wakubwa na Israeli na Urusi, India haina uhusiano na ulimwengu wa kiarabu. Na tangia hapo India ikawa mnunuzi wa zana za kijeshi kutoka USSR na kwa leo kwa Urusi ingawa sasa imepunguza kwa 61$ na kuanza kuwekeza binafsi zana binafsi.
Baada ya anguko la Soviet (1991) India ilifanya muhafaka na Marekani na nchi za NATO na kuondolewa vikwazo. Ingawa India na Urusi ni marafiki wa zama lakini sasa urafiki wa India na Marekani unazidi kuongezeka hasa sababu ya mgogoro wa mipaka kati ya China na India. Hivyo kando ya uhusiano wa kibiashara kati ya US na India, wanao pia uhusiano wa kijeshi (defence partner) na wana aina ya NATO yao inayoitwa Quad ambao wapo US, Japan na India dhidi ya China. Kwahiyo basi India ni kama kirusi cha mkakati, hata Brics India haoneshi mshikamano wa kweli. Zingatia Marekani hana urafiki ama uadui wa kudumu bali maslahi ya kudumu.
Kwa hivyo India na Pakistan ni washirika wa Marekani wa kihistoria na wote wanamiliki mabomu ya nyuklia na wote Marekani aliwaondoa kwenye lists ya maadui waovu. Hivyo baba yao alipoona wanawe wanataka vagi kwa haraka alijitokeza kuwapatanisha, maana bado wanafaa kwa matumizi.
Waislamu wasiojielewa katika mzozo huu walikaa upande wa Pakistan, nafikiri hawakutambua haya, kwamba Pakistan ni mtoto wa Marekani pia.
Mchambuzi wa dini, mambo ya jamii, siasa na historia,mwanazuoni wakujitegemea