Vita ya Al Shabaab na Ahlul Sunna Wal Jamaa, dhana ya Ugaidi na ulafi wa Madaraka uliojificha chini ya kivuli cha Uislam

Mtapambana sana kwa kuwa kuna uhaba vichwani
 
Usiende mbali sana!
Alshabaab hawatetei Uislam
Al Qaeda hawatetei Uislam
Isis hawatetei Uislam
Boko haram hawatetei Uislam.

Mwanzo wa wino wako unaonyesha dhahiri ya kuutetea upande wa Al Shabaab. Usitekwe na hizo mambo. Soma dini utayajua haya. Ila ukiendekeza mapenzi ya kiitakidi ya upande unaoupenda utapata hasara.
 
Acha ubwege anachonganisha nini wakati anaandika kitu kilichotokea? Wewe wasiwasi wako ni kuwa anazigusa dini zenu za wazungu na waarabu? Ndo unachotetea.... 😂😂😂😂
Oooh! Kumbe unawajuwa na kufahamu wazungu na waarabu??
Aidha umeziekewa dini zao pia??
Kwa hiyo umebaki na jina lako (id) hiyohiyo.. Chizi endelea kw chizi
 
Thank you. Endelea kutupa historia mbalimbali nadhani upo vizuri sana katika uchambuzi na uandishi kuhusiana na ugaidi

AHLUL SUNNA WAL JAMAA Vs AL SHABAAB

Mapambano kati ya Ahlul Sunna Wal Jamaa yalipata moto kuanzia Novemba 1 mpaka Disemba 16 mwaka 2008 katika mji wa Galgaduud uliopo katikati ya nchi ya Somalia na uliopo maili 230 kutoka mji mkuu Mogadishu. Katika mapigano hayo kila kundi lilikua linatumia silaha za kisasa mfano SMG, AK47 pamoja na RPG. Kila kikundi kilipigana kwa hali na mali huku wanamgambo wa Al Shabaab kuonekana kua wenye uhodari na uzoefu mkubwa wa kivita. Kwa upande mwengine Ahlul Sunna Wal Jamaa walikua hawana mafunzo yeyote katika kuiendea vita ile lakini walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ambao wengine walijitolea magari yao yawe yanatumika katika hio vita hapo ndipo kundi hilo likaamua kupambana kufa na kupona na kufanikiwa kuukomboa mji wa Galgaduud ambao ulikua himaya ya Al Shabaab. Hili lilikua pigo kubwa kwa wapiganaji wa Al Shabaab kundi ambalo lilikua likiogopewa na kuheshimika kuambulia kipigo kutoka kwa Ahlul Sunna Wal Jamaa. Lakini anguko la Al Shabaab halikuishia hapo…..

MAPAMBANO YA DUSA MAREB

Ikiwa bado Al Shabaab wanaugulia maumivu ya kuupoteza mji wa Galgaduud wakapata tena pigo lengine la kushtukiza, hili lilikua ni baada ya vijana wa Ahlul Sunna Wal Jamaa kufanya mashambulizi ya kushtukiza (ambush) kwa wanamgambo wa Al Shabaab kwenye mji mdogo wa Dusa Mareb.

Kutokana na Al Shabaab kutojiandaa la shambulizi hilo ikapelekea kupoteza mji huo na hili lilikua pigo jengine kubwa kwa Al Shabaab. Baadhi ya wakazi wa mji wa Dusa Mareb walikua wakisheherekea ushindi huo hadharani kwa kudai kua Al Shabaab waliingilia uhuru wao na maamuzi kuhusu Maisha yao. Haikuishia hapo tuu Al Shabaab wakapoteza sehem nyengine muhimu ya Garaceel. Waislamu kwa Waislamu wanapigana, je hio ni JIHAD?

Hilo ndilo katazo ambalo alielezea Al marhum Shahid Aboud Roggo…….ITAENDELEA
 
KARIBU TUPATE MADINI😂😂😂😂😂

Back
Top Bottom