Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
VITA YA AZANIA NA TAMBAZA (1993 - 1994)
Mwaka 1993 Jeshi la Sekondari ya Tambaza liliivamia Sekondari ya Azania kutokea Bonde la Jangwani nyuma ya Hospitali ya Muhimbili baada ya juhudi za kutama kusitisha mapigano kushindikana! Kufumba na kufumbua, askari wa Tambaza walirusha makombora na kuanza kulipua jengo la Maabara ya Kemia wakitumia Mabomu ya Petroli.
Wakati huo mimi nilikuwa Kidato cha Sita na mmoja wa viongozi katika Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) katika Tawi la Azania na Jangwani (Azajangwa). Nilikuwa pia kiongozi katika Serikali ya Wanafunzi ya Azania ambapo nilikuwa General Prefect!
Mimi na Kiongozi mwenzangu wa UKWATA aliyeitwa Enock Mayage, tuliitisha kikao cha viongozi wa vikundi vya dini kilichofanyika katika Ofisi ya UKWATA maarufu kama Chemba ya UKWATA. Viongozi waliohudhiria kikao kile walitoka ASA, UKWATA, TYCS, JUWAKWATA na DAMUSA. Pamoja na kutaka kuweka mikakati ya kuzuia vita, endapo tutavamiwa niliazimia kutumia kikao kile kuwashawishi wenzangu ili waumini wetu wasipigane.
Tukafikia muafaka wa kupeleka mapendekezo yetu kwa Mkuu wa Shule. Tulimshauri yeye aongee na Mkuu wa Shule ya Tambaza ili kiitishwe kikao cha viongozi wa vikundi vya dini na Serikali za Wanafunzi kutoka Shule zote mbili kwa majadiliano.
Wakati tukiwa katika Ofisi ya Shule, kijana mmoja wa Tambaza alipiga simu ya Shule akisema Jeshi lao liko njiani kuja kuivamia Azania. Kama kijana yule alitumia simu ya Shule au ya nyumbani kwao hatujui. Ingawa Kuna uwezekano alikuwa Mkazi wa Muhimbili Hivyo uwezekano mkubwa alitumia simu ya nyumbani kwao!
Baada ya taarifa ile, nilitoka nje na baada ya dakika 10 hivi, niliona utitiri wa vijana wa Tambaza wapatao 200 au hata 300 wakiibukia kutokea eneo ambalo sasa imejengwa MOI kile Muhimbili!
Safari hii, Tambaza walikuwa wanapambana bila kuwa na mmoja wa makamanda wao aliyeitwa Puza ambaye alifariki dunia miaka miaka mitatu nyuma kwa kunywa sumu. 'Jenerali Okelo' alikuwa mstaafu kwani alimaliza Shule mwaka 1989 au 1990.
Msela Shetani alikuwa amesahaulika katika Jeshi la Tambaza. Kikosi chake cha Tambaza International Smokers Association (TISA) kiliendelea kuwepo ingawa muda huo kilikuwa kimeanza kizidiwa umaarufu na Kikosi cha Nyau. Hata hivyo, kikosi cha Nyau hakikuwa na uwezo wa kupambana na Azania kwa sababu kilikuwa kimeandaliwa mahususi kwa ajili ya kupigana na makondakta wa daladala.
Mimi nilijitosa na nilikuwa mstari wa mbele katika kuongoza Jeshi la Uokozi kutoka Azania ambapo tulifanikiwa kuuzima moto ule kwa kutumia mchanga ndani ya dakika 10 tu pasipo kuleta madhara ye yote. Kutokana na ugeni wa mazingira, wapiganaji wa Tambaza walikwama katika uzio wa Jangwani walipotaka kukimbia. Majeshi ya Azania yalitumia kuni za kupikia zilizokuwa katika Bwalo la Shule kama silaha.
Mimi niliendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano yale nikifanya kazi ya kuwaokoa vijana wa Tambaza waliokuwa wamezidiwa ili wasiuliwe au wasiumizwe. Kwa kuwa nilikuwa Kiongozi wa Dini pale Azania, vijana wa Azania kila waliponiona na kusikia sauti yangu waliona aibu na hivyo waliacha kuwaumiza vijana wa Tambaza. Lile ni moja ya matukio ya kutisha ambayo kamwe sitayasahau maishani.
Vilevile, mimi naliona tukio lile kama moja ya matukio ambayo Mungu alinitia ujasiri kuwa mtetezi hata kwa adui. Ninaamini kuwa Mungu alianza kuniandaa tangu zamani kwa ajili ya wajibu huu wa utetezi ninaoufanya sasa!
Je, ni kitu gani kilchokushangazs kuhusiana na tukio lile? Je, wewe ni miongoni mwa watu walioshiriki katika mapigano yale? Je, wewe ni miongoni mwa watu walioshuhudia kwa mbali? Je, unakumbuka nini kuhusiana na vita ile?
Je, ulikuwa unajua kuwa vita ile ndio ambayo iliyosababisha Serikali kuifunga kabisa Shule ya Tambaza na Wanafunzi wake kuhamishiwa Shule nyingine za Serikali ikiwemo Kwiro? Baadaye Serikali ikaifanya Tambaza kuwa High School na kuwa mchanganyiko. Ilipofunguliwa wakaletwa wanafunzi wapya wa Kidato cha Tano na kuongezwa michepuo ambayo huko awali haikuwepo ya HGL, HGK, EGM, CBG, nk.
Wakati Tambaza inafungwa, wanafunzi wa Kidato cha Sita waliokuwepo waliruhusiwa kumalizia pale pale Tambaza. Walikuwa wakisoma michepuo ya PCM na PCB na kulikuwa na wasichana wachache. Wanafunzi wote wa O' Levels walihamishwa.
Hakika tunasafiri na tumetoka mbali sana katika maisha haya!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Soma pia Ebu tujikumbushe enzi za tambaza na azania kabla tambaza kubadilishwa kuwa high school