Vita ya biashara Del Monte Kenya na Azam Bakhresa Group of companies


Kweli kuna vikwazo sana katika soko la Kenya kwa bidhaa inayoingia;Tatizo kubwa ni gharama zao wanazotoza na unatakiwa ulipe kwa pesa yao ambayo inathamani kubwa kuliko yetu ukipiga mchanganuo unaona gharama za bidhaa yako inakuwa juu so inakuwa ngumu kushindanisha.Pia Wakenya wanajali sana Documentation hakuna mkato lazima ufate taratibu zote ukitaka kuingiza mzigo nchini kwao hakuna shortcut kama ilivyo hapa kwetu.
 
Watanzania tujiulize tuna bank,kampuni za insurance,bidhaa iliyotayari kuliwa inayouzwa kenya?jibu hakuna.jamaa wabaguzi sana hawataki chochote tufanye kwao zaidi ya kuchukua raw materials toka kwetu.wao wanauza bidhaa zote hapa tanzania
 

Mkuu,
Uko sawa nimekaa Kenya kipindi fulani najua adha yake kibiashara kama una import mzigo kwao.
 
Kwa hili sikubaliani na wanaokebehi bidhaa zetu,tuna TBS,TFDA wote hawa wanashughulika na ubora wa vyakula(vinywaji)bidhaa za Azam zina ubora unaotakiwa atujasikia malalamiko toka kwa watumiaji wa TZ.Kenya wao wanataka kuodhi soko la EA,wanazuia kuingiza bidhaa toka TZ ili viwanda vya kwao vijipanue na ajira ya watu wao iongezeke.Wakati tunasaini mkataba wa soko la pamoja sisi wa TZ tulikuwa na ofu,kenya wakatafsiri kuwa ofu yetu kuwa atuwezi kupenya kwenye masoko yao ndio maana tunasita,baadae hali imekuwa tofauti bidhaa zetu zimepenya kila mahali.Vipingamizi vipo vingi tu kuna wakati magari ya Azam yakiwa na shehena ya unga(sembe) yalikaa mwezi mmoja Horohoro yamezuiwa kuingia Kenya bila sababu mpaka waziri wetu wa EA alipoingilia kati. Ingawa Kenya wana viwanda vingi zaidi ya Tanzania+Uganda lakini sisi tunauza zaidi Kenya kuliko wao TZ,Tanzania tunaweza kufanya mapinduzi ya Agro-industries tukazizidi nchi zote za EA kwa ujumla wao ifikapo 2020 kwa uzalishaji.Matatizo kama haya yanatakiwa mh Sita na Wabunge wetu ktk bunge la EA wasiyafumbie macho kabisa,tupo makini kwenye ushindani na lazima kuwe na kanuni sawa kwa ubora wa bidhaa ktk EA,kila nchi inawajibika kuvilinda viwanda vya ndani pamoja na wazalishaji wa malighafi wa ndani
 

Kwa taarifa yako siyo Konyagi tu,pombe zote Safari beer ndiyo kabisaaa ukikitwa nayo hata chupa tupu lakini ina label kesi yake ni ya uhujumu, hata vyakula mfano unga wa Azam uwe wa ngano sembe hawataki,Kanga vitenge hadi najiuliza hivi ndiyo aina ya ushikiano wa Afrika mashariki na kibiashara tuliokuwa tunautaka?au viongozi wetu wanatuburuza tu,Wakenya wanachukua machungwa karibu yote ya Moro Muheza hadi viazi vya chips na magogo huko Iringa,mahindi maharage hadi ng'ombe lakini ukipeleka badhaa iliyokamilika kutokana na hizi malighafi zetu hawazitaki lakini wakizipeleka kwao wakazitengeneza wanajisifia na kuzitafutia masoko kwetu,nawasihi viongozi wetu nao waamke wakemee hii tabia ni mbaya sana,sasa imehamia katika utalii, watalii wanaotokea Tanzania pamoja na wewe mtanzania ukienda Kenya huduma yenu ni ghali sana,nashuhudia binafsi nilienda Kenya nikataka kupanda juu ya KICC ili nione mji vizuri niliposema mi ni M_TZ bei ikabadilika ghafla nikalipa kama mgeni kutoka ulaya na zaidi na kufuatwa na mashushushu kibao hadi nikajiuliza ni uhusiano gani huu tunaoutafuta sisi watanzania nchi ya maziwa na asali kwa kuwa na ushirikiano na watu kama hawa?.hivi mbona wakija huku kwetu kila kitu shwari kama watu wengine,lingine nililoligundua wakenya wengi wananunua mahitaji yao vituo vya mipakani mfano Namanga Sirari nilishangaa msururu wa magari kutoka Nairobi kuja Namanga siku ya Jumamosi hadi nikauliza hawa wanaenda wapi nikaambiwa Namanga kununua mahitaji kama sukari ,mchele,mafuta ya kupikia ya alizeti,unga wa ngano na wa mahindi n.k kwani kwao Kenya havishikiki bei hadi maji sikuamini! sasa kwa mshangao wakati wa ku-check out pale Namanga baadhi ya wakenya walikuwa wanatumia pass za Tanzania hata kiswahili chao hakijanyooka,wakati watanzania wengine halali wanatumia pass za muda,ukichunguza magari ya abiria kutoka TZ kwenda Kenya ni mifuko mikubwa mikubwa tu imefungwa kama mitumba kumbe la ni mitumba ya nguo mpya zinenda kuuzwa Kenya kwa bei mbaya sana kwa ujumla niliweza kununua rangi ya viatu na kibiriti huko Kenya kwa sababu ya bei karibu bidhaa zote nzuri zinazouzwa Kenya zinatoka TZ katika njia za panya ila zile formal hawataki hata kuzisikia eti hazina viwango mara zinaua soko lao la ndani,sijui ni aina gani hii ya ushirikiano ila tuwe macho kwani sasa wanachotaka kwetu ni ardhi,tukilegea kidogo tu watahamia wote huku na biashara zao uchwara.
 
...Ok. Next time we will have ask how Azam is giving back to the society-corporate social responsibility.
 
kama kaweza kudhibiti hao nyang'au basi safi sana. Wakenya ni tatizo. Wenyewe kama watu hawana viwango.
 
Tulishawaambia hao sio watu hawatuthamini na walishatyuita Manyang'au leo tunajipendekeza, sasa wameshajazana humu na wamefungua Vyuo eti vya wajasiria mali na kutuajiri wakitaka mwenye Degree wakati wao ni Diploma
Kweli sisi mamburula lakini ipo siku tutagoma na kichapo chake ni kuwatoa na kuvunja Jumuia tena
 
Chukua hii, maji ya uhai yenyewe kimeo, nimetumia mimi mkuu, tumbo linauma mbaya, hayapiti hata mdomoni, il akilimanjaro poa sana
 
Hazina ubora na ukitaka kujua kama una watoto wadogo kwako wape wanywe kwa week moja tu utapata majibu. Zina lots of allergies, tumbo kuuma watoto, vitu vingi saana. Nilipo wastop baada ya kupata ushauri toka kwa rafiki yangu sasa hivi shwari

Jamii ya juice ya wiwandani na soda si nzuri kwa watoto wadogo. Zote usababisha matatizo uliyo orodhesha hapo juu. Hivyo siyo kipimo cha ubora.
 
Kenya wana bahati we dont have the right leaders otherwise protectionism inakuwa practised all over the world.
Lazima ulinde viwanda vyako vya ndani ata any cost including kuyafanyia kazi mapungufu ya bidhaa za ndani which is possible.
Azam anaajiri dada yako na kaka yako pia kuna karevenue kanaenda kwa serikali japo magumashi yapo.
Support Tz products for the growth of our Nations
 

ile ya kijoti?
 
...Ok. Next time we will have ask how Azam is giving back to the society-corporate social responsibility.
huwa amamwaga pesa msikitini siku ya Ijumaa. niliwahi kusikia siku ya ijumaa omba omba wote wanahamia msikiti anaosali BHARESA
 
mpaka hapo bidhaa za TZ zitakapokuwa kwenye ubora stahiki, tutaendelea kulalama hivi hivi na kutafuta visingizio.
Kama serikali ya kenya imeweka taratibu zinazotupa ugumu kuuza bidhaa zetu Kenye, kwa nIni na ya TZ isifanye?
Huwezi kufananisha juisi ya azam na del monte, huwezi kufananisha sanitary towels za jassy na always za Kenya, tanga fresh (ukichemsha yanaganda) na brookeside au tuzo.
Hata pipi zetu ni daraja la chini kulinganisha na zao.

the best we can do is to improve the quality of our products. Wenzetu KBS yao haitaki masihara, yetu hata kitaa unapata nembo, leo nimesikia redioni nembo za TBS maani zinapatikana.

Tuendelee kuwapondelea wakenya basi kama itasaidia kitu.
 
huwa amamwaga pesa msikitini siku ya Ijumaa. niliwahi kusikia siku ya ijumaa omba omba wote wanahamia msikiti anaosali BHARESA
..Jambo zuri. Lakini ningependa kiwe kitu ambacho ni 'sustainable' kama msaada kwenye elimu. Hiyo ya kuwapa watu 10,000 kila ijumaa, na wiki ijayo mtu anakuja kukinga zingine sio msaada endelevu. Ni msaada wa kutukuzana na kutafuta sifa-sio wa kumkomboa mwenye shida. I wish he was more liberal.
 
Ulimwengu huu ni wa kuigilizia sasa wewe-milinganyo hii ni ya enzi hizo usiwatetee jamaa hawa wanoko tu
 
Mimi naishi Namanga mpakani mwa Kenya na Tanzania,kwa kiasi fulani hali ya kibaguzi kutoka kwa Wakenya nina iexperience zaidi.Najua kweli kuwa baadhi ya bidhaa za Kenya ni bora zaidi kuliko za kwetu interms of quality, lakini siyo kila kitu.Kuna vitu vingi sana ambavyo tunawazidi na wao wanatuzidi, ila jambo moja kubwa la kufahamu ni kuwa hawa jamaa ni wabaguzi sana na huthamini sana shilingi yao na hutumia kila mbinu kuilinda! Ilitokea wakati kulikuwa na influx kubwa sana ya machangudoa kutoka Kenya hapa ambao walikuwa wakijiuza ghali tena kwa hela yao ya Kenya au dola tofauti na wakwetu wa Kibongo!! Hapa issue ya quality inakuwa wapi? Ni dhana tu iliyojengeka na kutokujiamiani kwetu ndo maana hata bidhaa zetu wenyewe tunazidharau! Ila kwa taarifa yenu ni kuwa hali hii haitadumu muda mrefu hasa kama tutapata akina Bakhresa wengi zaidi Tz ambao watasaidia kutingisha soko la Kenya na kisha kuliangusha kabisa. Uwezo huo Wa Bongo wanao ila muda tu haujafika!! Time will tell!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…