Vita ya biashara Del Monte Kenya na Azam Bakhresa Group of companies

Na sio Bakhressa peke yake

Mzee Mzindakaya na wafanya biashara wakubwa na wadogo wa Tanzania. Someni hii thread muone jinis gani mawaziri husika walivyokimya na hii inatisha sana. Hivi kama Bakhressa pamoja na ajira na kodi zote anazolipa anatelekezwa na serikali yetu je wewe mfanyaboashara mdogo utaweza kweli?

zaidi soma hapa:

https://www.jamiiforums.com/busines...enya-na-azam-bakhresa-group-of-companies.html


Hatari sana hii
 
Mkuu Ngongo, kiukweli, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!, juice za Azam zimejitahidi sana vifungashio ila sio contents!, huwezi kulinganisha na Del Monte, tena afadhali zile juice kubwa ndio angalau amout ya natural fruit ni nyingi, lakini vile vido wanavyovikimbilia watoto wetu wa shule, vile ni vi chemicals kabisa na flavours tupu!, tatizo hata balancing ni shida hivyo ukinywa tuu vinakereketa!. Hata ICE Cream zake, liko jambo!. Kanunue Ice cream zile za hoteli zozote kula, ukishamaliza kanunue za Azam, kula!, utanotice the diference, najua anatumia maziwa ya unga ila I doubt kama ni maziwa ya ngombe!. Kama Mchina ametengeneza mayai cheaper kuliko ya kuku na kumwangwa soko la Tanzania, why not milk?.

Lazima tukubali kuwa Bhahressa anahitaji pongezi, lakini pia lazima atimize viwango vya ubora!.

Kiukweli sisi Watanzania tumezidi uvivu!, nenda pale Mlimani City sehemu ya mboga moga!, sasa hadi nyanya, kitunguu, karoti, kabichi etc ni imported!. Its a shame!. Hebu someni hapa Sitta anasema nini Watanzania Watakiwa Kuacha Hofu ya Shirikisho la EAC, na Badala ...
Pasco
 
Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani

Juisi za Azam ni mbaya sana. Mwanzoni nilikuwa nadhani ni mimi tu ninayeziona hivyo kwa sababu labda nina tendency ya kuwa choosy.

Lakini hapana, tatizo si mimi. Tatizo ni ubora wa hizo bidhaa zao, hususan hizo za vinywaji.

Zina ladha mbaya. Texture mbaya. Harufu mbaya. Yaani ni mbaya katika almost kila aspect.

Ile juisi yao ya mananasi, kwa mfano, huwa ina ladha na harufu kama ya mananasi yaliyooza.

Juisi yao ya mapera ina texture nzito utadhani uji. Juisi gani nzito hivyo?

Azam cola nayo ina ladha mbovu sana.

Sina hakika kama wana utaratibu wa kupokea consumer feedback na kama wanao ni wapi watu tunaweza kuzipeleka hizo feedback ili walau wajitahidi kuzifanyia kazi.

Mimi binafsi wameshanipoteza kama mteja. Sijui kwa wengine but I'm through with them.

So for the time being I'm sticking with Ceres, Minute Maid, and my own freshly squeezed homemade lemonade.
 
Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani

hapo pana utatanishi, unga wa mahindi na wa ngano kutoka kwa bakhresa unauzwa katika maduka mengi ulaya, binafsi nimewahi kuuona katika maduka ukiuzwa, sasa ikiwa ni kweli kiwango ni kidogo, uingereza imewezaje kuingiza katika soko la raia wake lakini kenya ikawa vigumu? au tuseme serikali ya kenya na kampuni yake ya viwango ni bora kuliko ya waingereza?
 

Bidhaa za Azam hazina ubora wowote hata ufungaji wake haukidhi matakwa ya kimataifa sema tu kwa Tanzania ni jalala la bidhaaa fake fake hakuna noma,wanajamvi mtakubaliana nami kuwa Tanzania ni jalala kila kitu kikikataliwa Kenya kitatupwa Tanzania tuliona na kushuhudia na kusikia kipindi kile kuna Pedi za wanawake almaarufu kama Always hizi zilikuwa hazina viwango na Kenya walisema zinahatarisha afya za wanawake kama watazitumia huenda wakapa madhara kwa sehemu zao za siri wakakataa makonteina yale baada ya siku mbili tatu aaah mbona zilitinga ndani ya Bongo na wakina mama na wadada waliuziwa then baaadae ndio ikajulikana kuwa zilikuwa fake swali nani kazikubalia kuingia nchini sasa ndio sawa na Bidhaa za Azam hata ziwe feki au hazina ubora kwa Tanzania atauza tu na hakuna wa kuzikataa kwani Tanzania maskini hakuna wa kuwatetea wanyonge kila leo utasikia watu wana kansa wakati miaka hiyo tulifahamu kansa ni magonjwa ya kurithi lakini leo hii hata familia haina historia ya magonjwa hayo utasikia kuna mtu ana kansa kumbe ni mijibizaa michafu tuuziwayo lol kwa Afrika Tanzania inajulikana kama nchi inayozoa kila kitu kwani wale jamaa wa viwango wako corrupt ni balaaa kwani tulisoma kwa news mika miwili au mmoja kuwa walicheza movie kama kawaida ya Kibongo bongo kuwa wanayo ofisi kule Korea kumbe ilikuwa hewa hata ile kesi sifahamu iliishaje naona wanakuja na kesi zisizo za msingi kufukia zile za ukweli ama kweli Tanzania kila kitu kinawezekana hata ukitaka Uprofessor kesho tu unapata makaratasi yote.
 

Mkuu,
Nimeingia katika website ya AZAM JUICES na wanatuhakikishia wanafuata viwango vya ubora si wa Tanzania tu bali pia viwango vya kimataifa katika usindikaji, usafi wa mali ghafi na ufungashaji.

Fruit Processing Division

Bakhresa Food Products Ltd (BFPL) has got state of the art fruit and vegetable processing plant of 150 tons per day capacity from Fratelli Indelicate and FBR-ELPO, Italy to process wide range of locally grown fruits and vegetables that include Mango, Pine Apple, Orange, Guava, Passion fruit, Tomato etc.

At BFPL, the choicest fruits are selected, inspected, sorted, washed and then taken to the ripening chambers where they are ripened in a uniform manner under controlled conditions to maintain the color, flavor and taste. The ripened fruits are then thermally processed and aseptically packed in pre-sterilized high barrier bags to retain the natural taste, flavor, color and aroma of the fruit.

The process of manufacture passes through frequent & stringent quality checks for physical, chemical, organoleptic and microbiological parameters and immediate corrective measures are carried out on detection of variance in parameters. The tests are carried out in the in-house laboratory equipped with the latest facilities to perform all necessary tests.

The fruit pulp produced is packed in aseptic bags of 210 Ltrs, which is further packed in a drum.

The BFPL Fruit juice processing plant is the first indigenous aseptic packing facility for fruit juices in Tanzania. The plant has capacity of packing 41 million liters per annum. The product range includes Apple, Azamto (Black currant fruit juice drink), Mango, Orange, Pineapple, Guava, Mango Orange Guava (mix fruit juice drink) and a blend of Apple and Black currant juice.

This is Tanzania’s first food plant certified with ISO 22000 by URS, UK. ISO 22000 includes HACCP. The high quality processing equipment supplied by world renowned manufacturers enables retaining the taste and Aroma of fruits of Tanzania at its best. The process employed ensures best retention of nutrients and originality of the fruit juice. The products are also fortified with Vitamin C (Ascorbic Acid).

Source: Juices Division | Bakhresa Group

Naamini Bakhresa group of companies suala la ubora wa bidhaa zake hulichukulia kwa uzito maana wana viwanda/kuuza bidhaa Rwanda, Uganda, Mozambique, Malawi na Zambia na zoezi hilo hulifanya mara kadhaa kila baada ya kipindi zikiwemo taasisi kama TBS, ISO n.k naona kufanya zoezi hilo kivyao. Bakhresa Group - Reaching life

kuhusu suala la baadhi ya watoto kupata matatizo baada ya kunywa juisi, kitu hiki siyo cha ajabu sana maana kuna baadhi ya watu wana aleji za aina mbalimbali mfano aleji ya maziwa ya ng'ombe akinywa maziwa Milk Allergy Diet

Hivyo mwanaJF yeyote akinywa juisi au maziwa au 'wine' n.k na kupata mtafaruku wa msokoto wa tumbo au aleji basi aende hospitali kwa ushauri ambapo ataelezwa kama ni 'food poisoning au allergy'' n.k Signs of Food Poisoning: How Do You Know If It's Food Poisoning or a Virus? - Yahoo! Voices - voices.yahoo.com

 
Tanzania kwanza mambo mengine baadaye. Iwe Bakhresa au mfanyabiashara mwingine yeyote kutoka Tanzania lazima Serikali ichukue hatua za makusudi kuwalinda na kuhakikisha wanapata soko nje ya nchi ili mradi bidhaa zao zina viwango vya kimataifa. Bila ya Serikali kufanya hivyo wafanyabiashara wetu hawawezi kupenyeza kokote kwani huu ni mfumo unaotumika dunia nzima kwa Serikali kuwalinda na kuwasaidia wafanya biashara wazalendo kwani ndio wanaolipa kodi Serikalini, wanaotoa ajira kwa wananchi na wanaosambaza jina na utamaduni wa nchi sehemu zingine za dunia.

Kuna siku nilienda Kenya maeneo ya Kisumu kikazi na Wakenya wakawa wanasema bila aibu kwamba wakiona biashara ya Mchaga basi hawanunui!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hivyo haya si mambo ya mchezo. Hivi hatuelewi kwamba hawa watu ni wakabila sana?

Kuna kila haja kwa Serikali yetu kuanzisha mfumo wa Quota ili wafanyabiashara wetu waweze kupata masoko kenya. Haiwezekani wao washikilie zaidi ya asilimia 60 ya uchumi wetu katika kila nyanja halafu wasitake kuona bidhaa na huduma zetu zikipenyeza kwao. Huu ni upuuzi wa hali ya juu!!!
 

Mkuu unachosema ni sahihi 100%. Lakini kwa serikali hii ya ccm hilo haliwezekani hata kidogo.... ccm ni tatizo kuliko hata tunavyofikiria...
 
Watanzania sijui sisi ni viumbe wa aina gani, yaani kwenye bidhaa zote za BAKHRESSA lazima uone nembo ya International standard kuonyesha bidhaa ina-comply viwango vya kimataifa lakini kwa majungu yetu watu wanakuja na comments utafikiri ni wataalamu wa kupima viwangu vya bidhaa za vyakula.

Kwani hiyo Del Monte inafuata viwango gani vya ubora kama siyo ISO hiyo hiyo anayoifuata BAKHRESA?Au viwango vya wakenya vimethibitishwa na Mungu? Lazima serikali ifuatilie suala hili kama kweli lipo vinginevyo tutaendelea kulalamika kunyonya na mataifa ya magharibi kila siku kumbe sisi wenyewe waafrika miongoni mwetu ni tunafanyiana husda.
 
Wakuu Pasco & Nyani Ngabu

Mnaweza kuwa sahihi kuhusiana na ubora wa Juice za Azam lakini ukichunguza sana utabaini Kenya wana protect soko lao hasa wanapobaini bei ya bidhaa toka nchi mwanachama wa EAC inaweza kuhatarisha soko la bidhaa zinazozalishwa Kenya.Nimetoa mfano wa matairi ya General Tyre yalikuwa na soko kubwa kenya na Somalia kilichofanyika ni kuzuia tyres zisiingie kwenye soko lake na kuhakikisha wasambazaji wote waliokuwawakipeleka tyres Somalia waacha mara moja.Kiwanda cha kusindika nyama SAAFI,kuna kiwanda cha kusindika maziwa Musoma na nk.Vipi Konyagi imekosa viwango,Bia ya Kilimanjaro ?.........

Kuna ufisadi mkubwa unaofanywa na kiwanja cha ndege JomoKenyatta dhidi ya biashara ya maua ya Tanzania.Kwanza yanacheleweshwa,pili wanahakikisha maua yote ya Kenya yakishanadiwa ndiyo maua ya Tanzania yanaruhusiwa kusafirishwa.Jambo limeshalalamikiwa sana na jumuiya ya wafanyabiashara ya maua upande wa Tanzania lakini hakuna hatua mahususi zilizochukuliwa.Suluhisho la muda mrefu ni uwanja wa ndege KIA kuwekewa majofu na ndege nyingi za kimataifa kuutumia uwanja wa KIA.Tayari Kenya ina mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa mpakani (Holili) kilometa chache toka uwanja wa KIA nia ni kuhujumu biashara ya utalii na bidhaa za Tanzania zisivuke mipaka kwa urahisi.




 
Last edited by a moderator:
wakenya bana wana roho mbaya sana!

Hii EA wanaitaka kwa maslahi yao wenyewe, lazima sisi wabongo tukae mguu sawa.

Wakija mapebari wa kikenya utashangaa wananunua eneo kama mkoa mzima.
 

Ndiyo maana nasema hata kwa EAC with common market bado tanzania itakuwa dumping place ya bidhaa za Kenya!!! Na kwa taarifa ni kuwa Kenya wana export nje ya Africa Mashariki bidhaa bora sana, same bidhaa ikiwa Tanzania ni sub-standard na wanasema wazi!! Siwataki wakenya hata kidogo. Kwanza hawana upendo kwa watanzania kabisa, wanatuita wakora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…