G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 30
- 23
Najua kwa sasa hoja na habari kuu ni "Mauaji ya Asimwe" na nitakuja kusema kuhusu hili, lakini kwa vile sikupata fursa ya kutoa maoni yangu kuhusu suala la DC Ubungo kukamata watu na kuwaweka ndani kwa kosa la "kufanya ukahaba", tena kwenye siku ya siku kuu huku akiagiza mara baada ya siku kuu wafikishwe mahakamani na mahakama ichukue hatua za kisheria, naomba mnivumilie niulize maswali machache ya mantiki na ufahamu.
Kwanza ni namna "ukamataji" ulivyofanyika. Mheshimiwa DC amekwenda na askari na vyombo vya habari kuwakamata "watuhumiwa wa ukahaba". Kweli ukahaba ni kosa kwa sheria za Tanzania na hata kwa maadili yetu tu, si jambo linalokubalika; lakini nilidhani kwa misingi ya kisheria, mtuhumiwa anazo haki zake zinazopaswa kulindwa hadi anapothibitika kuwa na hatia! Kama tumemuweka "mtuhumiwa" mbele ya vyombo vya habari kwa "tuhuma", tukamshikilia mahabusu kwa saa 24, na kisha mahakama ikamkuta "hana hatia" baada ya kumsikiliza na kugundua huenda alikuwa 'anapita tu njia na akawa anasalimiana na mtu wakati DC na kikosi kazi nao wanafika "kukamata", tunamfidiaje huyu kwa udhalilishaji na madhara yaliyotokea kwenye jamii kwake na kwa familia yake!!? Kwanini tumemhukumu (kwenye media/public) kabla mahakama haijatoa hukumu!!? Tumetaka kuonyesha tu kwamba tunakamata "makahaba" bila kulinda haki za kisheria za watu kwa sababu gani!!?
Kisha kuna suala la "ushahidi". Hivi tunao ushahidi wa kutosha kuthibitisha "pasipo kuacha shaka yoyote" kwamba wafu wale tuliowakusanya kwa mtutu wa bunduki, mbele ya wanahabari, na kuwaweka rumande kwa tuhuma za "kufanya ukahaba" walikuwa kweli "wakifanya ukahaba" kwenye eneo lile!!? Tunaweza kuthibitisha hili kwa kujibu wa sheria tena pasina kuacha shaka, au tumewakamata na kuuambia umma kwamba ni "makahaba" lakini tutatafuta shitaka litakalofaa kwa mazingira yale ili tuweze kuwafikisha mahakamani kwalo!!? Busara hapa ya Mheshimiwa DC na Mwanasheria wa Halmashauri zinatuelekezaje!!? Au ndiyo tumeamua we are "all in one" yaani wapelelezi ni sisi, wakamataji ni sisi, washitaki ni sisi, mahakimu ni sisi, wazee wa baraza ni sisi, mabwana jela ni sisi sisi!? Nawaza tu!
Hivi sheria ya Tanzania inasemaje kuhusu "ukamataji" wa makosa ya jinai!!? Tunakamata ndipo tuanze upelelezi au tunapeleleza, tunapata ushahidi, ndipo tunakamata ili tushitaki!!? Kama ni kamata kwanza, peleleza baadaye, tunajiepushaje na mashtaka yatakayofuatia kushindwa kesi hizi (jambo ambalo naona kama ushahidi wa "ukahaba" wa makahaba wetu hawa utakuwa mgumu)!!?
Anyway, aliwahi kusema Mwalimu Nyerere kwamba "sheria na haki ni mawili tofauti" na sasa nadhani naanza kuelewa.
Wasalaam!!!
PIA SOMA
- Tetesi: - Waliokamatwa kwa tuhuma za kununua Makahaba Ubungo kumburuza mahakamani Mkuu wa Wilaya kwa kudhalilishwa! Wadai walifuatwa Guest!
- Kuna kesi ya udhalilishaji kama wale walioonekana kwenye video ya kukamata makahaba watapata mwanasheria mzuri
- Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?