BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 9,528
- 24,071
Katika vita yoyote, mshindi mara zote ni yule mwenye kisosi jasiri, nyenzo za vita, na mbinu za ushindi. Hata hivyo, ujasiri ndio kiambata muhimu zaidi katika saikolojia ya mwanajeshi.
Bila ujasiri na morali, nyenzo za vita zinaweza zisiwe na maana sana, na unaweza ukajihakikishia kuwa, jeshi litapigwa na kusagika.
Kwa msingi huo, ili kushinda vita dhidi ya jeshi lingine, lazima ujasiri wa jeshi la adui uvunjwe vunjwe kwa kutumia propaganda na mbinu zingine za kisaikolojia za kuwashusha morali wanajeshi wa upande wa pili.
Propaganda kama za mishahara duni, au kuwafanya wajione dhaifu, au kuwaonesha maguvu ya jeshi pinzani, vyote hivyo vinaweza kuvunja vunja utayari na kujiamini kwa kikosi husika.
Bahati mbaya mbinu hizi za kisaikolojia zinaweza kutumiwa na jeshi dhidi ya raia, na zikafanya kazi vizuri sana kwa kuwa raia hawana ufahamu, uwezo wala mikakati ya kudhibiti propaganda na mbinu za kisaikolojia zinazotumiwa dhidi yao.
Ni lazima magari ya jeshi yajipitishe barabarani ili wanaotarajia kuleta fyoko wasithubutu kusogeza hata ukucha nje. Si kwa sababu ya hatari halisi, lakini kwa sababu ya hofu ya hatari inayotarajiwa.
Suala si kudhibiti maandamano, suala ni kuyazuia kabla hayajatokea bila kusababisha madhara yoyote.
Mtu mmoja anauliza kwanini jeshi lisisubiri siku husika? Kudhibiti kuna sadaka na gharama. Lazima damu imwagike kidogo. Hawako tayari kubeba gharama hiyo.
Kwa muktadha huo, wanaotarajia kuandamana kwenye ile nchi ya Afrika mashariki wasithubutu.
Nimepata taarifa hapa kwamba kuna virungu spesheli vimeandaliwa vina michongoma kwa mbele. Ukigongwa ugoko lazima upumue kwenye matundu yote matatu.
Piga kura nenda ukalale.