Vita ya Kiuchumi: Ningekuwa Rais wa Tanzania ningeanzisha ujenzi wa reli ya SGR kutokea Bandari ya Tanga hadi Kagera, Rwanda na Uganda

Kuwa na Fikra za Kumpa Mandate Mtu (Rais) ndio afanye cha kufanya ndio mzizi wa makosa Nchi haipaswi kuendelezwa kwa fikra za mtu..., bali collectively wadau wote kwenye sekta zote kwa kuangalia long term pro and cons na vipi kimoja kina complement vingine.....

In the best case scenario huyu Rais sasa hivi angekuwa anaendeleza na kuboresha mawazo ambayo mzizi wake ulikuwepo hata miaka mia moja iliyopita..., Hio ndio tunaita DIRA
 
DIRA yenyewe ndo kwanza wanakusanya maoni sasaivi.

Kwa hali ilivyo twende hivi hivi, hiyo DIRA itatukuta. Dunia inakimbia sana na maamuzi haya yanapaswa kufanywa wakati huu!
 
mkuu, tayari bandari ishapanuliwa meli zinazotia nanga tanga ni sawa na zile za dar na tayari kuna ongezeko kubwa la meli. kuhusu sgr, kutoka tanga kwenda kagera kupitia wapi? geographia hairuhusu, kuna bonde la ufa, kuna mbuga ya serengeti na kuna lake victoria,

Lakini pia wazo lako lilishafanyiwa kazi kuna bomba la mafuta kutoka hoima kwenda Tanga nalo lina manufaa sawa au zaidi ya sgr.

ushindani na kenya hizo ni siasa tu strategycally kenya sio mshindani wetu mshindani wetu ni africa ya kusini na angola hilo somo nitaleta siku ingine.

Sgr ya tz na kenya kuwa katika ushindani, sgr yetu inatumia umeme ina rated speed ya 160mph, ya kenya inatimia diesel rated speed ni 120kph, hivyo yakwetu ipo kwenye best comperative advantage. treni ya kenya itatumia lita za diesel elfu 20 sawa na 70m za kitanzania wakati yakwetu itatumia umeme wa lakitano tu kugika kigali. niishie hapa kwa leo

Hakuna faida upotevu tu wa pesa.
Nadhani sio kupoteza pesa labda tuanze na lipi na kifuate kipi?
Hizo zote ni njia mbadala.
Labda tuanze na kuzalisha chuma chenyewe Mchuchuma- Liganga kupata mataluma ya reli.
Pili tujenge Reli Kutokea Mtwara Port kwenda Malawi na Zambia.
Tatu tujenge reli kutokea Isaka kupitia Kagera itakayounganisha Uganda na Rwanda.
Nne Tanga Port kuunganisha na reli ya kati via Morogoro au Dodoma kwenda Tabora ikiwa na njia yake.
Tano ni Arusha kupitia Korogwe kwenda Tanga.
In 30 to 50 years haya yanawezekana bila kusahau kuja kwa tekinologia mpya mbeleni ambazo tunachokitaka leo kitakuwa archives kwenye nyumba za makumbusho.
 
Reli kutoka mtwara port haitaweza kufika Malawi maana Nyasa kuna ziwa. Suluhisho ni kuweka tawi la Tazara Mbeya mjini lishuke hadi kyela kuingia Malawi.
 
Wewe utakuwa mnywarwanda. Soko kubwa liko DRC, Zambia, Malawi na ndio zinafuata hizo nchi ambazo ni kama mikoa tu.
 
Kaskazini ya Malawi kwenda mji wa Kalonga Malawi hakuna maji yaani ziwa.Reli inapitika vizuri mkuu kuunganisha na Zambia. Angalia ramani ya Malawi.
 
Ukielewa faida ya ujenzi wa reli ni ipi huwezi kuandika mashudu uliyoandika hapa.

Faida ya ujenzi wa reli hii ni kusafirisha mizigo ambapo gharama za usafirishaji huo ndo pesa zitakazoinufaisha nchi.

Sie tukiacha kufanya maana yake anayekwenda kufanya kile tulichopaswa kufanya ndiye atakayenufaika zaidi
Ni vigumu wewe kuelewa umuhimu WA kujenga Reli Kwanza nchini mwako kuamsha uchumi

Kongo NI nchi tajiri kuliko nchi yeyote duniani Kwa Mali asili hasa madini lakini NI nchi maskini mno sababu haina miundombinu ya kuyatoa hayo madini na kuyasafirisha

Mfano kusafiri toka Kinshasa hadi Katanga NI safari ya miezi mitatu
Kwa gari tena kufika NI bahatigari utaliacha screpa hukohuko au ukienda ukirudi madaraka yote ya miti hayapo au unakuta barabara imesombwa na maji haipo
 
Wewe utakuwa mnywarwanda. Soko kubwa liko DRC, Zambia, Malawi na ndio zinafuata hizo nchi ambazo ni kama mikoa tu.
kabisa, na mizigo hii ya zambia drc south africa wanainyemelea na angola nao wanaitizama kwa hamu, hivyo tukifocus kwenye hizi nchi ni more important kuliko uganda na rwanda ambavyo hamna chochote porojo tu
 
Nadhani sio kupoteza pesa labda tuanze na lipi na kifuate kipi?
Hizo zote ni njia mbadala.
Labda tuanze na kuzalisha chuma chenyewe Mchuchuma- Liganga kupata mataluma ya reli.
Pili tujenge Reli Kutokea Mtwara Port kwenda Malawi na Zambia.
Tatu tujenge reli kutokea Isaka kupitia Kagera itakayounganisha Uganda na Rwanda.
Nne Tanga Port kuunganisha na reli ya kati via Morogoro au Dodoma kwenda Tabora ikiwa na njia yake.
Tano ni Arusha kupitia Korogwe kwenda Tanga.
In 30 to 50 years haya yanawezekana bila kusahau kuja kwa tekinologia mpya mbeleni ambazo tunachokitaka leo kitakuwa archives kwenye nyumba za makumbusho.
Hakuna linaloweza fanikiwa na kuleta tija.

Unaiwazia Tanzania maendeleo na mabadiliko kama vile Tanzania ni Japan ama China.

Huwezi fanikiwa lolote kama una serikali mbovu.
 
kabisa, na mizigo hii ya zambia drc south africa wanainyemelea na angola nao wanaitizama kwa hamu, hivyo tukifocus kwenye hizi nchi ni more important kuliko uganda na rwanda ambavyo hamna chochote porojo tu
Tayari mazungumzo na China yanaendelea kuiboresha Tazara kwa kiwango cha SGR. Nina uhakika kwenye hili wataifikisha hadi Kusini mwa Congo kwenye mji wa kibiashara Lubumbashi.

We can grab opportunities zote za kusini na kaskazini kwa kuwa The Logistic Hub of East and Central Africa. Hakuna shida yeyote tukikamata fursa kotekote. Zaidi ni faida kubwa zaidi kwetu!
 
kabisa, na mizigo hii ya zambia drc south africa wanainyemelea na angola nao wanaitizama kwa hamu, hivyo tukifocus kwenye hizi nchi ni more important kuliko uganda na rwanda ambavyo hamna chochote porojo tu
Rwanda inaweza ikawa isiwe na mizigo mingi ila Uganda na Sudan Kusini zinaweza kuwa na faida kubwa sana huko mbeleni.
 
Ni vigumu wewe kuelewa umuhimu WA kujenga Reli Kwanza nchini mwako kuamsha uchumi

Kongo NI nchi tajiri kuliko nchi yeyote duniani Kwa Mali asili hasa madini lakini NI nchi maskini mno sababu haina miundombinu ya kuyatoa hayo madini na kuyasafirisha

Mfano kusafiri toka Kinshasa hadi Katanga NI safari ya miezi mitatu
Kwa gari tena kufika NI bahatigari utaliacha screpa hukohuko au ukienda ukirudi madaraka yote ya miti hayapo au unakuta barabara imesombwa na maji haipo
Congo ni potential kwa pande zote, kusini, katikati, kaskazini na Mashariki.

Kwa sasa Katikati mwa Congo tumesha unlock kwa kujenga Bandari ya Kalemi kule Tanyangika. Kinachotakiwa sasa ni kupeleka meli kubwa zenye uwezo na uwekezaji mkubwa wa Mashine za kisasa za kupakia na kupakua mzigo. Pili ni ujenzi wa Barabara ya Mpanda hadi Tanganyika kwa kiwango cha rami/ zege.

Mashariki na Kaskazini mwa Congo ambapo napo kuna uzalishaji mwingi kuna hatari kubwa reli yetu itakayoingia Burundi kisha Congo kutopata mizigo ya kutosha endapo reli ya Kenya itakayoingia Uganda ikifika Congo kupitia Uganda.

Ni muhimu hizi nchi zikaitegemea Tanzania kwa urahisi wa usafirishaji wa mizigo yao. Na ili hili lifanyike wakati ni sasa! Tuamue na tufanye
 
Hakuna linaloweza fanikiwa na kuleta tija.

Unaiwazia Tanzania maendeleo na mabadiliko kama vile Tanzania ni Japan ama China.

Huwezi fanikiwa lolote kama una serikali mbovu.
Maendeleo yanaletwa na mtu mmoja mmoja.hata uvumbuzi ni wa mtu sio wa umma mfano ni antibiotic peninslin ,cocacola,traffic light, ndege n.k
Bila kuwepo serikali maisha yanakuwepo.
 
Africa hali ni tofauti
 
Maendeleo yanaletwa na mtu mmoja mmoja.hata uvumbuzi ni wa mtu sio wa umma mfano ni antibiotic peninslin ,cocacola,traffic light, ndege n.k
Bila kuwepo serikali maisha yanakuwepo.
Unasikitisha sana.
 
Rwanda inaweza ikawa isiwe na mizigo mingi ila Uganda na Sudan Kusini zinaweza kuwa na faida kubwa sana huko mbeleni.
Uganda na Sudan hamna nchi hapo, ni wastage of time kuzifikiria, uganda hawana product hata ya kujaza meli moja, its only oil ambayo tushalamba deal. sudan ya kusini hamna biashara, bomba la mafuta linaenda khartom na walishalishana yamin hamna kuvunja mkataba.

80% ya logistics za darport ni zambania na congo zinazobaki ndo wengine wanagawana. kukaa na kuwazia uganda na south sudan ni ujuha tu.
lets focus on zambia drc zimbabwe malawi n msumbiji, northen mozambique wanategemea sana logistics kutoka tanzania.

katika report ya world bank ya african intra trade statistics tanzania ni ya kumi katika ufanyaji biashara na nchi zingine za africa. tunapaswa kukuza zaidi angalau tuwe top three. katika ukuaji wa kibiashara yaani trade grouth rate ni ya 4 ikiwa na ukuwaji wa 11.29% na business balance ya 2.27.
 
Uganda cargo zao nyingi zinapitia Mbombasa. Na Uganda anafanya mapinduzi makubwa sana ya Viwanda.

Pia South Sudan still ni potential kibiashara maana anahutaji sana bidhaa kwa ajili ya kuijenga nchi yake. Wao ni landlocked na wanategemea sana Kenya na Uganda.

Congo upande wa mpaka wake na Uganda pako active zaidi kuliko upande wa border yake na Rwanda pamoja na Burundi hivyo kuna faida zaidi kuingia Congo kupitia Border yake na Uganda.

Bidhaa nyingi zinazoenda Congo kupitia Tanzania zinapitia njia ya Tunduma then Zambia ambapo pia TAZARA inaboreshwa.

It's a matter of time but the future is promising. Tunahitaji tu kufanya maamuzi magumu
 
Vita vya kiuchumi ni pamoja kutumia akili vizuri.
Utajihangaisha vipi kwenda Sudan Kusini na huku biashara imejaa tele huku kwingine kote?

Kupapatika kwa vile huyo anayekupiga vita anataka kukupoteza lengo, hiyo nayo ni mbinu ya vita. Acha Sudan Kusini na Ethiopia washiriki kwenye (LAPSSET) Lamu Port South Sudan Ethiopia Transit; au hujawahi kusikia mpango huo? Bandari ya Lamu tayari inazo ghati tatu katika mpango huo.

Hata hivyo, ninakubaliana nawe juu ya SGR tokea Tanga hadi Musoma; lakini ni lazima uelewe kuwa uwepo wa SGR pekee si hoja. Ni lazima Bandari zetu zote ziwe na ufanisi katika huduma zake. Burundi na Rwanda, hata sasa, bila kujali uwepo wa SGR, wanalilia kwenda Mombasa, pamoja na kwamba ni mbali zaidi ya Dar. Sababu kubwa inayo wapeleka huko ni ufinyu wa huduma wa bandari zetu.

Kwa hiyo kiufupi, Ujenzi wa SGR ni lazima uambatane na kuimarisha huduma za bandari zetu zote muhimu - Tanga, Dar, Musoma, Mwanza, Kemondo, Mtwara .n.k..
Ni muhimu sana Kuwepo na Bandari ya Bagamoyo, kubwa zaidi na yenye uwezo wa kuhudumia nchi zote zinazohitaji kuhudumiwa nasi, kama vile: DRC, Zambia, Malawi, Burundi, Rwanda; na kujihudumia vizuri sisi wenyewe, kwa maeneo kama Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Manyara, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, n.k., n.k..
 
Back
Top Bottom