Vita ya mboga

Vita ya mboga

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Nyanja: Mahusiano

(Siyo tukio halisi)

Wateja wa mgahawa mmoja wa chakula unaoitwa Kowak 4 Star Motel ulioko Ingri-Juu Wilayani Rorya wamefikishwa kituo cha Polisi baada ya kupigana vibaya sana na kuharibu mali za mfanyabiashara wa mgahawa huo ndugu Mahende Koroso mzaliwa wa Bumera. Kwenye mahojiano kituo cha Polisi, mmiliki wa mgahawa huo Mahende Koroso alisema mteja mmoja ambaye amehamishiwa Rorya ndugu Wambura Bita Magige alifika na wenzake muda wa kupata chakula cha mchana akiwa ananuka bangi, baada ya mgahawa kujaa wateja ndipo Wambura Bita Magige akamfuata mmiliki wa mgahawa Mahende Koroso ambaye wakati huo alikuwa akiwaratibu wahudumu wake katika zoezi la ugawaji chakula; na kuanza kumfokea akisema kwamba wafanyakazi wote wa serikali (sekta rasmi) wapewe maharagwe kwa sababu ndiyo mboga ya serikali (waienzi serikali muajiri wao) na wafanyakazi wa sekta binafsi (ambaye naye Wambura Bita Magige yumo) wapewe nyama, kuku na samaki ambazo ndizo mboga za sekta binafsi. Mmiliki Mahende Koroso alipojenga hoja kwamba yeye kwake ela ni ela tu hakuna ela ya sekta rasmi wala sekta binafsi hivyo anagawa mboga bila kujali mteja anatoka sekta gani. Kauli hiyo ikamchefua Wambura Bita Magige aliyezua madai haya, ndipo akavamia na kuteka nyara vyungu vya mboga za nyama, kuku na samaki na kuanza kuwagawia wafanyakazi wa sekta binafsi kwa sharti la kumuonyesha kitambulisho cha kazi kwanza ili akutambue kama ni wa sekta binafsi huku akiachana na chungu cha maharagwe, unalipa ela kwa Cashier kwanza ndipo anakupakulia mboga. Mmiliki wa mgahawa Mahende Koroso akaingiwa hofu kwamba hesabu zitakata kwa kuwa Wambura Bita Magige hajui kukadiria kipimo cha kupakua mboga, alipoingilia kati ndipo wafanyakazi wa serikali (sekta rasmi) waliokuwa wakishuhudia vitoweo vya nyama, kuku na samaki vikiondoka huku wao wakisisitizwa wamsubirie mpakuaji wa maharagwe atakapopatikana; wakaungana naye mmiliki Mahende Koroso kumshambulia Wambura Bita Magige na kusababisha vurugu kubwa zilizoharibu mali za mgahawa. Vurugu zilipokosa udhibiti mmiliki Mahende Koroso akapiga simu Polisi na kuja kuwazoa wateja wote kwa mahojiano.

Naomba kura zote.
 
Back
Top Bottom