MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Siasa zetu na nyomi huwa haziachani. Wataalamu wa mambo wanadai chama kinachojaza nyomi kwenye mikutano yake ndio chenye uwezekano mkubwa wa kushinda kwenye uchaguzi.
Sasa hivi nyomi si la uchaguzi tena bali ni pro ubinafsishaji bandari (CCM) dhidi ya anti ubinafsishaji (CHADEMA).
Siku tatu zilizopita CHADEMA walikinukisha vibaya maeneo ya Temeke japo kuwa na hali mbaya ya hewa watu walijaa mpaka kumwagikia Kuja kuziona top guns za CHADEMA zikimwaga madini. Kila mtu muhimu alikuwepo uwanjani kutoa maarifa isipokuwa Lissu tu.
Wasomi , wataalamu wa sheria, wanauchumi, viongozi wa dini wote walizungumza. Uwanja ulikuwa umejaa mpaka hamna sehemu ya kutemea mate.
Tarehe 30/07 CCM wako Kirumba Mwanza, tofauti na CHADEMA wao wanategemea kuzungumzia yote walioongea CHADEMA lakini Kinyume. Pamoja na makada wengine wadogowadogo vigogo kadhaa wataongea wakiongozwa na Chongolo, Jerry Slaa na Kitila Mkumbo.
Pamoja na Mambo mengine wadadisi wa mambo wanasema itakuwa vigumu Sana kwa CCM angalau kufikia nusu ya nyomi la CHADEMA.
Muda ni mwalimu mzuri.
Uzi huu huu utakuletea unachohitaji trh 30.