Vita ya pili ya dunia katika picha (WW2), tupia uliyonayo

Mkuu naona umeiva sana kuhusu vita ya pili ya dunia...Swali langu je kati ya russia na muunganiko wa british na u.s.a ni nani alikua tishio kwa Nazi.Pia ni nani kati yao alie sababisha kwa kiasi kikubwa kwa kushindwa vita kwa ujerumani?
Kwa mchakato mzima wa vita vya pili vya dunia, Hitler aliweza kuwamudu muunganiko wa UK na US, vizuri tu, ila aliharibu pale alipoanzisha vita ya "Operesheni Barbarosa" na Muungano wa Kisoviet,

Hii alisababisha kukunyongea kwa uwezo wa kuhimili na kumudu kuhudumia pande zote mbili za kivita.
Pia kutokana na Ukubwa wa nchi na jeshi la muungano wa kisoviet, hii ilimbidi apeleke huduma zaidi kwenye hii vita na kudharau muungano wa UK na US ambao walitumia mwanya huu na kuweza kufanya uvamizi kwenye fukwe za ufaransa kwenye operesheni ijilikanayo kama D-DAY.

Hitler aliwaaona wa Soviet kama watu dhaifu na sio binadamu kamili na wanatakiwa watawaliwe na kutumikia muendelezo wa ndoto za Third Reich, hapo ndipo alipoingia cha kike alivyoanza vita nao.
 
Lakin pia Hitler alikubaliwa sana na Italy na Japan walimsapoti sana,walimpa nguvu na walimpa wanajeshi makini
 
Aina hii ya miwani inaitwaje!?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…