GE2025 Vita ya udiwani Mawenzi; Wananchi wachoshwa na diwani aliyekaa zaidi ya miaka 15 bila mafanikio

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
G

guest-1787180022

Guest
WANANCHI WA KATA YA MAWENZI WAAMKA:
WAMCHOSWA NA DIWANI ALIYEKAA MADARAKANI ZAIDI YA MIAKA 15 BILA MAFANIKIO

Moshi, Tanzania
– Katika kile kinachoonekana kuwa mwamko mpya wa kisiasa miongoni mwa wananchi wa Kata ya Mawenzi, Moshi Mjini, wananchi wengi sasa wameamua kusema wazi kuhusu kutoridhishwa kwao na uongozi wa diwani aliyepo madarakani ambaye ameongoza kwa zaidi ya miaka 15 – lakini bila kuwa suluhisho la matatizo yao ya kila siku.

Diwani huyo anayejulikana kwa jina la APAIKUNDA NABURI ambaye ameshika wadhifa huo wa udiwani kwa zaidi ya miaka 15 ( Diwani Viti maalumu- 2005-2010, Diwani wa kuchaguliwa- 2010-2015, Diwani wa kuchaguliwa 2018-2020, Diwani wa Kuchaguliwa 2020-2025)

Kwa mujibu wa maoni ya wakazi wa eneo hilo, diwani huyo amekuwa mbali na maisha halisi ya wananchi, hajawa sauti ya wanyonge, wala hajatekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kuunganisha jamii na kusukuma maendeleo ya kweli. Wananchi wanasema kwa uchungu kuwa kiongozi huyo amekuwa kiongozi wa timu yake binafsi, badala ya kuwa kiongozi wa watu wote, Pamoja na kutaliwa na visasi na vinyongo kwa wale wanaodhubutu kumpa changamoto katika nafasi yake.




Uongozi Usio na Dira Wazidi Kuwakatisha Tamaa Wananchi

Wananchi wanasema kwa kipindi chote cha utawala wake, diwani huyo hajawa na dira ya maendeleo, hajashughulikia miundombinu ya msingi kama barabara za mitaa, huduma bora za afya, ajira kwa vijana au hata miradi ya kuinua uchumi wa kata. Badala yake, amejikita katika maslahi binafsi na kudumisha kundi la wafuasi wanaomlinda kisiasa.

Kiongozi huyo, licha ya utendaji wake duni, bado amejitosa tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu kuwania kipindi kingine. Hali hii imezua mjadala mkali mitaani na mitandaoni, huku wengi wakieleza kuwa ni wakati sasa wa kufanya mabadiliko na kumpa nafasi kiongozi mpya.

“Kiongozi wa kweli ni yule anayesikiliza wananchi wake, si anayewatumia kama kura na kisha kuwasahau,” alisema kijana mmoja kutoka Mawenzi, aliyejitambulisha kwa jina la Michael.



Sasa Ni Wakati wa Mabadiliko

Wito wa wananchi wa Kata ya Mawenzi ni mmoja tu: Mabadiliko ya kweli. Wanahitaji kiongozi mwenye maono, aliye tayari kushirikiana na jamii, na anayetambua dhamana ya uongozi si kama heshima binafsi bali kama nafasi ya kuhudumia wananchi.

Wananchi wanawahamasisha wagombea wenye nia ya dhati kujitokeza, hasa wale wanaokuja na ajenda ya maendeleo, usawa, uwazi na mshikamano wa kijamii.

Kata ya Mawenzi inahitaji uongozi mpya – uongozi wa matumaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…