Vita ya Uganda kwa Echolima

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Ndugu Wana Jamii Forum, Humu Ndani Tume Bahatika Kuwa Na Mdau Echolima, Alishiliki Vita Ya Uganda, Kama Unaswali Tunaweza Tukamuuliza, Kama Unajibu Bara~bara Zaidi Unaweza Ukamsaidia Pia Kujibu. Naanza___ 1) Eti, Nimesikia Kuwa Mambo Mengi Tunayo Yasikia Kumuhusu Amini Kama Kuzamisha Mto Kagera Vikongwe, Kula Nyama Za Watu, Kufanya Ngono Hovyo, Kuua Hovyo Na Mengi Mengineyo, Yalikuwa Ni Plopaganda Za Uongo Alizo Ziandaa Mwalimu? Maneno Haya Yana Ukweli?
 




Mkuu!

Yaani umenifanza nicheke pita kiasi! Kwi! Kwi! Kwi!

Watu wengi waliingiwa na zile propagandas za ki-Communist za yule Nyerere na matokeo yake waliamini/wanaamini utumbo na uharo mwingi mno waliolishwa!

Ukiangalia kwa upande mwingine;Nyerere alichochea saana na kusababisha mgogoro ulioleta ile vita dhidi ya Uganda/Amin kwa miaka kadhaa, kabla ya Amin kuchoshwa na vile vitimbi ndipo akaamua kuchukua zile "hatua za kijeshi"!

Tanzania "ilifuga",kuwafunza na kuwagharamia mno magaidi wengi wa kutoka Uganda,baada ya Milton Obote kuondolewa madarakani na Amin. Matokeo yake, hayo magaidi kwa masaada wa Nyerere walikua haweshi kuleta chokochoko na kuihujumu Serikali ya Uganda khasa tokea maeneno yaliokua mipakani na Tanzania.

Yule Obote nae aliporejeshwa madarakani mara ya pili kwa msaada na maguvu ya Nyerere;inajulikana yakuwa ndo aliuwa na kubaka vikongwe,watoto,wanawake na kufanza unyama/uharamia mwingi mno wa kulipiza kisasi kwa Wananchi wake wa makabila mengine na Wapinzani wake wa kisiasa kuliko hata huyo Amin!

Kwa kifupi sina haja wala madhumuni ya "kumtetea" Idd Amin,kama naye kuna yoyote mabaya alofanza na yaliwahi kuthibitishwa...lakini lazim wakti mwingine tujifunze kuangalia majambo kitaaluma na bila ya ushabiki au propagandas za ma-Dictators wengine!

Najua hii thread yako wengi wataichungulia tu kwa mbali na kukimbia kuchangia/kutoa hoja...lakini usijali. Sisi wengine wachache tunajaribu kukufahamu mantik yako japo umeandika kwa maskhara kiduchu! Kwi! Kwi! Kw!

Huyo Echolima unaemtaja;hakuonekana tena kuja kumalizia ile story/thread yake ya "Vita ya Kagera"...nakumbuka mara ya mwisho alitupa ahadi ya kusuburia kwa wiki mbili, lakini sasa yakurubia takriban mwezi wa pili!?

Imepatikana khabar yakuwa huyo Echolima ati ameanzisha thread/mnakasha mwengine kuhusu "vita ya Waarabu na Israel" humuhumu Jf!? Kwi! Kwi! Kwi!

Ahsanta.
 
Unajua Mwalimu Nyerere bwana alikuwa na mambo mengi sana, eti mkombozi wa Africa haya sasa waje wachambue vizuri watuelezee vizuri
 
na clips za video za amin alitengeneza nyerere..?? mbona zinaonyesha matendo.hayo...
 

JIFUNZE KISWAHILI EWE MGANDA..

majambo - mambo

kufanza - kufanya


NYERERE NI BABA WA TAIFA,HIVI TUNAJIANDAA KWA AJIRI YA KUMBUKUMBU YA SIKU YAKE YA KIFO 14/10..
 
Aliondokea OKELO, Alikuwa Askari Mwiba Kwa Amin. Ni Kati Ya Watu Wachache Walio Diriki Kumuhoji Amin! Inasemekana Alitoweshwa Ghafla Wakati Wa Amin. Sasa Nauliza Huyu Okelo Ndie Yule Kiongozi Wa Mapinduz Zanzbar? Na Kama Ndiye Aliwezaje Kuondoka Zanzibar Wakati Wana Mapinduzi Wengi Walitafutwa Na Kuuawa?
 
JIFUNZE KISWAHILI EWE MGANDA..

majambo - mambo

kufanza - kufanya


NYERERE NI BABA WA TAIFA,HIVI TUNAJIANDAA KWA AJIRI YA KUMBUKUMBU YA SIKU YAKE YA KIFO 14/10..

Kaa Pemben Kdoooogo!
 
simple fact: huwezi shinda vita yoyote duniani kama unaenda vamia nchi ambayo viongozi wake wanapendwa na wanachi? kitendo cha majeshi ya tz kushangiliwa na wananchi wa uganda mitaani na kupokelewa kama heroes kinathibitisha kua kulikua kuna kitu kibaya amin anawafanyia raia wake... kwa mfano sasa huwezi kuja tanzania uvamie alafu mpite mitaani tuwashangilie hata kama JK ana mapungufu yake hatujafikia hatua ya kukubali majeshi ya nje yaje kutusaidia kumtoa!!!
 

kweli mkuu
 
Sio kweli, mbona saddam Hussein na gadafi wameshindwa vita , je walikuwa hawapendwi na raia ?
 
Kuandoka sio issue, kumbuka okelo alikuwa askari wa kukodi, kwa hiyo yy akimaliza kazi yaka anaondoka , kama vile bob dennard
 
Okello ndio baba wa taifa la wazanzibari wote wajitahidi kumkubali baba yao wa taifa ili laana isiwatafune
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…