Ndugu Wana Jamii Forum, Humu Ndani Tume Bahatika Kuwa Na Mdau Echolima, Alishiliki Vita Ya Uganda, Kama Unaswali Tunaweza Tukamuuliza, Kama Unajibu Bara~bara Zaidi Unaweza Ukamsaidia Pia Kujibu. Naanza___ 1) Eti, Nimesikia Kuwa Mambo Mengi Tunayo Yasikia Kumuhusu Amini Kama Kuzamisha Mto Kagera Vikongwe, Kula Nyama Za Watu, Kufanya Ngono Hovyo, Kuua Hovyo Na Mengi Mengineyo, Yalikuwa Ni Plopaganda Za Uongo Alizo Ziandaa Mwalimu? Maneno Haya Yana Ukweli?
Mkuu!
Yaani umenifanza nicheke pita kiasi! Kwi! Kwi! Kwi!
Watu wengi waliingiwa na zile
propagandas za ki-
Communist za yule
Nyerere na matokeo yake waliamini/wanaamini utumbo na uharo mwingi mno waliolishwa!
Ukiangalia kwa upande mwingine;Nyerere
alichochea saana na kusababisha mgogoro ulioleta ile vita dhidi ya
Uganda/Amin kwa miaka kadhaa, kabla ya Amin kuchoshwa na vile vitimbi ndipo akaamua kuchukua zile
"hatua za kijeshi"!
Tanzania "ilifuga",kuwafunza na kuwagharamia mno
magaidi wengi wa kutoka
Uganda,baada ya
Milton Obote kuondolewa madarakani na
Amin. Matokeo yake, hayo magaidi kwa masaada wa
Nyerere walikua haweshi kuleta chokochoko na
kuihujumu Serikali ya Uganda khasa tokea maeneno yaliokua mipakani na
Tanzania.
Yule
Obote nae aliporejeshwa madarakani mara ya pili kwa msaada na maguvu ya
Nyerere;inajulikana yakuwa ndo
aliuwa na
kubaka vikongwe,watoto,wanawake na kufanza
unyama/uharamia mwingi mno wa kulipiza kisasi kwa Wananchi wake wa makabila mengine na Wapinzani wake wa kisiasa kuliko hata huyo
Amin!
Kwa kifupi sina haja wala madhumuni ya "kumtetea"
Idd Amin,kama naye kuna yoyote mabaya alofanza na yaliwahi kuthibitishwa...lakini lazim wakti mwingine tujifunze kuangalia majambo kitaaluma na bila ya ushabiki au
propagandas za ma-
Dictators wengine!
Najua hii
thread yako wengi wataichungulia tu kwa mbali na kukimbia kuchangia/kutoa hoja...lakini usijali. Sisi wengine wachache
tunajaribu kukufahamu
mantik yako japo umeandika kwa maskhara kiduchu! Kwi! Kwi! Kw!
Huyo
Echolima unaemtaja;hakuonekana tena kuja kumalizia ile story/thread yake ya
"Vita ya Kagera"...nakumbuka mara ya mwisho alitupa
ahadi ya kusuburia kwa wiki mbili, lakini sasa yakurubia takriban mwezi wa pili!?
Imepatikana khabar yakuwa huyo
Echolima ati ameanzisha thread/mnakasha mwengine kuhusu
"vita ya Waarabu na Israel" humuhumu
Jf!? Kwi! Kwi! Kwi!
Ahsanta.