Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Siyo siri kwa sasa. Inaelekea Vita ya Ukraine haiungwi mkono na wamarekani. Na Trump aliahidi kuimaliza vita hii ndani ya siku moja kwa kukata misaada yote ya kivita kwa Ukraine.
Trump mara kwa mara amesikikia akisema huyu bwana mdogo Zelensky kila akija Waashington anabeba kitita chetu cha maTrilioni-na kuahidi kukomesha hilo.
- Breaking News: - Donald Trump ashinda Urais wa Marekani
Kwa mashariki ya kati, wananchi wengi wa marekani inaelekea hawapendezwi na mauaji yanayoendelea huko Israeli na majirani zake.
Kuwaondoa Democrats madarakani ni kama vote of no confidence.
Hata hivyo sisi makabwela wa dunia, hakuna cha matumaini kwa Trump, maana katika awamu yake ya kwanza alisha sema, sisi shithole countries hatunaa maana kabisa.