Huo ndio ukweli mkuu vita ya Ukraine na gaza imeigharimu Demokratic
Hisia siyo lazima iwe uhalisia.
Kwa Marekani imekuwa jambo la kawaida vyama kupokezana madaraka.
Republican, chini ya Trump, walivyoshindwa uchaguzi, kulikuwa na vita ya Ukraine au Gaza?
Tena huko Gaza, Trump ana msimamo mkali zaidi. Alikwishawahi kusema kuwa kwa kile walichofanyiwa Israel na Hamas mwakajana, yeye angekuwa Rais wa Israel angefanya zaidi ya alivyofanya Netanyahu, ila aliwalaumu Israel kwa kuonesha picha. Akasema Israel ilitakiwa kuwaangamiza Hamas bila ya kuonesha maangamizi wanayoyafanya.
Huko Ukraine alisema kuwa yeye akiwa Rais ataimailiza hiyo vita mara moja, alipoulizwa ni kwa namna gani, alisema hawezi kufafanua zaidi, ila atawapa Russia chaguo, wakikataa, msaada wa USA kwa Ukraine hautakuwa wa kugusagusa, bali utakuwa ni msaada kamili wa ushindi.
Sasa tusubiri tuone huo mpango wake ni upi. Ufahamu kuwa Trump, ni miongoni wa wale watu wenye misimamo mikali, akifanya uamuzi wake, hajaribishi bali ni full force.