Salamuni...
Tukielekea kwenye maandalizi ya Sikukuu za mwisho wa mwaka... ambazo wale wenzangu na mimi tunaolipa kodi kupitia manywaji zinatuhusu... hebu sogeeni hapa tuwekane sawa kidogo....
Maana tumechoka kila siku tunasoma Dsm Vs Nairobi, Clouds Vs EFM, Wanaume wa Dar Vs wa Mikoani, Vibamia Vs Matango, Sura Vs Chura... gadeimm
Kuna vita kali imeibuka kwenye tasnia yetu ya ulipaji kodi kupitia ulabu
Pilsner lager Ikichuana na Balimi
Serengeti Lite ikiumana vibaya na Castle Lite
Na kuna hii ligi yenye mvuto wa aina yake imeibuka kati ya K Vant na Konyagi
View attachment 933640
View attachment 933642
Kwa wale wa Pepsi Vs Mirinda wanaweza kupiga juu kwa juu
Mimi kama mimi naona kama hii Vita ya Serengeti Lite Vs Castle lite... huyu Castle lite ni kama anapumulia mashine....
Hii ya K Vant Vs Konyagi... hapa naona njemba nyingi za nyagi zinahamia K vant kuunga mkono juhudi za kupoteza memory...
Ah ngoja niuchune hapa maana huu ulabu sichelewi kuandika matusi ...