Vitabu tu au kuna vingine? ushauri plzzz


wala sio uongo,we kumbuka tulisoma lwa hali ngumu kiasi gani na sasa tupo wapi?babangu alikuwa na utaratibu wa ajabu kabisa lakini sasa naelewa kwanini alitufanyia vile.kila siku asubuhi yeye na mkewe wanaondoka na usafri kwenda mjini na mimi na dada zangu plus kakaz tulikuwa tunapanda mabasi,kila jumamosi tulikuwa tunaenda shambani,na kila jumapili ilikuwa ni day off kwa waliokuwa wanatusaidia kazi pale home.kila siku lazima kusoma usiku wote mezani mpka baba naposema huu ni muda wa kulala,tena tulikuwa hatuna umeme nakumbuka ilikuwa ni karabai,vitabu alivosomea aliyekutangulia darasa inakupasa uvitunze ili anayefuata avikute sasa ole wako kipotelee kwako!
 

shida pia 'huleta furaha ukifanikiwa kuitatua'
mtoto ambae anatumia magari ya wazazi unafikiri
atakuja kupata 'furaha akinunua lake?
sansana utawasikia 'ahhh ningepata vogue hapa ndo ingekuwa bomba'
yaani hawezi hata kuthamini 'kidogo cha kwake'
 

hiyo discipline imekusaidia mno
na pengine unatamani wanao wangeipata hiyo routines....
 

yani hawa watoto sijui tyunakosea wapi kulea jamani,manake mi sielewi to be frank!yani kijana naona ni haki kabisa tena anaidai kuwa ili aoe lazima anunuliwe gari,nyumba.atafutiwe kazi matokeo yake ndo mabinti wanakutana na mamaz boy humu,unafikiri kwa kijana aliyenunuliwa kila kitu na wazazi wake ndo ameoa huyo mzazi akija kuwaamulia wazae watoto wangapi kwenye ndoa yao mtamlaumu?
 
shida pia 'huleta furaha ukifanikiwa kuitatua'
mtoto ambae anatumia magari ya wazazi unafikiri
atakuja kupata 'furaha akinunua lake?
sansana utawasikia 'ahhh ningepata vogue hapa ndo ingekuwa bomba'
yaani hawezi hata kuthamini 'kidogo cha kwake'

Ni kweli kabisa mkuu inakuwa ngumu sana kujisimamia kiakili kwa mtoto anayezaliwa na kukuta mazingira mazuri ya kifamilia. Na hata ukiangalia wale wanaofumba macho na kuonyesha moyo wa kujitafutia vya kwao huwa na moyo wa kujali sana na huwa na mafanikio pia. Niliwahi kupanga nyumba moja hvi ambamo kijana alikuwa anademand hela ya nauli ya mzazi wake tu..yaan hata sie wapangaji tukimpa haiesabu anadai lazima apewe na mamaake na kweli asipopewa haendi shule hata kama nyie mmempa!!!
 

Mzazi wenu alikuwa anawajengea 'self discipline'
Unapozaliwa na kukuta kila kitu kipo kwenu unajenga katabia flani kakuona kuwa 'kila kitu ni haki yako'
Na mbaya zaidi unasahau kuwa hata wazazi wako walifight pia kufika hapo walipo!!!
 
pole, nakumbuka enzi zangu lol
iliwahi tokea ila kwa staili tofauti.

Niliduwaa kama nimebanwa mlango.

dah.....mi nakumbuka niliambiwa nitembee na kopo lenye mfuniko......nikimuona niingie humo.....kisa nimemkataa.....akanidai kanda yake ya Dr Dre nikawa nimepoteza.......wavulana bana......
 
Mpaka waje kufungua shule mbona kazi tunayo......lol!
Afu ukute wewe unachoma ada kumbe yeye anaendekeza hizi habari...

yaani acha tu kaka mkubwa haya mambo haya nilimwambia mwanagu siku nikisikia ana mdada nitamtahiri mara ya pili lkn baba yake akanizodoa unataka awe na mkaka ikabidi niwe mpole. jamani tuwamombee watoto wetu
 

dah!unanikumbusha enzi zile za mkoloni wetu acha kabisa yale yalikuwa maisha bana. mtoto nyumbani unajua huyu ni baba na huyu ni mama mtalima mboga na mashamba kama kubota akikupeleka shule anachagua shule yenye kazi eti kisa ukirud home uwe na akili ya kazi.

jamani nilisoma weruweru huko kazi mtido mmoja hadi kuosha ng'ombe ukirud home hakuna kupumzika tena kama kuonsha ng'ombe uje na skills ulizo pata shule ukienda kupanda mahindi uje na skills ulizopewa shule yaani hadi unahisi duia si yako tena. leo hii mpe mtoto bustani ya hatua 4 tu uone cha mtema kuni lol!
 

HARD TIMES MAKES A MAN snowhite.....never forget that
 
Last edited by a moderator:

watoto kuwapa kila wanachikitaka ni kuwa haribu
wape mahitaji tu....wajifunze tofauti ya 'haki yao' na 'privilege'
 

Kuna utaratibu walikua nao wachaga,yaani mtoto akifeli shule anafukuzwa nyumbani,huu utaratibu kumbe ulikua mzuri!!
 
Huu utoto jamani ni balaa..Kwa kipindi hiki kwake yeye anahisi yuko sawa tu na ndiyo maana anaomba ushauri jinsi gani atamface mama yake mlezi.
Daah!! Wazazi kazi tunayo. Yaan kama ni mwanangu sijui nikufanyaje tu.
Any way ni upepo tu utapita.
 
Kuna utaratibu walikua nao wachaga,yaani mtoto akifeli shule anafukuzwa nyumbani,huu utaratibu kumbe ulikua mzuri!!

na wengi waliofukuzwa hawakufeli maisha
 
Yaani nimeangua kicheko kwa subwoofer hadi nakohoa!
Duh!
dah.....mi nakumbuka niliambiwa nitembee na kopo lenye mfuniko......nikimuona niingie humo.....kisa nimemkataa.....akanidai kanda yake ya Dr Dre nikawa nimepoteza.......wavulana bana......
 
ha ha ha, mie walienda kukodi mabaunsa tena yule pawa mabula.

Nikawaambia, sasa mende mnamuua kwa bomu??

Uzuri tukafunga shule hadi kuja kufungua wakawa wamesahau.

Afu hadi leo tuko mabesti kinoma, huwa nawakumbusha wanacheeka.

dah.....mi nakumbuka niliambiwa nitembee na kopo lenye mfuniko......nikimuona niingie humo.....kisa nimemkataa.....akanidai kanda yake ya Dr Dre nikawa nimepoteza.......wavulana bana......
 
Dada yangu nikushauri kwa sasa zingatia masomo kwanza, soma kwa bidii, hayo mambo utayakuta tuu usiwe na haraka nayo.
Pili just be honest kwa mlezi wako kihusu killichotokea na mwombe samahani, na kuapa kuto kurudia tena, akishakusamehe usirudie tena...


 
watoto kuwapa kila wanachikitaka ni kuwa haribu
wape mahitaji tu....wajifunze tofauti ya 'haki yao' na 'privilege'

Well said. Remembering times nilikuwa naharibu madaftari kufungia mihogo. Kila kukicha siachi kuomba daftari mpya.
Mwishowe mzee akachoka nakuhitaji ni mletee daftari zangu zote lol. Daftari zikaja akahesabu karatasi za daftari zote hazifiki hata daftari moja.
Mzee akaenda dukani akaninunulia daftar moja akaja mbele ya macho yangu akachana karatasi mpaka zilizobaki kufikia jumla ya idadi ya karatsi zilizobaki kwa daftari yangu. He said hizi zitakutosha kwa masomo yako.
Hiyo wiki nilijifunza somo jamani, maana kila mwalimu alikuwa ananipakipondo cha hali ya juu kutokuwa na daftari ya somo husika.
Tangu hapo nilijifunza lol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…