Vitabu vitakatifu vimekataza kuabudu miungu. Je, kuanzisha uchifu siyo kupingana na maagizo ya Mungu? Wanasiasa mnamkufuru Mungu

Vitabu vitakatifu vimekataza kuabudu miungu. Je, kuanzisha uchifu siyo kupingana na maagizo ya Mungu? Wanasiasa mnamkufuru Mungu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii inatokana na ukweli kwamba wale wanaoitwa machifu siyo viongozi wa kimila Bali ni wazee wastaafu wenye kadi ya Chama cha Mapinduzi. It's like Jumuiya ya wazazi imeshindwa kuaminika nakufanya kazi sasa wametafuta wazee fulan fulan aidha wa vyombo vya usalama au wazee maarufu nakuwafanya machifu wakiamini 2025 matamko ya machifu yatapunguza nguvu ya uponzani.

Lakini jambo la pili uchifu unamiiko yake ambayo ni kinyume kabisa na miiko ya KIKRISTO na KIISLAM. Machifu wanaamini kwenye mizimu. Lakini fuatilia majina ya machifu wote wanaotajwa, wengi Wana majina ya kiislam au Ukristo Jambo linaloashiria kwamba Hawa siyo machifu maana wanakosa sifa kuu ya uchifu ambayo ni kuabudu Miungu. Chief kwa mfano akina Fundikira huko Tabora, wanao mfumo wao wa kusali, kutoa Sadaka na kuomba Toba. Vyote hivi havielekezwi Kwa Mungu vinaenda Kwa Miungu.

Nataka kusema hivi; Hawa chiefs wamegawanywa mostly Kwa Kanda. Na kama nilivyorleza hapo juu tunaowaita machifu siyo machifu Bali ni viongozi wa siasa wenye mrengo wa CCM waliopewa jukumu lakisiasa 2025 na Sasa wapo kwenye majaribio. Chiefs wengi hawana nguvu ya kiuchumi kuweza kusafiri kutoka Kanda zote kwenda Mwanza na Kilimanjaro, wamelipiwa na serikali na walilipiwa na serikali. Kwanini wanalipiwa ni kwa Sababu siyo wao wanaoandaa tamasha na hawana economic power yakuandaa tamasha Bali serikali inaandaa tamasha Kisha wanaalikwa na ndiyo maana unaona imetoka short notice na wamesafiri.

Lakini pia Kwa wale tuliowahi kufanya kazi kwenye mashirika tutakubaliana kwamba hii ni Mbinu ya viongozi wachache wasio na patriotism kutengeneza Mbinu za kupata pesa. Wapo watumishi wamekaa Kilimanjaro more than 14 days wanaandaa tamasha, wapo waliopewa tenda nk hii yote nikutafuta ada ya Januari watoto wakasome bila usumbufu na Januari isionekane Kama mwezi wa kabeji kwao.

Kwa kuwa tumeanza kuona umuhimu wa kuandaa utawala wa kikanda, ni vyema pia tukaamua Sasa kwamba sera ya Majimbo ni sera sahihi kwenye ugatuzi wa Madaraka. Tukiendelea kutumia fedha za Umma kwenye matamasha ya machifu tutaitia nchi hasara Kwa watu wachache kunufaika na haya machaka. Twende tukaestablish Majimbo tuteue masenetor wasimamie hizi zones tunazotaka kufufua nazo uchief.

Ukijiuliza tamasha limetumia kiasi gani na limeingiza kiasi gani utapata kichefuchefu, watu wamekatwa tozo zikaandae tamasha lisilo na tija. Na viongozi wa Dini Ili nijaribu la kiimani kwenu. Mnapohubiri tusiabudu MIUNGU MINGINE ILA MUNGU jitahidini mbapoona waumini wenu wameanza kuabudu Miungu MINGINE basi watengeni na Kanisa au misikiti kuepusha nyumba za ibada kuingiliwa na Miungu.

Tumewaona wanasiasa wanavyosherekea Miungu ya uchifu kwanini tusizame rohoni tukaomba ujasiri wa kuhubiri kuwakanya? Kama tunaamini wanachoabudu na kukitukuza kina usahihi basi Anzeni upya kutufundisha hiyo Miungu MINGINE ni ipi?
 
Umesahau, machifu wana wake 10 nakuendelea sijui pale nani mwenye wake 10 na zaidi, hii ni sawa kama ilivyokuwa hapo nyuma kuwa rais anaenda kuongea na wazee wa Dar isalaama baada ya vyama vingi kuingia wazee wakaanza kuchambuliwa wewe kama inaiunga chadema mkono haupewi mwaliko, mzee wa dar isalaama ni yule mwenye tshirt na kofia ya ccm.
 
Povu jingi sana nimeshindwa kulipitia hadi mwisho.
 
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii inatokana na ukweli kwamba wale wanaoitwa machifu siyo viongozi wa kimila Bali ...
Kitu kikubwa kwa Chifu ni kuwa na uwezo wa Kipesa na Nyumba au Ikulu ya chief, ambayo ina hakisi u chifu wake , sasa sijui hawa machifu wetu "ikulu" zao zipoje
 
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii
Mmesahau tozo ni pesa kwa uchafuzi 2025
Kwani sikuhizi umesikia tena mchanganuo wake?
Ukweli ndio kazi ya Mwigulu hiyo fungu analo
I
IFM/TOZO money hapo ndio bao lamkono waulizeni watufafanulie hizo pesa
Ccm mchwa
 
We ni mpumbavu kabisa nani alikwambia kuna vitabu vitakatifu vya Mungu?

Hivyo ni vitabu vya wazungu na waarabu waliowapata wajinga kama wewe na kuwaambia kuna Mungu na Miungu.jiongeze!!
Umeandika niliyotaka kuandika, na hii ndio maana halisi ya kuwa brainwashed.. Kila kitu chenye asili yetu tunakichukia na kuona hakina maana na mbaya zaidi wale waliowatesa na kuwaua wazee wetu ndio wametuelekeza namna ya kumjua MUNGU
 
We ni mpumbavu kabisa nani alikwambia kuna vitabu vitakatifu vya Mungu?

Hivyo ni vitabu vya wazungu na waarabu waliowapata wajinga kama wewe na kuwaambia kuna Mungu na Miungu.jiongeze!!
Ubongo wako unakudanganya sana! Bible imekuwepo duniani kabla ya hao Wazungu wako. Mlaumu sana mwalimu wako wa historia because seemingly alikuwa prejudiced & biased.

Umeandika niliyotaka kuandika, na hii ndio maana halisi ya kuwa brainwashed.. Kila kitu chenye asili yetu tunakichukia na kuona hakina maana na mbaya zaidi wale waliowatesa na kuwaua wazee wetu ndio wametuelekeza namna ya kumjua MUNGU
 
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii inatokana na ukweli kwamba wale wanaoitwa machifu siyo viongozi...
Sidhani kama machifu siku hizi wanachukuliwa kama miungu. Ila twachofahamu hawa machifu ni viongozi wetu kikabila. Kama huwapendi au huamini hiyo halali yako.

Ila sisi Wanyamwezi na Wasukuma machifu kwetu ni viongozi muhimu mno, ila sijasikia wakiabudiwa kama miungu. Poa tu wacha mama aule kama yote kwa sasa maana 2025 hakuna guarantee autaukwea urais…
 
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii inatokana na ukweli kwamba wale wanaoitwa machifu siyo viongozi wa kimila Bali ni wazee wastaafu wenye kadi ya Chama cha Mapinduzi. It's like Jumuiya ya wazazi imeshindwa kuaminika nakufanya kazi sasa wametafuta wazee flan flan aidha wa vyombo vya usalama au wazee maarufu nakuwafanya machifu wakiamini 2025 matamko ya machifu yatapunguza nguvu ya uponzani.

Lakini jambo la pili uchifu unamiiko yake ambayo ni kinyume kabisa na miiko ya KIKRISTO na KIISLAM. Machifu wanaamini kwenye mizimu. Lakini fuatilia majina ya machifu wote wanaotajwa, wengi Wana majina ya kiislam au Ukristo Jambo linaloashiria kwamba Hawa siyo machifu maana wanakosa sifa kuu ya uchifu ambayo ni kuabudu Miungu. Chief kwa mfano akina Fundikira huko Tabora, wanao mfumo wao wa kusali, kutoa Sadaka na kuomba Toba. Vyote hivi havielekezwi Kwa Mungu vinaenda Kwa Miungu.

Nataka kusema hivi; Hawa chiefs wamegawanywa mostly Kwa Kanda. Na kama nilivyorleza hapo juu tunaowaita machifu siyo machifu Bali ni viongozi wa siasa wenye mrengo wa CCM waliopewa jukumu lakisiasa 2025 na Sasa wapo kwenye majaribio. Chiefs wengi hawana nguvu ya kiuchumi kuweza kusafiri kutoka Kanda zote kwenda Mwanza na Kilimanjaro, wamelipiwa na serikali na walilipiwa na serikali. Kwanini wanalipiwa ni kwa Sababu siyo wao wanaoandaa tamasha na hawana economic power yakuandaa tamasha Bali serikali inaandaa tamasha Kisha wanaalikwa na ndiyo maana unaona imetoka short notice na wamesafiri.

Lakini pia Kwa wale tuliowahi kufanya kazi kwenye mashirika tutakubaliana kwamba hii ni Mbinu ya viongozi wachache wasio na patriotism kutengeneza Mbinu za kupata pesa. Wapo watumishi wamekaa Kilimanjaro more than 14 days wanaandaa tamasha, wapo waliopewa tenda nk hii yote nikutafuta ada ya Januari watoto wakasome bila usumbufu na Januari isionekane Kama mwezi wa kabeji kwao.

Kwa kuwa tumeanza kuona umuhimu wa kuandaa utawala wa kikanda, ni vyema pia tukaamua Sasa kwamba sera ya Majimbo ni sera sahihi kwenye ugatuzi wa Madaraka. Tukiendelea kutumia fedha za Umma kwenye matamasha ya machifu tutaitia nchi hasara Kwa watu wachache kunufaika na haya machaka. Twende tukaestablish Majimbo tuteue masenetor wasimamie hizi zones tunazotaka kufufua nazo uchief.

Ukijiuliza tamasha limetumia kiasi gani na limeingiza kiasi gani utapata kichefuchefu, watu wamekatwa tozo zikaandae tamasha lisilo na tija. Na viongozi wa Dini Ili nijaribu la kiimani kwenu. Mnapohubiri tusiabudu MIUNGU MINGINE ILA MUNGU jitahidini mbapoona waumini wenu wameanza kuabudu Miungu MINGINE basi watengeni na Kanisa au misikiti kuepusha nyumba za ibada kuingiliwa na Miungu.

Tumewaona wanasiasa wanavyosherekea Miungu ya uchifu kwanini tusizame rohoni tukaomba ujasiri wa kuhubiri kuwakanya? Kama tunaamini wanachoabudu na kukitukuza kina usahihi basi Anzeni upya kutufundisha hiyo Miungu MINGINE ni ipi?
Viongozi wengi wa ccm ni washirikina,ulimsikia makamu wa Rais alivyokuwa analalamika kuhusu mawaziri kulogana?

Anachofanya Hangai ni kuhalalisha uchawi na ushirikina serikalini,mambo ya ovyo sana haya
 
Nchi imekuwa ngumu kutawalika, tunawatafuta machifu Kwa lengo lakuwatumia Kwenye Siasa 2025. Hii inatokana na ukweli kwamba wale wanaoitwa machifu...
Umeambiwa selikali hauna dini ndio maaana haya yapo,kamari,riba,pombe,biashara ya ngono,kama selikari ingekuaa na dini haya yasingekuwepo,upo nyonyo?
 
Shitholes mlivyo wagumu katika mioyo yenu mnampinga hata aliyewadanganya mkoloni na kusema haya

Hiyo biblia iliyokuwepo kabla ya wakiloni ni ipi au unajitongozesha kwa wazungu?

Iliandikwa ktk lugha ipi na nani aliiandika?

Hao mitume wa Kiafrika walioandikwa humo ni kina nani?

Waafrika mmelaaniwa na nani nyie?

Ukweli ni kwamba wengi mnasali kwa uoga wa kutokuzikwa basi
Mbona una makasiriko mengi sana asubuhi hii? Nimeshakwambia historia yako imepinda; mlaumu teacher wako wa historia amekupoteza maboya. Never criticize something you aren't fully sure of; utaonekana mpuuzi na kituko tu.
 
Hakujawahi kuwepo mwanaccm anayeamini Mungu
This is fallacy of generalization. Mimi siyo Mwanachama wala mfuasi wa Chama chochote kile cha siasa ila naamini wapo wana-CCM ambao ni wacha Mungu wazuri tu. Mahaba na vyama vyenu vya siasa usiwatie upofu wapendwa.
 
Back
Top Bottom