Vitabu vya Kiswahili vinavyofundisha 'Creative writing'

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
3,539
Reaction score
3,551
Habari waungwana wa JF!

Naombeni msaada wa kupata vitabu/vitini vya kiswahili kwa ajili ya kujifunza 'creative writing'. Nahitaji kujifunza mimi mwenyewe ili niwe naandika vitu (kama hadithi fupi na ndefu, makala n.k) katika muda wangu wa ziada ambao huwa unapotea bure! Naomba hata kama una-'soft copy' (ambayo ndiyo ningependelea zaidi).

Chonde chonde jamani najua hapa kuna wanafunzi/wakufunzi wa UDSM, UDOM, OUT na hata chuo chochote ambao wanaweza wakanisaidia kwa hili, nimetafuta Internet na kupata vya Kiingereza lakini pia kwa vile napendele na vya kiswahili nikasema nije kwa wana bodi!
Thank you guys, hope my want is met!

CC. Kongosho, Mentor, CYBERTEQ, Mtambuzi, King'asti et all
 
Huo mtihani mkuu!
Hahahahaaaaa, kwanini mtihani kaka? Vipo, japo mtu unaweza kujifunza kupitia uzoefu wa kusoma vitabu mbalimbali hivyo kujua uandishi wa watu mbalimbali then at the end na wewe kutengeneza mchanyato wa design yake katika uandishi wako! Sasa, sema nahisi watu kwa haraka zaidi wanaweza kupata vya kiingereza tu!
 
yaani wewe hufai kabisaaaaa. unanifukuzia na unamtuma salamu babangu Mtambuzi! utapigwa panga la makalio wewe!

mie kiurahisi bwana ninge-google. ila nikiri tu nimeharibiwa na ukoloni, siwezi kuwaza sana kwa kiswahili. kila la kheri with your new hobby
Asante sana mkuu Mtambuzi! Msalimie sana Ngina na binti yako King'asti! Teh teh teh!
 
Last edited by a moderator:
Hakyanani sitaacha kukufukuzia mpaka nikupate!! Najua baba yako Mtambuzi ni wa mjini hata kama nikimtuma vijana wa siku hizi wanasema hamna 'shobo'!
Nimegugo (usishangae hapo nimetohoa kutoka kwenye neno 'google', teh teh!) nikapata makabrasha yaliyoandikwa kwa kiingereza! Kiingereza pia si shida kwangu ila tu nimefanya kiswahili kama chaguo la kwanza kwani maudhui itakuwa ya kiafrika/kitanzania zaidi kuliko kiingereza ambayo itakuwa na maudhui iliyojaa radha ya mawazo ya kimagharibi! Lakini hata hivyo nadhani kwa kiasi kikubwa itanisaidia!
Writing is my hobby tangu zamani ila sasa kwa miaka mingi niliizika na sasa inafukuta kweli ndani ya moyo wangu ili niifufue, thats why!!
 
Last edited by a moderator:
hakyamama!

sasa lets cut a deal, nitakufanyia proof reading bure kwa sababu napenda kusoma. ila tukubaliane uache kunifukuzia. siku nikikutolea macho (ndo lugha ya mjini ya kutamani nadhani), mie ndo nitakufukuzia.

nimechoka kufukuziwa, nisije nikaishiwa pumzi ukanikata ngwala bureee:llama::llama:
 
Thanks, point taken!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…