Nilikuwa napitia vitabu vya shule za msingi vya sasa na vile vya zamani ofsin ili kupata ni kitabu kipi kinafaa kufundishia kabla ya shirika kupeleka mawazo wizara ya elimu. tumegundua kuwa vitabu vilivyokuwa vya zamani kwa somo la kingereza vilikuwa bora zaidi kuliko vya sasa na vilimfanya mwanafunzi aweze kuelewa lugha vizuri, si kwa lugha hii hata kiswahili vivyo hivyo. kuanzia mpangilo wa uwandishi, visa (visa vya musa, neema, baraka) na mengineyo. hebu changia mada hii kweli vina ubora kiliko vya sasa? ukipick hata mfano mmoja, sababu kuna wadau wa elimu wanahitaji virudishwe vitabu vya zamani kwa shule za msingi, ila sehemu palipo na mapungufu virekebishwe.