Vitabu vya zamani na vya sasa mashuleni

Vitabu vya zamani na vya sasa mashuleni

fered

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2013
Posts
224
Reaction score
40
Nilikuwa napitia vitabu vya shule za msingi vya sasa na vile vya zamani ofsin ili kupata ni kitabu kipi kinafaa kufundishia kabla ya shirika kupeleka mawazo wizara ya elimu. tumegundua kuwa vitabu vilivyokuwa vya zamani kwa somo la kingereza vilikuwa bora zaidi kuliko vya sasa na vilimfanya mwanafunzi aweze kuelewa lugha vizuri, si kwa lugha hii hata kiswahili vivyo hivyo. kuanzia mpangilo wa uwandishi, visa (visa vya musa, neema, baraka) na mengineyo. hebu changia mada hii kweli vina ubora kiliko vya sasa? ukipick hata mfano mmoja, sababu kuna wadau wa elimu wanahitaji virudishwe vitabu vya zamani kwa shule za msingi, ila sehemu palipo na mapungufu virekebishwe.
 
Kwa ukweli vitabu hivyo vilikuwa bora kwani vililenga kwa urahisi kurahisisha uelewa wa wanafunzi kwa wakati ule.... Pamoja na hayo dunia imebadilika kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba kumeathiri hata utungaji wa vitabu vya kiada si ndani ya Tanzania tu, bali dunia nzima popote elimu itolewapo! Najua utakuwa unavisifu vitabu hivyo kwa kuwa ulipendezwa navyo kwa visa vilivyokuwamo ndani ya hadithi katika vitabu vile na akili yako kujenga dhana kwamba hivyo ndio vitabu bora! Je, kwa mfano rahisi, kuna kitabu chochote cha kiada ndani ya nchi ya Tanzania kwa kipindi kile labda kilikuwa na picha walau ya 'Computer'? Jibu kwa asilimia kubwa litakuwa hapana, hivyo tambua vitabu vya sasa vinatungwa kulingana na mabadiliko makubwa yaliyoletwa na ukuaji wa Teknolojia! Si hoja kwamba kweli vitabu vya zamani ni bora kuliko vya sasa tena kuzingatia utamu wa visa vya hadithi zake!
NAWASILISHA
 
ni kweli tunahitaji kuendana na mabadiliko ya ulimwengu kulingana na teknolojia inavyobadilika au inavyokuwa, cha msingi hapa nikuangalia uzito wa mambo yaliyomo ndani ya vitabu na si visa vilivyomo, leo hii pitia pitia baadhi ya vitabu uone vitu vilivyomo kweli vinafaa katika karne hii ya sayansi na teknolojia au la?.
 
Pia mabadiliko hayo hayo yanasababisha kukosekana ubora ule uliozoeleka, hivyo kufanya wanafunzi wa kipindi hiki na kipindi kijacho kutolingana kiuwezo kabisa na watu waliosoma nyakati zile, yaani wengi wao nyakati zile walikuwa na uelewa mkubwa, Lakini kadri miaka inavyosonga mbele uelewa unapungua utazidi pungua na kupelekea kufa kwa elimu kabisa kama mambo haya hayatatazamwa kwa umakini.
 
Back
Top Bottom