Vitabu vyangu bora vya nyakati zote. Vipi vyako?

Shoe Dog. Phils ni bonge ya Story teller. Kitabu kizuri sana.
Bonge moja la kitabu nimekusoma zaid ya mara5 .
Mwamba bill gates alikielezea as a true tale of sucess.
Ila phil has got a world class humility, kusoma chuo kama stanford then unauza viatu.
Hata baba yake alikuwa anamdiss sikukupeleka the best school ili uuze viatu.
Ila today's nike is worth $254 billion what a story to devour.
 
You have done a great job
Thanks for share with us a wide and useful knowldge My Next Thirty Years

One of My Fav' book is "The Mamba Mentality" By Kobe Byrant.
 
Uzi mzuri sana na umefafanua vizuri,hadi hapo vingine nimetamani kusoma. Nitasoma hicho Prisoners of geography, King Leopold ghost na how to rig an election.

Nimesoma Guns, Germs and steel. Moja ya vitabu bora sana kuwahi kusoma. Tuko na project moja ya kutafsiri vitabu kwa kiswahili. Tumetafsiri kitabu The Prince, ilikuwa kazi ngumu kutokana na kitabu chenyewe kilivyo, lakini tumekimaliza. Nafikiri mtoa mada umekiona jukwaa la Great thinkers. Ntaweka hapo tafsiri yote(lakini pia kitapatikana bure ndani ya maktaba app, labda kuanzia kesho) Hiki ni kitabu bora sana nafikiri watu wote, wanasiasa na raia wa kawaida wanapaswa kukisoma. Vingine tulivyotafsiri, ambavyo ni non fiction ni The art of war cha Sun Tzu na The richest man in Babylon.

Nafikiri mtu yeyote akisoma vitabu kunakuwa na tamaa ndani yake ya kupenda na wengine wasome kitabu hicho. Nilisoma The Alchemist. Ni kitabu kizuri sana, hata kama mtu hujaona sifa zake unaweza kukipenda. Hiki ni cha kusomwa na kila mtu. Na ni moja ya kitabu kilichotafsiriwa kwa lugha nyingi zaidi duniani. Kinaongoza kwa vile ambavyo waandishi wake bado wako hai. Kwa kutamani kila mtu akisome niliwasiliana na jamaa wanaosimamia hakimiliki za Coelho. Wakaniambia natakiwa kuongea na Publishing house, wao wananegotiate na publishing house.

Pia mkuu kama unasoftcopy ya hicho cha A knight in Africa naomba unisaidie. Ni kitabu kizuri ila nashindwa kukipata tena online.

Nimesoma vitabu vingi na nitakuja na list ya vile bora ambavyo ningependa wengine wasome. Lakini hivi karibuni nimesoma kitabu Gamba la Nyoka cha Euphrase Kezilahabi, 1979. Hiki kinaelezea jinsi oparesheni za kuanzisha vijiji vya ujamaa zilivyoendeshwa na madhara yake katika jamii. Pia kinachambua kwa kina siasa ya ujamaa, na jinsi tulivyoifuata kikasuku. Kezilahabi alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo.
 
Jambo moja kuhusu jamaa, naona alikuwa mtu aliyerelax sana. Yaani anahustle na harakati za kuwapiga Fix wajapan wamuuzie viatu, huku akiendelea kuishi kama kutembelea maeneo mbalimbali. Yaani ni mtu wa Kazi na Bata.
 
Anza na hicho cha Prisoners of Geography.
 
Ajabu, sijawahi soma vitabu vya Kezilahabi. Kuna kimoji kinaitwa Kaptula La Marx kuna jamaa alikifanyia review yake, kilinivutia sana. Itabidi nivisome. Na nadhani softcopy zake ninazo.
 
Nimekiona hicho Cha Prince. Na ninausoma huo uzi. Mmejitahidi. Kutafsiri ni kazi ngumu sana. Mimi napenda sana kuandika, so huwa wakati mwingine, out of fun tu, natafsiri vitabu navyosoma, hata kama sio chote. Kuna kitabu nimekitafsiri sehemu ndogo, cha historia ya Muziki wa Kongo, ipo kwenye Jukwaa la Entertainment.
 
Cha Chande hiki hapa. Version zote mbili, za Kiswahili na Kiingereza. View attachment A_KNIGHT_IN_AFRICA_by_SIR_JKC.pdfView attachment SHUJAA_KATIKA_AFRIKA_by_JKC.pdf
 
Looo hiki ninacho na nimeona kikipendekezwa kweli kweli, nitakipitia now naendelea na rich dad, poor dad baada ya kumaliza the richest man in Babylon through ni kitamu sana mpk nina mpango wa kukirudia.
Hadithi ya Arkadi ina mafunzo sana. Na kwa kweli mafunzo yake yanauhalisia sana hasa juu ya nidhamu ya fedha.
 
Nitumie namba nikutumie hicho kitabu unachotaka hapo juu alafu mimi nimetafsiri vitabu vingi sina

Vipo kwenye mfumo wa hard copy na soft copy
 
Naam na mimi ngoja nifanye kushare top favorite books.
1.Twilight saga
Hii ni riwaya ya kusisimua iliyoandikwa na Stephanie meyer inayomhusisha mrembo mmoja anaitwa Isabella swan baada ya kutoka kutemtembelea mama yake california anarud washington kwa baba yake ambaye washatengana na mama yake .lakini katika hali ya kutatanisha akiwa shuleni anajikuta anampenda mkaka mmoja hivi anaitwa Edward ambaye ni vampire kutoka familia ya cullens hapo ndipo utamu unaanzia..by the way Hii riwaya ina movie yake.


2.LONDONISTAN
Chake mwana mama melanie phillips
Ambacho kinaelezea ni jinsi gani mitaa ya London ilikuwa chimbo la magaidi haswa waliolipua wtc huko manhattan USA mwaka 2001 na pia waliolipua treni ya chini ya ardhi huko london mwaka 2005.

3.MIND WARS.
hichi ni kitabu ambacho kwa kiasi kikubwa kinaelezea ni jinsi gani mtu anaweza kushikiliwa akili yake ( mind control)pasipo ridhaa yake kwa njia mbalimbali kuanzia mafunzo ya kidini,media,ugaidi ,hadi kupigwa shoti za ubongo ( electroshock )
Ili kufanya alteration ya personality ya mtu either positively or negatively.
Kitabu hiki kime inspire kwa kiasi kikubwa utengenezwaji wa filamu zifuatazo
Kama; the manchurian candidate ya 2004 ,jason bourne film series n.k.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…