Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Joachim Wangabo amesogeza mbele kwa muda usiojulikana ziara yake katika Wilaya ya KALAMBO baada ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Wajasiriamali kususua.
Ziara hiyo ilikuwa ianze tarehe 14-17/01/2019. Hadi Jumapili tarehe 13/01/2019 ni vitambulisho 150 tu vilivyokuwa vimegawiwa kwa Wajasiriamali kati ya vitambulisho 6200 vilivyotegwa kwa wilaya hiyo.