Vitasa live

The real Daniel

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2017
Posts
2,117
Reaction score
7,899
Aisee leo vimenoga kweli kweli maana mpaka Sasa mapambano ma tatu na yote watanzania tumepoteza 'kihalali kabisa'. Mabondia wa tz Leo Hawako vizuri kabisa
 
Wapenzi wa JongoJongo tukutane hapa.
Nilivyomwangalia tu yule mpinzani wake nikasema leo tuna Knock down, no ni Knock up, hizi lugha za boti hizi labda Knock away.
Na ikawa asubuhi Na ikawa jioni. Ukweli ukadhihirika
 
Jongo Jongo kapiga mmarekani mapema asubuhi ya pambano.

Ila kuna jamaa kazingua sana. Kapigwa kizembe. Hata familia yaje itakuwa inamcheka huko.
Nilipomuona tu nikajua lazima apigwe, kwanza ana mwili wa ofisini😀😀
 
Maandalizi yamekua mazuri,
Ukumbi umependeza, na una viwango..
Imebaki sisi wananchi kutoa support kwa kuhudhuria
Viti empty vingi
Asante Sana Kwa ku note hii

Nimewasha gari kutoka tabata mpaka Next door Arena.

maaamaamaaeee nafika nataka kuingia nauliza kiingilio shs ngapi. Naaambiwa kuna laki moja, laki moja na nusu nadhani na laki mbili.
Nikalala mbelee mamaaamae.
These morons are not serious aisee. Mimi nimhudhuriaji mzuri Sana WA ngumi. Mashabiki wengi ni wahuni wale wa manzese na kwingineko. In short wa Hali ya chini na ndio wanajua boxing kinoma.
Sasa Leo hii unaweka kiingilio laki cha chini kabisa what do you expect? Viti empty
 
Uko sa Sana Kwa ku note hii

Uko sahihi.
Nadhani ni kwa sababu mapambano ya leo baadhi yanahusisha wapiganaji wenye majina yao huko mbele kama hawa kina Pulev na yule Mmarekani.

Na ni mapambano ya ubingwa hivyo kwa vyovyote vile yana dau kubwa.

Na pia yawezekana ni njia ya kupunguza waswahili na watu wasio wastaarabu kuhudhuria hii mipambano yenye hadhi ya kimataifa wasije wakaharibu hadhi na status ya mpambano wenyewe.

Lakini kwa kweli ukumbi umeandaliwa vizuri sana, kama mbele tu.
 
Jongo Jongo kapiga mmarekani mapema asubuhi ya pambano.

Ila kuna jamaa kazingua sana. Kapigwa kizembe. Hata familia yaje itakuwa inamcheka huko.
Nilipomuona tu nikajua lazima apigwe, kwanza ana mwili wa ofisini[emoji3][emoji3]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
MNamibia ku-surrender kwa Pulev.
Jamaa wa Bulgaria ana pumzi hatari.
Jamaa aliogopa kupigwa ngumi zaidi maana pulev alikuwa anataka knockout na mnamibia alikuwa kasha iva kweli kweli.
Uamuzi aliofanya ni busara zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…