Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Mnakaa pamoja na kuelewana ni jinsi gani wata finance biashara yako na kisha mtagwana faida ya biashara kwa kila mwezi kwa kipindi maalumu. Percentage za kugawana mtakubaliana pia ukipata hasara katika mwezi husika hamtagawana kwakuwa hakuna faida itakuwa imepatikana. Kwa lugha nyingine buashara inakuwa ni partneship kwa kipindi maalum kisha biashara itakuwa yako peke yako.

Kimsingi wao wataangalia kama biashara yako inafaida, kama haina faida hawatakuwezesha kwasababu hata wewe huwezi ingia ubia kwenye biashara isiyo na faida.
 
Mkuu kwa tafsiri yangu ya bila riba ni kwamba ukinunuliwa mali zenye thamani ya 15m kwa ajili ya biashara.Urudishe 15m na sio zaidi.
Sio kweli, ukinunuliwa bidhaa, biashara inakuwa ni ya ubia (partneship) kwa muda maalumu ambao mtakuwa mnagawana faida hadi hapo aliekukopesha atakapo recover mtaji aliowekeza kwenye biashara na kupata faida fulani ndio anakuachia biashara inakuwa yako peke yako. Ni biashara ya kugawana faida, usipopata faida hakuna cha kugawana. Ila kumbuka mbia wa biashara ana haki ya kukagua hesabu zote za biashara kwa maana ni yenu wote hadi hapo ubia utakapoisha.
 
Mkuu, kwa uelewa wako hivi kwenye bank za riba ukipata hasara hudaiwi marejesho?? Ukijibu hilo nadhanj utaanza kuelewa tofauti ya riba na faida
 
kwenye suala la mikopo ya ujenzi pana utata...Kuna mtu anasema kwamba aliwapelekea invoice ya m 10 kwa hiyo wakamnunulia vifaa kwa mkopo wa milioni 18. Hapa kidogo kuna utata ukisema hii ni faida. Nilitegemea ingeitwa faida kama ungesema tu nini unataka kisha wao wanakuletea na kukupa invoice ya milioni 18. Lakini kama invoice naleta mimi haiwezi kuwa faida tena inakuwa riba...Hebu fafanunua kwenye hili.
 
Basi sawa mkuu.
 
Nimeipenda Sana.
 

Wacha porojo, benki za riba huachiwi, kama uliweka dhamana nyumba ndiyo imekwenda hiyo.
 

Ninavyofahamu mimi na nilivyosoma kuhusu (mortgage) za bila riba, ni kuwa aidha kuna nyumba unaitaka kununua na hauna pesa za kutosha za mara moja basi financers wanainunua na kukukodisha (Ijara). Au kama unataka kujenga nyumba mpya basi unajengewa nyumba uitakayo na wenye kutoa mkopo lakini hiyo nyumba inakuwa ni ya wanaotoa mkopo na wewe wanakukodisha kwa kipindi mlichoelewana, na hiyo kodi kila inavyolipwa ndiyo unalipia na ununuzi wa hiyo nyumba (hire purchase).

Naomba upitie hapa: Ijara Canada - ijaraCDC

Suala la kununuliwa vifaa vya kujengea kwa hapa kwetu nadhani pia linawezekana na ni namna mtakavyojipanga watoaji mkopo, kwani hapo mnaweza kuwa ni retailers wa vifaa vya ujenzi ambavyo mnawauzia wakopaji wenu na wao wanalipa kama wamenunua duka la retail (hii ni kwa banks).

Njia nzuri nionavyo na yenye usalama kwa wote ni kuwa kama sisi tunaotaka kuanzisha kikundi cha wawekezaji ambae kila mkopaji atakuwa ni mwanachama wa hicho kikundi na moja ya miradi ni vifaa vya ujenzi kwa reja reja ambapo faida zitakuwa mara mmbili, faida ya kuuza vifaa vya ujenzi itarudi kwenye kikundi na faida ya wana kikundi kuweza kukopa bila riba.

Ni mjadala unaendelea na hayo ya mwisho ni mawazo tu yangu sio final say.
 
Napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa wote waliochangia mada hii hapa na wale wote wengine walioona wawasiliane nasi kwa kutupigia simu na wengine kwa whatsapp.

Uamuzi tuliofikia ni kuwa tunaanzisha haraka iwezekanavyo, saccos ambayo itasajiliwa kisheria na kanununi zote za nchi kuhusu vyama vya ushirika kuzingatiwa. Saccos yetu itakuwa ni wazi kwa wote watakao kujiunga pia tutahamasisha zaidi Watanzania wa diaspora kujiunga na saacos hii mpya.

Saccos itaendeshwa kwa kuwekeza kwenye vitu vinavyokubalika kihalali na pia saccos haitatoza riba kwa wanachama wake pindi watakapohitaji mikopo.

Kutakuwa na kamati ya awali ya uaunzilishi wa saccos, kikao cha kwanza kitafanyika tarehe 1 May 2017 hapa kwetu Kibaha, Misugusugu, mtaa wa vitendo.

Wale wote waliojiunga na group yetu ya Vitendo Action Group wamekaribishwa rasmi.

Siku ya mkutano huo wa awali kutakuwa na agenda zifatazo:

Introduction
- Kujulishana na kujuana wote, nani ni nani.
- kutambulisha miradi iliyopo na inavyoendelea.
- kutambulisha sabuni mpya zilizotengenezwa kwa udongo wa Aunt Zainab's Natural Super Clay.
- maswali na majibu.

Saccos
- Kuongolea saccos mpya itayoanzishwa na kutengeneza njia (road map) ya kuianzisha.
- maswali na majibu.

Uwekezaji
- kuelezea uwekezaji mpya unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
- maswali na majibi.

Lunch
- Chakula cha mchana kimeandaliwa, tutakula saa saba kamili.

Tunaomba wote wanaohusika wafike mapema, maongezi yetu ya maendeleo yaanze saa nne kamili.

Asanteni.

Abdul
 

Mkuu tupo pamoja ...nafuatilia projects zako...na hili pia usinisahau ingawa sina uzoefu lakini niko interested.....nitakucheki kwa whatsapp
 
Yale yale vipi, tufafanulie ndugu yangu, tupo katika kuelimishana kwa sababu tunataka hivi karibuni sana kuanzisha mradi tupate kufaidika na mfumo huu wa "Islamic Finance".
Hapo mnapogawana faida ndio riba ileile. Na hawawezi kukuacha bila kumazana na wewe ktk faida. Tumsifu Yesu Kristo
 
Naomba kujua kuhusu Islamic bank hasa NBC BANK,nikiwa na account ya islamic na nikitaka kuweka fixed account ili nipate faida jee inawezekana?utaratibu wao upoje?
 
Naomba kujua kuhusu Islamic bank hasa NBC BANK,nikiwa na account ya islamic na nikitaka kuweka fixed account ili nipate faida jee inawezekana?utaratibu wao upoje?


Binafsi sina ufahamu wa NBC shughuli zao za "islamic Banking" zinafanywa vipi, lakini ukipenda kujua kuhusu Islamic microfinance tafadhali pitia hapa: Islamic microfinance: How is it different? itafanana sana na ambayo tupo njiani kuianzisha hivi karibuni.
 
Mkuu sina uhakika na hilo, ila bado kuna tofauti kati ya riba na faida, hapo hiyo 18 ni fixed hata ukizidisha muda uliotakiwa kumaliza , lkn riba huwa haipo fixed, ikichelewa kurejeshwa ndani ya muda inaendelea kudaiwa kwenye kiasi kilichobaki na wengine wanachaji kwenye principal, that means deni linaongezeka na muda.
 
kuna mdau mmoja amessuggest approach moja nimeipenda zaidi hasa hiyo ya wao kujenga na kukuuzia au kununua kisha wakakuuzia hiyo ndo ina make sense zaidi kwenye upande wa faida.
 
kuna mdau mmoja amessuggest approach moja nimeipenda zaidi hasa hiyo ya wao kujenga na kukuuzia au kununua kisha wakakuuzia hiyo ndo ina make sense zaidi kwenye upande wa faida.


Hiyo ni aina moja na aina nyingine ni kuingia ubia wa bishara husika inayochukuliwa mkopo. Faida inayopatikana mnagawana kwa asilimia husika za kama ubia mwengine wowote mpaka deni litakapokwisha. Asilimia ya deni hupungua kila unapolipa kutokana na faida na asilimia ya faida ya wakopeshaji pia hupungua.

Mwisho wote mnakuwa winners, wote mmepata faida na wote hamjatoa wala kupokea riba.

Tatizo kubwa la kuuelewa mfumo huu ni pale suala la "kukopa" linavyotafsiriwa, kukopesha kwa riba, mkopaji anakabidhiwa pesa akafanyie shughuli aliyoainisha katika kukopa kwake, kama ni kweli au uongo inabaki siri yake na mara nyingine ya wale walioidhinisha akopeshwe, hakuna siri kuwa wengi hupewa mikopo kwenye ma benki ya riba kwa kuwa afisa wa mikopo nae atafaidika kwa kuhongwa kutokana na kopo huo.

Pia ukopeshaji wa riba, uwe wa benki au biashara za watoaji mikopo hujikita zaidi katika kutoa mikopo ili riba ndiyo ilete faida. Hiyo riba ndio biashara yenyewe ya kuingizia faida.

Tofauti na benki au taasisi zisizotoa riba ni kuwa, faida ya tasisi hizi hupatikana katika kuwekeza na si katika riba, ukienda kukopa kibiashara basi wakopeshaji huitathmini biashara yako na kuingia ubia na wewe ili mgawane faida katika hiyo biashara, kwa mfumo huu mtagawana pia na hasara ikitokea bahati mbaya.
 
Napenda kuwajulisha kuwa wale wote waliotaka kujiunga kwenye group letu la whatsapp, tutaanza kuwaunganisha baada ya tarehe 1 May 2017.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…