Tofautisha riba na faida kwanza ndo utapata pakuanziaMimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.
Na kwa jambo hilo napenda kunasihi nafsi yangu na nyote humu hasa hasa mwanzilishi wa thread hii Zainab Tamim jambo hilo lina uharamu kwa yule aliyemkusudia Allah katika mambo yake. Ama yule ambae hajali kachuma wapi mali yake wala anaitoa wap, haya maneno hayawezi kumnufaisha. Na Allah anasema 'kumbusha kwa hakika ukumbusho unawanufaisha waumin' na katika dini yetu Alhamdulilah kila kitu kipo wazi kwa yule mwenye kujifunza kwa ajili ya Allah na kutaraji radhi zake akatak kujua bas atajulishwa. Rejea Surat Baqara 275-283 Napenda nasaha ziwe fupi, aliyewafikishwa hata manen matatu anaelewa na ambae hakuwafikishwa hata umjie na kitabu hawezi kuelewa.
Inawezekana mtu akasema ni faida..
Jibu: maana ya riba ni faida sema ni ya haram, na katika sheria Allah amejalia wenye uwezo kuwasaidia ambao hawana uwezo mpe k1 arudishe k1 aliyoichukua kwako, ama ukimzidishia unakua umempa uzito na umemwingiza katika haramu. Na ukidai mnashirikiana katik biashara bas kuna faida na hasara zote uzikubal wala asididimizwe mmoja...
Zainab Tamim nadhan ujaelewa hzo aya nimeandika surat Baqara nayo ndio sura ya 2 katika Qur'an aya kuanzia 275 mpaka 283, hivyo ndivyo nilivyoandika.
Huenda sikuelewa vizur nielezee kwa mfano mi nataka kukopeshwa m1. Mnanikopeshaje nyinyi? Na malipo?
Assalaam alaykum. Wakuu hakika katika jambo hili la 'Islamic banking' kuna kuwahadaa waislamu na wote wasiopenda riba, coz ndani ya mkopo huo kuna riba ila ijawekwa waz kama wale wengine wanavyofanya, unakuta unataka mfano m5 kufungulia duka ukienda kwao watakusikiza alaf watakwambia wanakununulia hvyo vitu(bidhaa) alaf unaambiwa marejesho yatakuwa jumla m5 na k1 kwa muda mtakao ongea. Sasa hii ni riba tena ya haramu kama ile, sema hii imewekewa hila mtu asipoangalia vizur anasema hakuna riba, na hata konyagi ikiwekwa katika thermos haiwi halali wala ile thermos haihalalish ile konyag. Kwaiyo ni wajibu kwetu kuwa makin hasahasa waislam coz mtego huu umekusudiwa sis, na pia usitarajie baraka kutoka kwa Allah katika mtaj huo wenye riba, vip akubariki wakati umemuasi? Na kukopeshana katika sheria kupo na makusudio yake ni kusaidiana wala si KUDIDIMIZANA. Huwezi kuta benki inakubali hasara, hivi niwaulize, biashara zote zinazoanzishwa hazipati hasara? Jibu mnalo. Bas ni mshirika gan huyu hatak hasara!?ye faida tu
Wadau wote,
Napenda kuwafahamisha kuwa jana tarehe 1-5-2017 tulikuwa na kikao kuhusu kuanzishwa kwa SACCOS yetu mpya.
Wahudhuriaji wa walikuwa wa kutosha. Kati yao walikuwepo (wengi wao) ambao ni wawekezaji tayari katika miradi yetu ya awali (nje ya SACCOS tarajiwa), wengine ni wawekezaji watarajiwa. Pia tulimualika Mwenyekiti wa serikali yetu ya mtaa wa Vitendo, ndugu Salehe Dibebile, tulimualika pia na Katibu wa vyama vya ushirika vya kata ya Misugusugu bwana Kussi. Pia tulikuwa na wawekezaji wawili ambao tayari wana miradi yao (nje na yetu) ya machimbo ya michanga.
Kwa kifupi, tulitambulishana, tukajadili ushirika tunaoufikiria na tukakubaliana (bila kuwa na hoja za kupingana). Hoja zilizotamalaki zilikuwa ni za kupeana elimu zaidi ya ushirika na faida zake...
Ikaamuliwa tuuanzishe ushirika haraka iwezekanavyo...
Ikaamuliwa tuanze kwa kukusanya masharti ya saccos tofauti na samples zake, members wote wapitie ili tuweze kuwa na SACCOS yetu tarajiwa haraka iwezekanavyo...
Imeamuliwa pia Abdu Ghafur awe Mwenyekiti wa muda mpaka ushirika wetu utakapo sajiliwa ndiyo kutakapokuwa na masharti ya uchaguzi rasmi. Watakaojiunga wote watakuwa wajumbe mpaka hapo sheria na kanuni rasmi rzitakapo patikana.
Pia Imeamuliwa kuanzia sasa kila atakaependa kujiunga kutakuwa na ada ya kiingilo itakayo saidia katika gharama za usajili na mpaka hapo tutapokuwa na masharti na kanuni zetu rasmi zilizopitishwa na wnahama wote kwa ujibu wa sheria...
Ushirika tutakaoanzisha utafata sheria na kanuni zote za nchi na sheria za vyama vya ushirika za Tanzania...
Ushirika hautakuwa na ukomo wa watakaojiunga mpka hapo itakapotangazwa rasmi baada ya kupata kanuni zilizokubalika na wanahama wote, kujiunga kutakuwa wazi kwa yeyote anaekubalika kisheria, awe popote Tanzania au duniani...
Ada ya kiingilo kwa sasa ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed.
Mahesabu yote ya chama yatakuwa wazi kwa wanachama wote, kwa sasa yatapatikana kupitia group la whatsapp la waliojiunga.
Kila atakaelipa ataingizwa kwenye group mahususi la whatsapp litalokuwa kwa ajili ya wanachama tu waliojiunga katika ushirika wetu mpya.
Tumeanza kupokea ada za viingilio na hesabu zote zitapatikana kwenye group mpya ya wanachama walioingia kwa kulipia ada...
Uwe popote ulimwenguni unakaribishwa kujiunga kwa faida ya wote.
Group mpya imeshafunguliwa kwa jina la muda Vitendo SACCOS na members wawili waliolipia ada tayari tumepatikana, maelezo zaidi kwenye group mpya...
Ada ya kiingilo ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed
Nawajulisha wote watakaotaka kujiunga muanze kwa kulipia ada ili tufanikishe usajili kwa haraka.
Ili kujiunga, (kwa sasa) inatakiwa utupatie jina kamili, namba za simu, email address na ulipo na utume 10,000 kwa Mpesa.
Tunakaribisha maswali.
Abdul
+255 625 249 605 (whatsapp)
Wish I was with you guys.
Nililiona pilau kwenye picha kwenye group. Count me in Zainab, nitilie pesa za membership, sina access ya account ya Mpesa wala Tigo for now.
Will talk to you on the phone.
Keep it up.
Nakuja
marejesho itakuwaje kwa mtu usiemjua au aliyeko mbali
Wadau wote,
Mtanisamehe sana kuwa whatsapp yangu leo ina matatizo, nilikuwa ninai update simu yangu baadhi ya apps zimeanza kugoma. Bado naendelea kui uninstall ili ni install upya, nitakuwa tena hewani kwa whatsapp mara nitakapofanikisha.
Asanteni sana kwa mwitikio mkubwa usio na mfano.
hakuna riba kabisa una maana hio mkuu?Sio yale yale, ktk mfumo wa kiislamu mnaelewana wakt mifumo mingine unakuta mashart tayar. Pia mifumo mingne shart kubwa ni riba wakt huku hakuna riba.