Wadau wote,
Napenda kuwafahamisha kuwa jana tarehe 1-5-2017 tulikuwa na kikao kuhusu kuanzishwa kwa SACCOS yetu mpya.
Wahudhuriaji wa walikuwa wa kutosha. Kati yao walikuwepo (wengi wao) ambao ni wawekezaji tayari katika miradi yetu ya awali (nje ya SACCOS tarajiwa), wengine ni wawekezaji watarajiwa. Pia tulimualika Mwenyekiti wa serikali yetu ya mtaa wa Vitendo, ndugu Salehe Dibebile, tulimualika pia na Katibu wa vyama vya ushirika vya kata ya Misugusugu bwana Kussi. Pia tulikuwa na wawekezaji wawili ambao tayari wana miradi yao (nje na yetu) ya machimbo ya michanga.
Kwa kifupi, tulitambulishana, tukajadili ushirika tunaoufikiria na tukakubaliana (bila kuwa na hoja za kupingana). Hoja zilizotamalaki zilikuwa ni za kupeana elimu zaidi ya ushirika na faida zake...
Ikaamuliwa tuuanzishe ushirika haraka iwezekanavyo...
Ikaamuliwa tuanze kwa kukusanya masharti ya saccos tofauti na samples zake, members wote wapitie ili tuweze kuwa na SACCOS yetu tarajiwa haraka iwezekanavyo...
Imeamuliwa pia Abdu Ghafur awe Mwenyekiti wa muda mpaka ushirika wetu utakapo sajiliwa ndiyo kutakapokuwa na masharti ya uchaguzi rasmi. Watakaojiunga wote watakuwa wajumbe mpaka hapo sheria na kanuni rasmi rzitakapo patikana.
Pia Imeamuliwa kuanzia sasa kila atakaependa kujiunga kutakuwa na ada ya kiingilo itakayo saidia katika gharama za usajili na mpaka hapo tutapokuwa na masharti na kanuni zetu rasmi zilizopitishwa na wnahama wote kwa ujibu wa sheria...
Ushirika tutakaoanzisha utafata sheria na kanuni zote za nchi na sheria za vyama vya ushirika za Tanzania...
Ushirika hautakuwa na ukomo wa watakaojiunga mpka hapo itakapotangazwa rasmi baada ya kupata kanuni zilizokubalika na wanahama wote, kujiunga kutakuwa wazi kwa yeyote anaekubalika kisheria, awe popote Tanzania au duniani...
Ada ya kiingilo kwa sasa ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed.
Mahesabu yote ya chama yatakuwa wazi kwa wanachama wote, kwa sasa yatapatikana kupitia group la whatsapp la waliojiunga.
Kila atakaelipa ataingizwa kwenye group mahususi la whatsapp litalokuwa kwa ajili ya wanachama tu waliojiunga katika ushirika wetu mpya.
Tumeanza kupokea ada za viingilio na hesabu zote zitapatikana kwenye group mpya ya wanachama walioingia kwa kulipia ada...
Uwe popote ulimwenguni unakaribishwa kujiunga kwa faida ya wote.
Group mpya imeshafunguliwa kwa jina la muda Vitendo SACCOS na members wawili waliolipia ada tayari tumepatikana, maelezo zaidi kwenye group mpya...
Ada ya kiingilo ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed
Nawajulisha wote watakaotaka kujiunga muanze kwa kulipia ada ili tufanikishe usajili kwa haraka.
Ili kujiunga, (kwa sasa) inatakiwa utupatie jina kamili, namba za simu, email address na ulipo na utume 10,000 kwa Mpesa.
Tunakaribisha maswali.
Abdul
+255 625 249 605 (whatsapp)