Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

shukrani....
 
niliahidi jana kujiunga but nilighafilika..sasa ivi nishajiunga.rasmi.wakuu nafasi adimu hii ..hasa wale wasiopenda kutoa riba au kula riba..nafasi yao ndio hii asante
 
18 ni ndogo? Basi bora nikomae na vicoba yangu asilimia 5 tu


Islamic bank haina riba.

Islamic bank au Islamic financing yoyote hutegemea kwenye kuwekeza kibiashara kupata faida na si kutza watu riba.

SACCOS yetu mpya ambayo inaendeshwa kwa misingi ya "islamic financing" haina riba kabisa.
 
Waarabu wanaiita غرر yaani hadaa.
We utakua salafy tu..
ALLAAH Akuongoze akhy..
 
Wadau wote,

Tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tumeshasajili wana saccos zaidi ya 40 na tunaendelea kusaiili wana saccos wapya kila kukicha, kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania na duniani kwa ujumla. Diaspora wengi wameanza kuitikia mwito wetu.

Pia tunapenda kuwafahamisha kuwa yeyote ataeungana nasi kwa sasa, tutamuingiza katika group letu jipya la "Biashara Vitendo SACCOS" (licha ya lile la "Vitendo SACCOS") ambalo unaungwa automatically unapojiunga tu na SACCOS yetu mpya.

Humo utaweza kutangaza biashara zako binafsi nasi pia tutasaidia kuzitangaza tena kwenye mitandao ya kijamii na baadae tutaziweka kwenye website yetu itakapokuwa tayari.

Karibuni sana wadau.
 

Unanifurahisha sana katika huu uzi, unajuwa huu uzi nilikuwa sijaupitia wote, leo nimepata nafasi ya kuupitia na nnaona jinsi ulivyo very positive.
 
Kwanza kabisa natoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Bi Zainab Tamim na mumeo, shoga'ngu, Bwana Abdul.

Nawapongeza sana jinsi mlivyoanzisha uzi huu uliokuwa wa kubadilishana mawazo tu na kwa muda mchache mawazo mmeyafanyia vitendo na sasa tunajivunia kuwa na Vitendo SACCOS.

Pia mnanifurahisha sana mnavyoendesha huu mjadala, mimi nisingevumilia.

Napenda pia ku declare interest nikiwa kati watu wa mwanzo mwanzo kabisa kujiunga na wazo lenu na hatimae kuwa wa mwanzo mwanzo kujiunga na SACCOS hii mpya blindly, bila kuelewa nini kitatokea. Nilijisemea tu kimoyomoyo "hakuna ajuae ghaib isipokuwa Allah pekee" nika jiunga. Sasa nafurahi sana kuona maendeleo na speed kali kabisa.

Hakika tunafaidi sana katika whatsapp group la Vitendo SACCOS. Ni miujiza, wazo kuwa saccos, saccos kuwa action, action kuwa members na miradi ya majaribio in record time. Naomba ule mradi wa majaribio wa azolla, ambao mnatuma video vipande vipande kwenye group, mzicompile na kufanya video moja. Itapendeza sana.

Mwenyezi Mungu awajaalie, atujaalie kila la kheri katika hili jambo jema, lenye malengo mema, lenye tija njema. Na atuondoshee hasad.

Ramadhan Kareem.

In sha Allah narudi TZ Ramadhan za kati. Nikija tu futari Vitendo.

Ushauri, mmebadilisha jina la uzi si mbadilishe na avatar muweke ile logo ya Vitendo SACCOS.
 
Ni mfumo mzuri sana ila lazma hulka kwenye nidhamu ya fedha ni tatizo sana hapa kwetu. Niliona challenge hii Amana bank Kariakoo. Wakopeshwaji ni tatizo inapelekea management kuwa kubwa sana.
 
Ni mfumo mzuri sana ila lazma hulka kwenye nidhamu ya fedha ni tatizo sana hapa kwetu. Niliona challenge hii Amana bank Kariakoo. Wakopeshwaji ni tatizo inapelekea management kuwa kubwa sana.


Nimekuelewa.

Tunajaribu sana kushirikisha wadau mbali mbali wajiunge nasi ili tujaribu kuepukana na mambo kama hayo.

Karibu sana ujiunge nasi kwa maendeleo ya wengi.
 


Asante sana kwa ushauri wako.

Tutaiweka logo tutapokuwa registered na tutafungua account ya Vitendo SACCOS, kwa sasa tutaendelea hivi hivi.
 
Nami pia nafurahi kuwa mtu mmojawapo kwenye SACCOS hii.... I see a lot of things ahead...Mungu atusaidie...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…