Kwanza kabisa natoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Bi
Zainab Tamim na mumeo, shoga'ngu, Bwana Abdul.
Nawapongeza sana jinsi mlivyoanzisha uzi huu uliokuwa wa kubadilishana mawazo tu na kwa muda mchache mawazo mmeyafanyia vitendo na sasa tunajivunia kuwa na Vitendo SACCOS.
Pia mnanifurahisha sana mnavyoendesha huu mjadala, mimi nisingevumilia.
Napenda pia ku declare interest nikiwa kati watu wa mwanzo mwanzo kabisa kujiunga na wazo lenu na hatimae kuwa wa mwanzo mwanzo kujiunga na SACCOS hii mpya blindly, bila kuelewa nini kitatokea. Nilijisemea tu kimoyomoyo "hakuna ajuae ghaib isipokuwa Allah pekee" nika jiunga. Sasa nafurahi sana kuona maendeleo na speed kali kabisa.
Hakika tunafaidi sana katika whatsapp group la Vitendo SACCOS. Ni miujiza, wazo kuwa saccos, saccos kuwa action, action kuwa members na miradi ya majaribio in record time. Naomba ule mradi wa majaribio wa azolla, ambao mnatuma video vipande vipande kwenye group, mzicompile na kufanya video moja. Itapendeza sana.
Mwenyezi Mungu awajaalie, atujaalie kila la kheri katika hili jambo jema, lenye malengo mema, lenye tija njema. Na atuondoshee hasad.
Ramadhan Kareem.
In sha Allah narudi TZ Ramadhan za kati. Nikija tu futari Vitendo.
Ushauri, mmebadilisha jina la uzi si mbadilishe na avatar muweke ile logo ya Vitendo SACCOS.