Nsimbinso
JF-Expert Member
- Dec 15, 2020
- 407
- 431
Habari wadau.
Imekuwa kawaida kusimamishwa na Askari wa barabarani kwa ajili ya ukaguzi. Huu ni moja kati ya wajibu wao wa msingi kwa ajili ya kuhakikisha usalama wetu watumia vyombo vya usafiri pamoja na wote wanaotumia barabara au wenye shughuli zao pembezoni mwa barabara.
Baadhi ya askari wanatekeleza wajibu huu kwa weledi mkubwa, kiasi kwamba wanapokagua gari lako unaona fahari. Kuna baadhi yao mimi huwa siwaelewi kabisa.
Tucheki kwa pamoja baadhi ya matukio niliyokutana nayo ambayo binafsi nakosa jina la kuyapa.
1. Nishawahi kukaguliwa na askari, kaomba fire extinguisher nikampatia, akaikagua ikawa poa. Akaomba reflector triangle nikampatia. Akaniambia niwashe taa za parking, zikawaka. Akaniambia nikanyage break akague taa za break. Sikuwa mbishi, nikakanyaga. Akanifuata na machine yake ya kukagulia gari akaniambia taa za break haziwaki. Akaanza kuandika fine. Nikamwomba asubirie.
Nikamwomba abiria aje akanyage pedal ya break nikazunguka kukagua mwenyewe. Cha ajabu nikakuta taa zinawaka. Nikamuita askari, eti akaanza kushangaa na kujiapia kuwa hazikuwa zinawaka. Nikasepa bila kuandikiwa fine.
2. Tukio lingine ambapo niliandikiwa fine nilikuwa nyuma ya semi trailer. Barabara ilizuia ku-over take. Ni sahihi kabisa.
Palikuwa na mpando ambao haukuzuia dereva wa nyuma kuona mbele. Nilitembea nyuma ya hii semi trailer kwa kilometer kadhaa. Hofu ikawa ni mwendo na uimara wa gari lililokuwa mbele yangu kwani niliona lilivokuwa linapanda kile kilima kwa tabu. Nikalipita...
Bahati mbaya askari huyo. Swali likawa kwanini nime-over take mahali pale. Nilimjibu kuwa tumezuiwa ku-over take pale sababu ya usalama... Ila usalama ni uko wapi, kukaa nyuma ya ile semi ambayo mwendo na aina ya mzigo iliyobeba vinaonekana ku-fail na kunikandamiza hapo nyuma muda wowote.
Busara ni kubaki hapo au kusaka usalama zaidi hata kama ni kwa kukiuka baadhi ya sheria za barabarani ambazo hazina madhara kwa mazingira husika, akaniambia nisimfundishe kazi, akanilima fine.
3. Tukio jingine ambalo mpaka muda huu naliwaza; mwezi uliopita nilipata ajali, Gari yangu iliharibika, waliofika eneo la tukio wakafuata process za kipolisi, wa gari garage. Kwa vile uchumi si rafiki kipindi hiki nikaomba gari ikae garage mpaka nitapojikusanya na nitapotoka hospitali. Kulikuwa na penalty ambayo baada ya ajali nilikaa hospitali siku kadhaa hivyo muda ukapita ikawa imeongezeka. Cha ajabu traffic police wakawa wanapita kwenye ma-garage kukagua madeni. Wakakuta gari langu limebondeka halifai na lina penalty ipo pending.
Chap wale askari wakanipigia nikawaeleza ndo nimetoka hospitali na sipo vizuri kiuchumi, ndio maana gari bado haijaanza kurekebishwa. Yule askari aligoma kuelewa, akaita breakdown wakabeba gari kutoka garage kwenda polisi huku akisema Serikali inataka mapato na nitafute pesa ya kulipia fine na pesa ya breakdown. Hao wakaburuza gari tena wakisababisha damages mpya ambazo zitanicost pesa zaidi wakati wa kutengeneza gari.
Haya ni baadhi ya matukio ambayo yamenifanya niwatafakari baadhi ya hawa watanzania wenzetu waliopewa dhamana ya kusimamia usalama wetu barabarani na kuniacha na maswali kadhaa.