Wazazi wanatumia pesa ndefu kusomesha vijana wao, wanawagaharamikia hadi kuwasomesha vyuo vya nje ili wawe nuru na mwangaza na mifano ya kuigwa katika jamii lkn matokeo yake ndo haya.
Kuna jirani yangu mzee mstaafu alikuwa maarufu sana enzi za mzee wa msoga pale magogoni presha haimuishi kwa sasa, kasomesha ulaya watoto wake wawili wa pekee(ke & me), matokeo yake watoto wamekuja likizo na wachumba wao yaani wa kike kaja na girlfriend wake, wa kiume kaja na boyfriend wake yaani jamaa anapelekewa moto. Imeenda huku na huku mama presha kakata moto.
Mzee kwa sasa hawataki watoto wale ila ndo hivyo tena kaasili mtoto mwingine, hana matumaini na uzao wake..., mzee kabaki kujilaumu tu kwamba bora angewazingatia kwenye malezi, alikuwa bize kuwatafutia tu akasahau kuwa walihitaji malezi yake.
Wazazi tuzingatieni sana malezi kwa watoto wetu, haya malezi ya kulelewa na walimu siyo malezi.