Viti bandari ya Unguja vibovu, mazingira pia machafu, mamlaka hamuoni hiki kinachoendelea?

Viti bandari ya Unguja vibovu, mazingira pia machafu, mamlaka hamuoni hiki kinachoendelea?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Nimekuwa na kawaida ya kusafiri kwenda Zanzibar mara kwa mara, kuna hili jambo limekuw alikinikera naona leo nilitolee povu, ni kuhusu baadhi ya viti vinavyotumiwa na abiria kusubiri muda wa kuanza safari. Hali ni mbaya, viti kadhaa vimeharibika na mamlaka zipo kimya tu, sometimes pia maeneo yanakuwa machafu wanashindwa kusafisha, ukijumlisha na joto linalokuwepo eneo hilo wakati wa mchana, hali inazidi kuwa mbaya. Mamlaka ya Bandari hamoni huu uchafu?

photo_2023-01-28_08-03-38.jpg

photo_2023-01-28_08-03-36.jpg
 
Najaribu tu kuwaza, kama sehemu ya kukaa inayoonekana ni mbovu hivyo, vipi maliwato kusipoonekana kutakuwaje!!!!
 
Back
Top Bottom