Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 2,188
- 4,116
Kimpira ni jambo la manufaa sana. Itapendeza siku moja uwanja wa Jamhuri uwe na hadhi ya CAF. Ila kitechnical ni sahihi viti vya uwanja wa umma kupelekwa uwanja binafsi?
====
Meneja wa Uwanja wa Jamhuri uliopo Mkoani Morogoro, John Simkoko amesema uwanja huo unatarajiwa kufungwa viti ambavyo vimetolewa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo amesema mpaka sasa tayari wamepokea viti elfu tatu kwa awamu ya kwanza huku wakitarajia kupokea viti elfu sita
Simkoko ameyasema hayo Machi 24, 2026 ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano mzuri kati ya Viongozi wa Chama cha Soka Mkoa Morogoro (MRAFA) na Chama cha Mapinduzi umesaidia kufanya maboresho ya uwanja kunzia eneo la kuchezea, jukwani, na vyumba vya kubadilishia nguo.
Aidha kwa upande wake Katibu wa Chama Cha soka Mkoa wa Morogoro (MRFA) Alfred Mdende amesema maboresho ya Uwanja huo umeanza kuvutia timu mbalimbali ikiwemo Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu ambao wanataka kutumia uwanja wao wa nyumbani.