PreGE2025 Viti Maalum nafasi zinazowalea wanawake kushindwa kwenda majimboni

PreGE2025 Viti Maalum nafasi zinazowalea wanawake kushindwa kwenda majimboni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Habari Hub

Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
11
Reaction score
0
Na Mwandihi wa Habari Hub

Katika Kikao cha 76 cha UNGA, Baraza Kuu kwa makubaliano liliitangaza tarehe 24 Juni kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya wanawake katika diplomasia.

Kwa azimio hilo (A/RES/76/269) Baraza kuu lilizialika nchi zote wanachama, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za kitaaluma na vyama vya wanadiplomasia wanawake popote walipo kuadhimisha siku hiyo kwa namna ambayo kila mmoja anaizingatia kwa usahihi zaidi.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (77) ibara ya 12 (i, na ii) inaonesha misingi ya usawa inavyotakiwa kutoa miongozo kwenye misingi ya sera na sheria zote ambazo zinahakikisha upatikanaji wa haki za binadamu. Ibara ya 21 (ii) ya katiba hiyo inasisitiza ushiriki wa wananchi katika masuala ya michakato ya utawala na uongozi. Kutokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanyika 2014, ibara ya 66(i) iliweka hatua mahususi (Affirmative action) za kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi.

Juhudi za kutaka kuongeza idadi ya wanawake kwenye vyombo vya uwakilishi kwa upande wa Bunge,zilionekana mwaka 1985.Katika kipindi hicho ndipo wabunge 15 wa kwanza wa viti maalum walipopatikana.

Viti maalumu vya wanawake ni nafasi zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kuongeza idadi ya wanawake katika Bunge na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ingawa utaratibu huo hutumiwa na nchi mbalimbali duniani katika siasa.

Uwakilishi wa wanawake kupitia viti maalumu, sio wa kudumu ni nafasi za kujiandaa kisiasa, pamoja na kuandaa mbinu za kupata ushindi wanapokwenda jimboni ili iwe rahisi kwao kushinda na kuwatumikia wananchi. Lakini kinachotokezea kwa baadhi ya wanawake wanaopata nafasi hizo,wanahudumu kwa muda mrefu, tofauti na malengo na hio kuwalemaza kwa kuwa na hofu ya kuingia majimboni.

Akiwa mwanasiasa ambaye amepata nafasi ya kuchaguliwa katika nafasi ya viti maalum Asya Mohamed, ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA anasema ni kweli viti maalum vinawalemaza baadhi ya wanawake wanaopata nafasi hizo.Amesema kuwa, vyama haviwazuii pia kuendelea kugombea nafasi hizo, kwani hakuna sheria maalum iliyoweka ukomo wa viti maalum wa muda wa kugombea.”Ni vyema kukaa miaka mitano tu inatosha kujipanga na kujiandaa kwenda jimboni kwani na wengine wanataka nafasi hizo ili kujifunza”Anashauri Mbunge huyo.

Licha ya kuwepo kwenye nafasi hio anaona ni vyema kuwepo kwa sheria itayoelekeza ukomo na sheria maalumu “Sheria ikiwepo ikatoa ukomo itasaidia wanawake ambao wapo kwenye nafasi hizo, kukaa kipindi kimoja tu ili nafasi hizo, zisiwalemaze “Anamaliza Asya.

Takwimu kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar idadi ya wajumbe wote ni 78 kati yao wanawake ni 29 na wanaume 48, huku wanawake wawakilishi wa majimbo kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni wanne tu, wanaume wakiwa 42 na wanawake wa viti maalum ni 18 na wajumbe waliobakia ni nafasi za kuteuliwa na Rais.

Rais wa Zanzibar anamamlaka ya kuwachagua wawakilishi wa viti maalum na hii ni kutokana na utendaji wa kazi na hata matakwa ya chama kumpendekeza, Fatma Abdul habib Ferej ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT WAZALENDO, anasema kuwa wanawake wengi wanaochaguliwa katika nafasi za viti maalumu, wanaenda kinyume na dhamira ya kuanzishwa kwa nafasi hizo, kwa kudumu kwa muda mrefu.”Wapo wanawake wanaong’ang’ania nafasi za viti maalumu kwa miaka mingi ,japo uwezo wao unaruhusu kwenda jimboni kugombea na kujilemaza kisiasa”.

Amesema Fatma na kuunga mkono suala la kuwepo kwa sheria ya ukomo wa nafasi za viti maalum, kwani ipo haja kwa wanawake kuingia kwenye majimbo kugombea ili kuongeza wingi wao.” Ule ni mfumo mzuri wa kijifunza kutoka kwao, ni Rais Samia ambae alikaa kwa kipindi kimoja tu katika nafasi za viti maalum na kijitupa jimboni katika jimbo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.” Anamaliza.

1749547908714.jpeg

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja Asha Abdalla Mussa anasema kuwa, hakupita kwenye viti maalum alitoka kwenye nafasi ya udiwani na kugombea jimboni kwa sababu aliona kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.,”Wanawake tukiamua tunaweza ni vizuri kuwa na uthubutu na kujiamini na utafanikiwa”.Amesema Mwakilishi huyo huku akiwasihi wanawake mwaka 2025 kuchangamkia fursa za majimboni na wakikosa watarudi kwenye viti maalum.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake kwa upande wa Zanzibar wanajihusisha moja kwa moja kwenye kuwasaidia wanawake kujitokeza kwenye masuala ya uongozi.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA-Z DKt Mzuri anasema ni kweli vyama vya siasa haviwasaidii wanawake kuondokana katika nafasi za viti maalumu.’’ Kuna mtu utamkuta yupo anagombea kiti maalumu miaka mitano hii na mingine na bado yupo hapo hapo wakati inatakiwa mtu akae miaka mitano ajifunze kisha atokee aende jimboni akagombee” ameshauri Dk Mzuri.

Dkt Mzuri anaongeza kuwa, kutokana na hali hiyo ipo haja ya wanawake kuongezeka katika nafasi za uwakilishi katika majimbo ya uchaguzi ifikapo 2025 “Vyama na wanawake wenyewe wajidhatiti kwenye uwezo wa kutoka kwenye nafasi hizo na Kwenda kuonesha uwezo wao kwenye majimbo” Anashauri.

Ripoti ya sensa ya watu na makaazi ya Tanzania ya mwaka 2022, inaonesha kuwa Zanzibar ina wakaazi milioni 1.8 kati ya hao wanaume ni 915,492 na wanawake ni 974,281.hii ina maana kwamba wanawake ni asilimia 51.6 ya wakaazi wote wa Zanzibar, lakini wingi huo hauonekani katika nafasi za uongozi.
 
Back
Top Bottom