Elections 2010 Viti maalumu chadema vyazidi kupasua kichwa

Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Posts
11,503
Reaction score
20,892
Gazeti la Mwananchi linareport hivi:

MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.

“Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie,” kilisema chanzo kimoja na kufafanua:

“Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,”.
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.

“Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena,” kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.

Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
“Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama,” kilisema chanzo kingine.

Chanzo kiningine kilidai: “Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye” .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
“Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura.”

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.

Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.

Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.

Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.

Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.

“Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni.” Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.

Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.

“Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu,” alieleza mmoja wa mapambe hao.

Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.

Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.

Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: “Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo

MY USHAURI:
Kama habari hii ni ya kweli, kuna haJa ya CHADEMA kumaliza issue hii haraka sana ''once and for all''. Mnatutia shaka sana sisi wenye mapenzi mema na tunaojiandaa kuwapigia kura za NDIO na kuwakabidhi nchi hii hapo 31st Oct.

Kama zoezi ''dogo'' la kuwapata wanawake kwa uwakilishi wa viti maalumu inakuwa issue, itakuwaje sasa kwenye uwaziri, ukuu wa mikoa etc??
 
Viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa

Saturday, 25 September 2010 22:41

Fredy Azzah na Frederick Katulanda, Mwanza (Mwananchi)

MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.

"Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie," kilisema chanzo kimoja na kufafanua:

"Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,".
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.
"Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena," kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.

Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
"Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama," kilisema chanzo kingine.

Chanzo kiningine kilidai: "Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye" .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
"Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura."

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.

Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.

Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.

Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.

Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.

"Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni." Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.

Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.

"Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu," alieleza mmoja wa mapambe hao.

Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.

Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.

Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: "Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo.
 
Amani haiji, ila kwa ncha ya upanga.

MIMI NAONA NI MAMBO YA KAWAIDA TU HAYA, HASA KWA VYAMA vilivyo na chati kama CHADEMA.
Mara nyingi migogoro ya namna hii huwa kama chekecheo la kuwachambua watu wenye nia mbaya na chama na kuwatenga, kwahiyo ni changamoto nzuri sana!

Ukiangalia historia za vyama vingi, hata nchi za jirani, zimekuwa za mapambano, lakini hatimaye miafaka hufikiwa, na hiyo huwa ndio precedence ya cases zingine zitakazojitokeza mbele!

Slaa For Presidency 2010
 
Note: Hili suala la Elimu kumbe ni muhimu sana. Sielewei ilikuwaje Slaa akabeba ndumbaro ya STD 7 kuwa mgombea mwenza?!

Viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa Viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa

Fredy Azzah na Frederick Katulanda, Mwanza
MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.

“Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie,” kilisema chanzo kimoja na kufafanua:

“Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,”.
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.
“Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena,” kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.

Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
“Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama,” kilisema chanzo kingine.

Chanzo kiningine kilidai: “Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye” .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
“Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura.”

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.

Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.

Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.

Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.

Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.

“Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni.” Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.

Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.

“Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu,” alieleza mmoja wa mapambe hao.

Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.

Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.

Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: “Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo
 
Mimi nafikiri ni dalili ya demokrasia kukomaa ni vizuri ja0bo hili lijadiliwe kwa kina 2abla ya uamuzi wa mw5sho kufikiwa.
 
Teh teh teh. Eti kawaida kwa "vyama vilivyokuwa na chati". Teh teh teh.

Halafu Slaa akigeuka kuwa fisadi baada ya kuukwaa Urais (kitu ambacho hakiwezekani) tutaambiwa hiyo ndiyo kawaida kwa "vyama vinavyokuwa madarakani".
 
Hizo ni rafu za mfa maji. kuna fununu kuwa masha ameugua, mwenye details atumwagie
 
Teh teh teh. Eti kawaida kwa "vyama vilivyokuwa na chati". Teh teh teh.

Halafu Slaa akigeuka kuwa fisadi baada ya kuukwaa Urais (kitu ambacho hakiwezekani) tutaambiwa hiyo ndiyo kawaida kwa "vyama vinavyokuwa madarakani".
On the bold speakes itself, chama chenye uhakika wa kupata viti vingi bungeni ndicho kinachogombaniwa, kwanini watu wagombane ndani ya SAU wakati hakina uhakika wa kupata hata kiti kimoja?
 
Yeah sure wakuu, hayo ni mambo ya chama kushika hatamu. Hao wanaogombania ni kwa kuwa wanauchungu na nchi yao, kila mmoja anataka kuwa katika historia kuleta mageuzi/mapinduzi makubwa kwa watz ili hatimaye hapo baadae waitwe mashujaa wa hii nchi yetu.

Dr Slaa for Presdency this year. No mistake at all.
 
TAYARI WATU WENYE AGENDA YA SIRI TARATIBU AIBU YAO INAANZA KUONEKANA, HAWA CHADEMA ATI NDIO WANATAKA KUONGOZA TZ!!! WAMESHAANZA KUGOMBEA MADARAKA HATA KABLA UCHAGUZI HAUJAFANYIKA!!!!

HABARI KAMILI SOMA HAPA:
Viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa

I like that news. This is the home of Great Thinkers.

Kadogoo, hiyo ndio hasa maana ya demokrasia ambayo chama chako kimekosa. Haiwezekani katika kikundi cha watu mkawa na mawazo na misimamo sawa. Kutokana na migongano ya mawazo ndipo mambo huenda mbele. Ungejifunza social psychology ungeelewa nina maanisha nini. Hiyo inaitwa "conflict". Na si ugomvi kama mnavyofikiria, ila ni mgongano wa mawazo.

Laiti chama chako kingejifunza hiyo njia ya uhuru wa mawazo na kukubali changamoto, msingetishiana kuvuana uanachama pale Dodoma. Na pia msingetumia mabilioni yote hayo kumnadi rais aliye madarakani.

Wajua ni kwanini manguvu na mahela yanatumiwa na chama chako kumnadi mgombea wake! The answer is very very simple, "Hakutimiza wajibu wake".
 
Si wapendi waandishi wa habari kwa kupotosha umma, sijui hawana dini? au hawana utu. hivi huwa wanaenda kanisani? mbona wanakiherehere sana? habari wamezipata wapi?
 
Wakipiga kura, viti vitaenda mikoani wakati wao wanataka kuchagua hao wanawake wanaowataka, wanaotumia nao Dar. Hapo tutapata ubunge wa chupi tu.

Wakitaka kuepuka balaa lingine kwenye viti vya wanawake lazima wawaachie wanawake wenyewe wachague.
 
CHADEMA si chama cha mafisadi, ambacho kinatumia udikiteta ktk kupitisha maamuzi yake.
 
chama cha demokrasia na maendeleo kinapokosa maendeleo ya demokrasia

kwa nini kwenye viti maalum kuwe na vigezo vya elimu wakati kwenye kura za wananchi wengi za majimbo kigezo cha elimu kisiwepo?kwanini chadema wanatoa nafasi kwa skeptics juu ya ubaguzi mdodogo uliopo katika upatikanaji wa nyadhifa mbalimbali ndani ya chadema?bila shaka issue ya elimu lazima itawafavour watu flanflan kutoka kanda flanflan na kuwadiscriminate wengine.

ni mambo kama haya ndipo watu wanakwesheni weledi wa chadema katika kutatua mizzozo na kuondoa elementi za ukanda zinazoitafuna, kwa nini msiwaache wanachama wawe huru zaidi?
 
Wakipiga kura, viti vitaenda mikoani wakati wao wanataka kuchagua hao wanawake wanaowataka, wanaotumia nao Dar. Hapo tutapata ubunge wa chupi tu.

Wakitaka kuepuka balaa lingine kwenye viti vya wanawake lazima wawaachie wanawake wenyewe wachague.
Una DADA nini kwenye kamati kuu.
 
Wakipiga kura, viti vitaenda mikoani wakati wao wanataka kuchagua hao wanawake wanaowataka, wanaotumia nao Dar. Hapo tutapata ubunge wa chupi tu.

Wakitaka kuepuka balaa lingine kwenye viti vya wanawake lazima wawaachie wanawake wenyewe wachague.
Hii inaeleza zaidi ya ulivyo, CCM huwa na kigezo hicho ambacho Sophia Simba hukitumia kugawa kama pipi.
 
Wabunge Viti Maalum Chadema hapatoshi

Na Mwandishi wetu

26th September 2010

headline_bullet.jpg
Waweka vigezo vya kukatisha tamaa
headline_bullet.jpg
Kama siyo msomi mwenye Phd hupati
headline_bullet.jpg
Darasa la saba ndiyo kabisa hataona ndani

Mkutano Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umeanza jana jijini Dar es Salaam huku ukiweka vigezo vya mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalum kuwa ni lazima wawe wawajibikaji na wasomi wanaoanzia Shahada ya Uzamifu (Phd).
Pamoja na mambo mengine Mkutano huo maalum ulioanza Jijini Dar es Salaam jana, pia unajadili mwenendo wa kampeni za chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao wa Urais na Wabunge zinavyoendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya mkutano huo, bado kuna mvutano mkubwa juu ya namna ya kuwapata wabunge wa Viti Maalum.
Taarifa hiyo ilisema, vigezo vilivyowekwa kusaidia kuwapata wabunge hao ni elimu ya mgombea na pia uwajibikaji wake kwa chama na kwa wananchi," kilisema chanzo hicho.
"Kama mtu ana shahada ya uzamifu (Phd) atapata alama 10 zitakazomuwezesha kuwa na uhakika wa kupata ubunge wa Viti Maalum kupitia Bawacha (Baraza la Wanawake wa Chadema).
Aidha, kama ana shahada ya Uzamili atapata alama 8, Stashada alama 6, Astashahada alama 4, Kidato cha Sita alama 2, na Darasa la Saba ni alama 0," kilisema chanzo hicho.
Mkutano huo unaoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na ulio katika ulinzi mkali na usiri, uliteua kamati ndogo ya kushughulikia mchakato mzima wa uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum kupitia Bawacha.
Kamati hiyo yenye wajumbe watano inaongozwa na Dk. Mkumbo Kitila ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano uliovunjika wa kuteua wabunge wa Viti Maalum mwezi uliopita.
"Sisi tuko makini sana katika hilo na hatutoi ubunge kama zawadi au kwa kujuana na ndiyo maana tumeunda kamati hiyo iliyo chini ya msomi maarufu ili kupata wawakilishi wazuri."
"Kama kuna mtu anajidanganya kwa kukaa bila ya kuwajibika jimboni alipo, basi hiyo imekula kwake. Unajua asiyefanya kazi na asile kila mtu atakula kwa juhudi zake kwani hakuna kubebana hapa".
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alisema "mimi nitaongea na waandishi kesho kwa leo nisameheni kwani nina kazi nyingi kwa ajili ya taarifa ya kesho," alisema. Dk. Slaa ni mgombea Urais kupitia chama hicho.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe alisema,"Mimi sio msemaji, mfuateni Katibu Mkuu ndiye anajua cha kusema na atakachosema ndiyo maamuzi ya chama.
Mkutano huo wa siku mbili umesababisha kusimama kwa kampeni za mgombea Urais na baadhi ya wagombea ubunge akiwemo John Mnyika wa Ubungo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Ninachojua mimi ni kwamba kimsingi - narudi, kimsingi - CCM inawaogopa Wabunge Viti Maalum wa CHADEMA. Ipo mifano hai ya jinsi wabunge hawa walivyoichachafya CCM bungeni; Halima Mdee, Grace Kiwelu, Mhonga Said, ni baadhi tu ya wabunge mahiri wanawake (viti maalum) wa CHADEMA, ambao waliipa CCM na serikali yake wakati mgumu.

Kinachofanyika ni kwamba, wako MAMLUKI ambao wamepandikizwa ndani ya CHADEMA, ambao wanataka kuhakikisha kwamba Wabunge wa Viti Maalum watakaopitishwa watakuwa wale ambao HAWATAICHACHAFYA CCM bungeni. Lakini hili haliwezekani. Hata ukiwaondoa akina Halima Mdee, Grace Kiwelu, Mhonga Said, utawapata wengine ambao ni DAMU ILE ILE.

CCM inajisumbua. Hampati kitu! Watapatikana wabunge mahiri wa CHADEMA, viti maalum, tena mwaka huu watakuwa WENGI ZAIDI! CCM mkae mkao wa kuwa CHAMA CHA UPINZANI, kama wenzenu wa KANU kule Kenya!

Huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM! Kila chenye mwanzo kina mwisho. Kubalini yaishe, MSITULETEE VITA BILA SABABU!
 
Amani haiji, ila kwa ncha ya upanga.

MIMI NAONA NI MAMBO YA KAWAIDA TU HAYA, HASA KWA VYAMA vilivyo na chati kama CHADEMA.
Mara nyingi migogoro ya namna hii huwa kama chekecheo la kuwachambua watu wenye nia mbaya na chama na kuwatenga, kwahiyo ni changamoto nzuri sana!

Ukiangalia historia za vyama vingi, hata nchi za jirani, zimekuwa za mapambano, lakini hatimaye miafaka hufikiwa, na hiyo huwa ndio precedence ya cases zingine zitakazojitokeza mbele!

Slaa For Presidency 2010
thanx mkulu kwa mawazo ya hekima.
 
Back
Top Bottom