Elections 2010 Viti maalumu chadema vyazidi kupasua kichwa

Elections 2010 Viti maalumu chadema vyazidi kupasua kichwa

amani haiji, ila kwa ncha ya upanga.

mimi naona ni mambo ya kawaida tu haya, hasa kwa vyama vilivyo na chati kama chadema.
mara nyingi migogoro ya namna hii huwa kama chekecheo la kuwachambua watu wenye nia mbaya na chama na kuwatenga, kwahiyo ni changamoto nzuri sana!

ukiangalia historia za vyama vingi, hata nchi za jirani, zimekuwa za mapambano, lakini hatimaye miafaka hufikiwa, na hiyo huwa ndio precedence ya cases zingine zitakazojitokeza mbele!

slaa for presidency 2010
nccr-mageuzi yaliwakuta kama haya miaka ya 90 na sasa nccr ni kama marehemu!!! Dalili za mvua ni mawingu!!! Kugombania vyeo hata kabla uchaguzi haujafanyika!!!!
Aibu tupu chadema yaani ni kichefuchefu!!!
 
Mimi nadhani hapa hakuna hoja ya msingi zaidi ya kutafuta makosa ambayo sii makosa ya chama ila ni mambo ya kawaida kabisa. Ndani ya CCM, CUF na vyama vinginevyo maswala kama haya yapo sana tu kwani tatizo ni umaskini na pengine ELIMU yenyewe hivyo nafasi kama hizi ndio mahala pa ulaji. Hizi ni fkra binafsi zenye ubinafsi zaidi ya sababu zilizotolewa.

Hili swala la wagombea binafsi linatakiwa uwakilishi wa taasisi husika na sii kila mtu kugombea nafasi hiyo ila yule anaye qualify wadhifa wa uwakilishi wa taasisi hiyo... Kwa mfano ikiwa swala ni Uwaziri, Umoja wa kina mama, vijana, walemavu au hata maswala ya sheria na katiba inatakiwa watu watakao chaguliwa kuwa na uwezo wa kuwakilisha nafasi hizo sio mtu kuchaguliwa kwa sababu kasoma (ELIMU) sijui wameandaliwa au anatoka mikoa mingine isiyo ya kaskazini na kadhalika.

Matatizo haya ndio yamekuwpo CCM siku zote na ndio yaliyotufikisha hapa tulipo, hivyo Chadema nao wakianza kufikiria kama CCM kuanza kumchambua mtu mbele ya jukumu atakalo shika iwe la uwakilishi au uongozi hapo ndipo tunakuta Madaktari wakipewa wizara ya fedha. Au mtu maarufu kushika nafasi asiweze kabisa kuiwakilisha kwa sababu hafahamu yaliyomo.

Huu ni wakati wa kuondoa fikra dhaifu na kwamba Uongozi ni dhamana kwa wanachi wote na kinachoweza kuwaokoa ni uwakilishi bora ktk nafasi husika..Ni wakati wa kuondoa zile fikra za kwamba rais akiwa Muislaam basi lazima makamu wake awe mkristu na kila upande uchukue awamu mbili za uongozi kama vile nchi inaongozwa na itikadi za dini.

Ni wakati wa kuondokana kabisa na fikra za kwamba rais akitoka bara basi ni lazima mgombea mwenza atoke Zanzibar hata kama viongozi bora na wenye nafasi kubwa ya ushindi wote wanatoka Zanzibar. Nitarudia kusema tena kwamba hakuna Mchagga ambaye ni mchagga wa Moshi asiwe wa Dar es salaam au Tabora wala Mzanzibar wa Zanzibar ambaye sii mbara ila sote ni kitu kimoja tukiwa na tofauti zetu..

Kuna mwanabodi kwa jina akiitwa AMI aliuliza nini hasa maana ya Udini ktk moja ya mada na hakika moja ya Udini au Ukabila huanzishwa na mgawanyiko kama huu, mpango wowote wa kuwagawa wananchi kwa dini, mipaka au makabila yao ndio chanzo cha Ubaguzi wowote ule iwe yaliyotokea Kenya, Rwanda au hata Nigeria. Kinachotangulia yote ni zile fikra za SISI against WAO kiasi kwamba hata yule anayejisikia inferior akianzisha vurumai la kudai haki kwa kuzungumzia nafasi yake ktk jumuiya hali hana uwezo wa kuongoza ndipo tatizo linapokuja kwani haki ya kabila, dini au jinsia haianzi na kushika madaraka makubwa ya uongozi bali ni kudai haki sawa pasipo kubaguliwa kwa kundi zima la wananchi wenye asili hiyo..

La mwisho na muhimu zaidi Ubunge wa viti maalum hauwakilishi watu wa sehemu fulani bali ni uwakilishi wa taasisi (zilizopendekezwa) kwani kuwakilisha majimbo au mikoa unatakiwa kugombea Ubunge au udiwani kwa kuchaguliwa na wananchi. Kama huyo mbunge wa Shinyanga anataka kuwakilisha Shinyanga ktk viti maalum kwa kupiga kura basi angefikiria hilo mwanzo na kujiandikisha kugombea ubunge au udiwani na apigiwe kura na wananchi na sio kuwakilisha jimbo au mkoa kwa kupitia viti maalum.

Nauomba Uongozi wa Chadema uchukue jukumu na maamuzi ya mwisho kuchagua watu wa viti maalum kwa kufuata vigezo vya taasisi ambazo Dr. Slaa anataka kusimamisha Kitaifa..
 
kazi kweli, mnataka dola ilihali isse ndogo tu inawasumbua namna hii
 
wakuu, safari hii nawasilisha kupitia mdomo wa ccm:

Tuesday, 28 September 2010 12:03 administrator
http://www.uhurupublications.com/in...hdGlkPTc3OnBlcnNvbmFsLXRlY2gmSXRlbWlkPTE3Ng== http://www.uhurupublications.com/in...t=default&page=&option=com_content&Itemid=176 http://www.uhurupublications.com/in...dema&format=pdf&option=com_content&Itemid=176

NA HAMIS SHIMYE
MIZENGWE imeendelea kutawala ndani ya CHADEMA kuhusu utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti maalumu, ambapo wagombea wote wametakiwa kujaza fomu upya. Mpango huo unatajwa una lengo la kuwaangusha wagombea walioshinda, ambao si wanamtandao na kuwarejesha ‘wazawa’.

Fomu hizo zimeanza kutolewa kwa wagombea kuanzia jana, huku baadhi ya walioshinda nafasi hizo katika uchaguzi wa awali, wakiweka bayana wataendelea kupigania haki hata kama ni kwenda mahakamani. Uchaguzi wa kuwapata wabunge wa viti maalumu uliofanyika Agosti 10, mwaka huu, haukumalizika kwa amani kutokana na wabunge wanaomaliza muda wao, ambao ni chaguo la viongozi wa juu kuangushwa.

Tangu wakati huo, makundi ndani ya CHADEMA yaliibuka, ambapo Mwenyekiti wa mkutano huo Dk. Kitila Mkumbo, alilazimika kuuahirisha kwa madai taratibu zilikiukwa. Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichoketi juzi, zilisema kutolewa fomu hizo ni mpango wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, kujaribu kuwarejesha baadhi ya wabunge wa zamani. Imeelezwa iwapo mpango huo wa Mbowe utafanikiwa, hali ndani ya CHADEMA itazidi kuwa tata, kutokana na ukweli kwamba, imekuwa ikitafunwa na dhana ya u-kaskazini.

Chanzo chetu ndani ya kikao hicho kilibainisha fomu hizo zimetolewa na wahusika kutakiwa kujaza bila muongozo kutolewa kwa madai kuwa ni serikali.

“Wagombea wote tuliogombea ubunge viti maalumu tumeambiwa tuchukue fomu na kuzijaza, hatujui zina lengo gani na wala hatujaelezwa zaidi.

“Haya ni maamuzi mabovu na ni uamuzi wa mtu mmoja ndani ya chama, kwani haiwezekani tuambiwe tujaze fomu bila kupewa maelezo yoyote. Hatujui mkutano wa BAWACHA utafanyika lini?’’ kilisema chanzo hicho. CHADEMA imeingia katika mvutano kuhusu viti hivyo, kutokana na kuwepo makundi mawili yanayopinga, hivyo uchaguzi kutawaliwa na mizengwe.

Wabunge wa viti maalumu wanaomaliza muda wao ni Lucy Owenya, Grace Kihwelu, Halima Mdee, Anna Komu na Susan Lyimo, ambao inaelezwa waliangushwa katika uchaguzi wa awali, huku Mhonga Ruhwanya akinusurika kwa kile kilichodaiwa kutokuwa kwenye mtandao wa Kanda ya Kaskazini. Kutokana na mizengwe hiyo, baadhi ya viongozi na makada maarufu wameamua kuihama CHADEMA. Miongoni mwao yumo aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, David Kafulila, ambaye sasa yupo NCCR-Mageuzi. Kafulila alikuwa anagombea uenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) na kuwa kipenzi kwa kundi linalotaka mabadiliko ndani ya chama hicho, lakini aliwekewa mizengwe.

Mbali ya kiongozi huyo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, aliutikisa uongozi pale alipotangaza kupimana ubavu na Mbowe kuwania nafasi ya uenyekiti, lakini alikutana na mizengwe na kulazimishwa kuondoa jina.

Source: Uhuru

Gazeti la UHURU? Tangu lini habari zake zikaletwa hapa JF?

Hili linafaa sana kuwekwa Msalani ili watu walitumie huko........
 
Hizi ni spin za kundi na watu wenye akili finyu mithili ya wakina Salva!!
 
Ati Source ni nini? UHURU?

UPUPU!!! CHECHE!!! HAKUNA LA MAANA HUMO

(KWANZA SIJASOMA. HIVI UMEPOST NINI HAPO JUU??)
 
Ati Source ni nini? UHURU?

UPUPU!!! CHECHE!!! HAKUNA LA MAANA HUMO

(KWANZA SIJASOMA. HIVI UMEPOST NINI HAPO JUU??)

mkuu punguza munkari, badala yake soma hiyo habari na uweke hasira zako kwa hoja za kimantiki.
 
Sioni tatizo hapo. Ni mchakato, waacheni wajadiliane na hatimaye suluhisho litapatikana. Ni vizuri iwapo hawatumii fedha kupata nafasi kama wanavyofanya hawa mafisadi wa CCM.
 
Back
Top Bottom