Viti Maalumu Vishindaniwe Kwa Wananchi na Sio Kubebana, Kuimarisha Uwakilishi wa Wanawake Kupitia Ushindani wa Kikweli

Viti Maalumu Vishindaniwe Kwa Wananchi na Sio Kubebana, Kuimarisha Uwakilishi wa Wanawake Kupitia Ushindani wa Kikweli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuelekea Uchaguzi Mkuu hapa nchini, mimi naona ni muhimu kuanzishwe mfumo mpya utakaofanya wanawake wa vyama mbalimbali wapambane kutafuta kura kwa wananchi moja kwa moja kuliko mfumo wa sasa ambapo viti hivyo vinaonekana kama fadhila au hisani za viongozi kwa wanawake kuliko stahili yao iliyotokana na uwezo.

Mfumo wa sasa umeonyesha udhaifu katika kutoa uwakilishi wa kweli kwa wanawake, huku ukijikita zaidi kwenye upendeleo wa kidini, ukabila, na rushwa.
1727939381147.png
Katika mchakato wa uchaguzi, kuna mwito wa dharura kwa jamii na vyama vya siasa kuhamasisha wanawake kuchukua hatua za kujitafutia nafasi hizo, ili kuwezesha uwakilishi wa kweli unaozingatia uwezo na jitihada zao.

Mabadiliko haya ni muhimu ili kuondoa dhana ya viti maalumu kama fadhila na kuimarisha usawa wa kijinsia katika maamuzi ya kisiasa.

Pia, Soma:
=> Ni wakati wakufutilia mbali "Viti Maalumu ". Viongozi wachaguliwe based on Qualifications
=> Je, kuna umuhimu wa kuwa na wabunge wa viti maalum?
=> Kwanini wanawake huwa hawaoneshi nia ya kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za mitaa?
 
Back
Top Bottom