Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Awali ya yote napenda nisieleweke kama namlaumu mtu yeyote bali natoa maoni ya kitaalamu kwa baadhi mambo ambayo yangestahili kuzingatiwa wakati wa ujenzi wa uwanja huu. Ambao kwa sura ni mzuri unapendeza, lakini functionally sivyo.
Kuhusu viti, sio mara ya kwanza kusikia uharibifu. Kuanzia siku ya ufunguzi wake nilisikia palikuwa na uharibifu mpaka vyooni! Nikajiuliza kwanini iwe hivyo ilhali uwanja ni mpya kabisa? Na kwakuwa hali hii inaendelea hadi leo ina maana wahusika hawajuwi dawa ya tatizo hili.
Viti au vyoo vya public kwa ujumla huwezi kutumia vile vya nyumbani au maofisini. Kwahiyo kuna specifications za facility hizi ambazo zinakidhi matumizi ya rafu ie. Vandal Proof seats na public toilets and fixtures.
Baadhi ya kampuni zinazotengeneza vitu hivi ni daplast seats and bleachers, ambapo kuna aina kadhaa za viti eg. CR3, CR4, CRM nk. Hivi ya CR4 vimetumika katika baadi ya viwanja vya nchi kadhaa za Africa: Egypt, Libya, Morocco na Sudan.
Ni wazi kwamba viti vya uwanja wetu hata vyoo pia, havikukidhi vigezo nilivyotaja ambavyo vinakubalika na vigezo vya FIFA/UEFA. Vile pale nahisi vilitoka China na wahusika huenda waliuziwa mbuzi kwenye gunia. Hata hivyo bei niliyosikia ikitajwa ya Sh. za Tz. 200,000/- kwa kiti moja, inazua maswali pia. Nimefanya utafiti wa aina hiyo ya viti toka China ni US. Dollars 5 - 10 kwa kiti! Ambayo ni kama Sh. 12500 hadi 25,000/-.
Nashauri kabla ya kununua viti vipya au vinginevyo; kwamba ili kuepusha gharama za aina hii kujirudia rudia; wakati mnapojenga facility kama hizi na mnapokarabati, muwatumie wataalamu au washauri wenye ujuzi wa vitu hivi.