fokofu
Member
- Oct 17, 2012
- 68
- 74
VITU 4 MUHIMU UNAVYOPASWA KUVIJUA KABLA YA KUNUNUA USED IPHONE (IPHONE ILIYOTUMIKA)
(ukipuuza utazidi kupoteza pesa yako)
(ukipuuza utazidi kupoteza pesa yako)
Leo nitaanika siri ziunazofanywa na wauzaji wa simu zilizotumika used iphone, Iphone ni simu nzuri sana na kila mtu anatamani awe nayo ila siyo simu rahisi (bei rahisi) ni simu za bei ghali ukilinganisha na simu nyingine
Kwaiyo kama unahitaji kutumia iphone bila ya kulipia bei kamili (kununua mpya) basi iliyotumika (used) itakuwa chagua sahihi kwako, ila kuna vitu vichache inabidi uzingatie kabla ya kufanya chaguo lako:
KAMA UNA MPANGO WA KUNUNUA IPHONE VIFUATAVYO NI VITU VITAO MUHIMU UNAVYOTAKIWA KUFANYA KABLA YA KUFANYA CHAGUO LAKO
1. HAKIKISHA SIMU UNAYONUNUA HAIJAIBIWA (CLEAN IMEI)
Unaponunua iphone iliyotumika hakikisha umeangalia kama ipo clean IMEI or MEID number hapa siongelei ICLOUD LOCK naongelea (CLEAN IMEI), kampuni ya APPLE huwa wanafunga na kuzuia simu zilizoibiwa zisitumike na watu wapya unaweza ukaangalia kama simu siyo ya wizi au kama ina clean IMEI baada ya kufuata hatua zifuatazo:-
I. Tambua imei yako (kwa kubofya setting app kwenye iphone unayotaka kununua)
II. Kisha bofya general
III. Shuka chini na utaona sehemu ya namba za IMEI au MEID
pia unaweza kupata imei yako kwa kubofya *#06#
Baada ya kufuata hatua hizo kopi IMEI yako bila kukosea kisha tembelea fungua google na utafute website inayoitwa www.imeipro.info utaingiza IMEI ya simu kisha utabofya check itakuonyesha kama simu yako iko safi kwa kutoa maneno ya kijani yaliyoandikwa clean.
2. HAKIKISHA UBORA WA BATTERY (BATTERY HEALTH)
Kabla ya kununua iphone yako hakikisha ina battery imara,used iphone ambayo ipo vizuri huwa inakuwa na battery imara,unaweza kuangalia afya ya betri kwa kufuata hatua zifuatazo.
I. Bofya setting app.
II. Kisha bofya battery
III. Kasha bofya Battery
IV. Asilimia itakayoonyesha kwenye sehemu ya Maximum capacity itakuonyesha ubora wa betri yako, betri nzuri huwa ina 100%, simu itakayoonyesha ubora wabetri chini ya 80% omba muuzaji akubadilishie betri.
3. ANGALIA VIFAA VINGINE VYA SIMU KAMA VINAFANYA KAZI
Kila iphone iliyotumika ina uchakavu wake namaanisha mikwaruzo (scratches) mbele, nyuma, na pembeni. Vifaa vingine muhimu vya kuangalia kabla ya kununa sim ni: TOUCH ID, FACE ID au 3D Touch sensor, CAMERA LENS,
Kingine cha muhimu ni kuangalia simu yako kama ina angalia kama simu yako ina unyevuunyevu au imeathiriwa na maji (water damage sensor)
• kuangalia water damage sensor fuata vitu vifuatavyo
Fungua sehemu ya line kasha angalia kwa umakini kikaratasi cheupe kama unavyoona hapo chini kwenye picha unaweza ukatumia tochi kuweza kumulika kama hautakuwa unaona vizuri ukishakionahicho kikaratasi kama kinaonyesha rangi nyeupe kama ilivyo kwenye picha basi iphone yako ipo safi namaanisha haijaadhiriwa na maji au unyevunyevu kama kitaonyesha rangi nyekundu ujue simu yako inashida ya unyevuunyevu au imeingiliwa na maji
4. HAKIKISHA MUUZAJI ANATOA WARRANTY.
Njia nyingine rahisi ya kumjua muuzaji sahihi omba akupatie warranty. Muuzaji yoyote mwaminifu huwa anasimama nyuma ya bidhaa yake.
zaidi ya yote bado nina vitu vingi ambavyo sijavigusia hapa na siwezi kuviandika vyote hapa kuna vitu vingine bingo kama utajuaje kama simu yako ni used au refurbished, utajuaje kama simu yako ina display Original (LCD NA OLED) na nk.
KAMA UMEVUTIWA NA MAKALA HII NA KAMA UNAHITAJI KUJUA ZAIDI AU KUSHAURI ZAIDI USISITE KUNIANDIKIA COMMENT YAKO PIA UNAWEZA UKANICHEKI KWA 0777821974 (CALL & WHATSAPP)