Vitu 6 Vya Muhimu Kuzingatia Kuwa Mwanaume Wa Thamani Zaidi Kwenye Jamii Inayokuzunguka

Vitu 6 Vya Muhimu Kuzingatia Kuwa Mwanaume Wa Thamani Zaidi Kwenye Jamii Inayokuzunguka

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Mwanaume mwenye thamani mara nyingi hupata anachokitaka.
Maana ya mwanaume wa thamani ni mwanaume ambaye ana mvuto wa kimapenzi kwa wanawake na pia wanaume wanataka kuwa kama yeye au wanamuangalia kama kiongozi. Watu hupenda kuwa karibu naye na kumsaidia. Ili na wao wapate kitu toka kwake.
Hivyo zingatia vifuatavyo ili kuongeza thamani yako
.
Muonekano. Sio kwasababu uliumbwa na mwonekano fulani basi ukate tamaa, ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya muonekano wako unaweza kuongeza mvuto na kuongeza thamani yako. Kwa kuhakikisha umeweka nywele zako vizuri, umenyoa vizuri na kuvaa nguo zinazoendana na wewe. Unaweza kufanya mazoezi na mwili ukawa fiti.
.
Uwe pesa. Pesa ni ya muhimu lakini hakikisha una uhuru wa kifedha. Hata kama upo chini ya mtu, jitahidi uwe na biashara yako.
Lakini usije ukadhani kuwa hili ndo la muhimu kuliko vyote kwamba utaweza pata wanawake kirahisi, hapana kuna wanawake hawatovutiwa na wewe au watakutumia kwa pesa zako tu na hawana mpango na wewe.
.
Hadhi/ cheo/ nafasi yako kwenye jamii. Umaarufu na kuwa tajiri ni vitu vinavyoongeza hadhi lakini ni vigumu kupata kwa wanaume wengi. Ila kuna hadhi unayoweza kupata kwenye jamii uliyopo. Mfano, upo kwenye vikoba unaweza kuongeza ujuzi wako kwenye uendeshaji wa vikoba na kusaidia wengine, au kama upo kwenye kikundi cha madereva unaweza kuwaongoza wengine na kupanga matukio yenu. Na ukaongeza hadhi yako bila kuhitaji kuwa tajiri au mtu maarufu.
.
Uwe na uwezo wa kuongoza hisia zako. Na sio kuongozwa/ kupelekeshwa na hisia zako. Mtu ambaye anakasirika tu kwa vitu vidogo vidogo sio mtu ambaye watu watamuangalia kama kiongozi ila watakua wanajitahidi kumkwepa. Mfano, kama nikilumbana/ hatujaelewana na mchumba wangu kwa kuwa amesema kitu kilichoniudhi, natambua ninavyojisikia na kumwambia kuwa sijapenda ulichokisema/ ulichokifanya kinanifanya nijisikie hivi, badala ya kukasirika na kugombezana.
.
Uwe na mipaka. Ukiwa na mipaka maana yake unajiheshimu. Ukiona unaruhusu mtu kukuendesha au mwanamke kukuendesha kwa namna yoyote ile ujue kuna mipaka hujaiweka sawa. Unaweza ukawa na pesa na ukawa na hadhi lakini kama huna mipaka kwenye mahusiano uliyonayo thamani yako inashuka, hasa kwa wanawake.
Hivyo, kuwa na mipaka na uhakikishe inafuatwa.
Na mtu akivuka mipaka yako usisite kuachana naye au kuiweka sawa mipaka.
.
Kuwa na malengo kwenye maisha. Kisha fuata na vitendo vinavyokusukuma kufanikiwa kwenye malengo yako. Pia hakikisha unapata mafanikio hata angalau kidogo ili kukusukuma zaidi na kukupa motisha.
Usikae na malengo bila kufanya vitendo, hautafika popote.
.
Uzuri wa vyote hivyo unaweza jifunza, hata kama nyuma ulikua upo upo tu au umefeli kwenye malengo au ulikua unaendeshwa na watu ovyo, unaweza kuamua leo kubadilika na kuanza kuongeza thamani yako kwenye jamii, hivyo usikate tamaa.
 
Yote hayo hili upendwe?
Ukishapendwa unapata faida gani?
Wanaotakiwa kupendwa ni watoto wa kihisia. Wakubwa wanadili na mambo makubwa si ya kitoto kama hayo.
 
Yote hayo hili upendwe?
Ukishapendwa unapata faida gani?
Wanaotakiwa kupendwa ni watoto wa kihisia. Wakubwa wanadili na mambo makubwa si ya kitoto kama hayo.
Suala ni thamani. Kupendwa ni matokeo ya thamani.
 
Yaani unatafuta upewe Thamani na Binadamu uo ni Upumbavu Mkubwa hamna umuhimu wa kufanya kitu chochote kwa ajili ya Binadamu
 
Back
Top Bottom